Redds
Miss Tanzania 2013, Happness Watimanywa (wa pili kushoto), akikata
utepe kuashiria ufunguzi wa Club ya kujisomea watoto ya ijulikanayo kwa
jina la Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Mtaa wa Kasana jirani na
Kituo kinachojengwa kwa ajli ya Mabasi ya Mwendokasi nyuma ya Sheli ya
Mwanamboka katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo, Getrude Kilyabusebu.
Redds
Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa (kushoto), akiwafundisha
kusoma watoto wakati wa hafla ya kufungua Club ya kujisomea watoto ya
Nkema Reading Club iliyopo Kinondoni Dar es Salaam juzi ambapo alikuwa
mgeni rasmi.
Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa akiwa katika picha ya pamoja na watoto na wazazi wao wakati wa hafla hiyo.
Mtoto Careen Elly akimlisha keki maalumu Redds Miss Tanzania, Happnes Watimanywa iliyoandaliwa kwa ufunguzi wa Club hiyo.
Mtoto Kelvin Elly akichora picha mbalimbali kwenye chumba maalumu cha kujisomea watoto ndani ya Club hiyo.
Watoto wakijisomea vitabu mbalimbali ndani ya Club hiyo. Kutoka kushoto ni Hope Njau, Careen Elly na Angel Mtango.
Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu (katikati), akiwafundisha kusoma watoto hao.
Mmoja wa maofisa wa Club hiyo, Hilda Ngaja (kulia), akiwaelekeza jambo watoto hao.
Keki maalumu ya hafla hiyo ilivyokuwa ikionekana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu
(katikati), akizungumza na wazazi watoto hao (hawapo pichani), wakati
wa uzinduzi huo. Kushoto ni Mmoja wa maofisa wa Club hiyo, Rose Kelly
na Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa.
Careen Elly (kulia), akimwelekeza mwenzake namna ya kuandika.
Redds Miss Tanzania 2013, Happyness Watimanywa akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Club hiyo pamoja na wazazi wao.
……………………………………………………………………………………….
Dotto Mwaibale
WAZAZI
wametakiwa kutowaacha watoto wao kucheza baada ya muda wa masomo badala
yake wawapeleke kwenye vituo vya kujisomea ili kupata maarifa zaidi.
Mwito
huo umetolewa na Redds Miss Tanzania 2014, Happyness Watimanywa wakati
wa hafla ya kufungua Club ya watoto ya kujisomea ya Nkema Reading Club
iliyopo Kinondoni Dar es Salaam juzi ambapo alikuwa mgeni rasmi.
“Tunawaomba
wazazi kote nchini wajenge tabia ya kuwapeleka watoto kwenye club za
namna hiyo badala ya kuwaacha wakicheza” alisema Watimanywa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Club hiyo Getrude Kilyabusebu alisema ameamua kuanzisha
clabu hiyo ili kutoa fursa kwa watoto kujifunza mambo mabalimbali ambayo
hawayapati katika shule zao.
“Tunahitaji
watoto wajifunze mambo ya utamaduni wetu badala ya kuiga utamaduni wa
nchi za nje ndio maana tumeanzisha club hii ambayo itakuwa
inawakutanisha watoto siku ya Jumamosi ambapo watakuwa na uwezo wa
kusoma bila kushurutishwa” alisema Kilyabusebu.
Alisema
watoto kushiriki katika club hiyo itawaongeza ujasiri na kujiamini
katika masomo yao na hasa namna ya kujieleza mbele ya watu kwani hapa
nchini kumekuwa na changamoto kubwa ya watoto na hata watu wazima
kujieleza kwa ufasaha kwa lugha ya kiingereza na kiswahili mbele za watu
tofauti na nchi zingine.
Mmoja
wa wazaizi wa watoto hao Hellen Mwenda alisema club kama hiyo
inawasaidia sana watoto kuwajengea uwezo wa kujiamini katika masomo yao
kutokana na kuchanika na watoto wenzao.
Mwenda
alisema pamoja na watoto kujifunza mambo mengine wakiwa shuleni kwao
lakini kwa kuwapeleka katika club hizo wanapata vitabu ambavyo
wanavikosa katika mashule yao.
Club hiyo ipo Kinondoni
jirani na Vijana Social Hall ndani ya Ghorofa kilipo chuo cha Mweni
Training College kwa maelekezo zaidi piga simu namba-0754-032589.
No comments:
Post a Comment