Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesema kuwa nishati ya umeme ni
kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo serikali ipo
tayari kushirikiana na wadau mbalimbali
ili kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inakuwa ni ya uhakika.
Simbachawene
aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano
uliokutanisha wadau wa nishati kutoka sekta binafsi, asasi za kiraia na wataalamu
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, katika
hoteli ya Protea jijini Dar es salaam. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni
kubadilishana ujuzi na uzoefu katika
usimamizi wa miradi ya umeme.
Alisema
kuwa, Serikali imekuwa ikiandaa mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha wananchi wote wanapata nishati ya
umeme ya uhakika na kwa gharama nafuu na
kusisitiza kuwa ili kufikia lengo hilo, Serikali
imebuni vyanzo mbalimbali kama vile
umeme wa jua, upepo, tungamotaka,
jotoardhi na gesi asilia
kulingana na Sera ya Nishati ya Mwaka
2003.
“
Umeme wa Gridi ya Taifa pekee hautoshi
kabisa katika kuhakikisha wananchi wote wanaunganishwa na huduma ya umeme ndio maana
Serikali imebuni vyanzo vingine ili
kuhakikisha kuwa yale maeneo ambayo
hayajafikiwa na umeme wa gridi
ya taifa, wanapata umeme na
kupunguza umasikini kupitia nishati hiyo,
“alisema Simbachawene.
Wakati
huohuo, Meneja Uhifadhi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala
ya utunzaji wa mazingira na maisha ya
wanyamapori (WWF; World Wide Fund for
Nature) Nchini Dk. Amani Ngusaru akizungumzia hali ya umeme duniani
alisema kuwa takribani watu bilioni 1.6
hawana nishati ya uhakika ya umeme huku
bilioni 2.4 wakiwa hawana nishati ya uhakika kwa ajili ya kupikia. Aliongeza
kuwa kwa upande wa Tanzania kwa kipindi
cha miaka 10 Serikali imefanya jitihada
mbalimbali katika kuhakikisha inapunguza upungufu wa umeme nchini.
Akizungumzia changamoto katika utekelezaji wa miradi
ya umeme nchini Dk. Ngusari alisema
teknolojia, fedha za uendeshaji na ukosefu wa ujuzi
zinazuia upatikanaji wa umeme wa
uhakika. Akielezea
mchago wa WWF katika nishati ya umeme Dk. Ngusari alieleza kuwa, WWF imekuwa
ikisaidiana na Serikali katika kuongeza
upatikanaji wa nishati mbadala na kuongeza
matumizi ya bayomass.
No comments:
Post a Comment