Meli
kubwa MSC Martina yenye urefu wa mita 244 na upana wa mita 32.2 ikiwa na uwezo
wa kubeba makontena 2,411 imefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es
Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, Mhandisi Madeni Kipande amesema, mafanikio hayo ni
juhudi zilizofanywa na Mamlaka kuzitangaza bandari zake pamoja na uboreshwaji
wa huduma.
“Ujio
huu wa meli kubwa za mizigo kama hizi ni faraja kubwa sana kwetu kwani pia
utaongeza uingiaji wa mizigo kwa wingi na hatimaye kuleta unafuu kwa mtumiaji
wa mwisho,” alisema Mhandisi Kipande. MSC
Martina Kampuni ya Mediterranean Shipping Company (MSC) ni miongoni mwa meli
kubwa na za kisasa ambazo zimefanikiwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es
Salaam na kupakia na kupakua mzigo.
Meli
nyingine kubwa na ya kisasa kuja nchini kwa mara ya kwanza ilikuwa ni Maersk
Cubango mali ya Maersk Line iliyokuwa na urefu wa mita 250 na upana wa mita 38
ikiwa na uwezo wa kubeba kontena 4,500.
Mhandishi
Kipande ameomba ushirikiano uliopo kati ya Mamlaka na mawakala wa meli uendelee
ili kuleta ufanisi zaidi na amewataka mawakala wengine kuleta meli kubwa kama
walivyofanya, Maersk and Mediterranean.
Kwa
upande wake Nahodha aliyeingiza meli hiyo ndani ya Bandari ya Dar es Salaam, Abdulah
Mwingamno alisema mabadiliko ya teknolojia yameongeza uwezo wa Bandari ya Dar
es Salaam kuhudumia meli kubwa zaidi.
“Tuliweza
kuingiza meli yenye urefu wa mita 250 ya kampuni ya Maersk iitwayo Maersk
Cubango na sasa tumeingiza meli nyingine kubwa ya kampuni ya MSC iiitwayo MSC
Martina yenye urefu wa mita 244, haya ni mafakio makubwa kwetu,” alisema.
Nahodha
Mwingamno aliongeza kwamba meli hiyo ya mizigo iliingia salama katika lango la
Bandari ya Dar es Salaam bila tatizo lolote kama ziingiavyo meli nyingine. Alisema
kwamba ujio wa meli hiyo na kufanikiwa kutia nanga katika bandari yetu bila
tatizo lolote ndio kumefungua milango kwa meli hiyo na nyingine za aina hiyo kuanza
safari zake kuja Dar es Salaam.
“Tunatarajia
ujio wa meli kubwa zaidi ya hii yenye urefu wa mita zipatazo 260 katika bandari
yetu kwenye miezi ya Machi na Aprili mwaka huu,” alisema. Naye
mwakilishi wa kampuni ya meli hiyo ya MSC nchini, Ndugu Ahmed Kamal alisema
kwamba wanatarajia kuleta meli kubwa zaidi nchini, kwani kampuni yao ina meli
kubwa zaidi zinazotia nanga katika bandari nyingine Duniani.
“Hii ni
meli kubwa ya kwanza ya kampuni yetu kuja nchini lakini lengo letu ni kuleta
meli kubwa zaidi ya hii nchini,” amesema Kamal.
Meli nyingine kubwa
zaidi zilizowahi kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam zilikuwa na urefu
wa mita 220 na mita 234, zikiwa na uwezo wa kubeba makontena kati ya 2800
na 3000. Awali meli zilizokuwa zinaruhusiwa kuingia katika bandari ya Dar es
Salaam hazikutakiwa kuzidi urefu wa mita 234.
Imetolewa na Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
S.L.P. 9184
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment