Wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi Iringa wakishiriki kuzima moto katika bweni la wanafunzi wa kike shuleni hapo amnbalo lilikuwa likiwaka moto leo asubuhi |
MOTO mkubwa ambao chanzo chake kinatajwa kuwa ni hitirafu ya umeme umeteketeza bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idodi wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Tukio hilo limetokea muda wa saa 4 asubuhi leo wakati
wanafunzi wakiwa wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Akizungumzia tukio hilo,kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Iringa, InspektaKennedy Komba alisema kuwa bweni hilo limeteketea lote na kuunguza mali zilizoko katika bweni hilo na chache kuokolewa na wananchi waliowahi kufika eneo la tukio kusaidia kuzima moto huo.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo imesababishwa nahitalafu ya umeme na hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa na moto huo. Komba alisema kuwa baada ya jeshi la zimamoto kupata taarifa waliondoka mjini Iringa ambapo ni zaidi ya kilometa 20 hadi ilipo shule hiyo ili kwenda kuzima moto huo.
Hata hivyo aliwapongeza wananchi kwa moyo wa ushujaa kujitolea kuzima moto huo na kuwataka kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapojitokeza katika maeneo yanayowazungu.
“Endapo tungepata taarifa mapema nina amini tungeweza kuokoa vitu vingi zaidi na kuwataka wananchi wasitegemee mtendaji au kiongozi apige simu katika kikosi cha kuzima moto kwani kila mtu ana haki ya kupiga simu 111 katika kitengo cha mawasiliano cha jeshi hilo kuweza kutoa taarifa ya majanga, tumetumia muda mdogo kufika eneo la tukio kutokana ubora wa gari hivyo nawashukuru sana wananchi kwa taarifa na kuweza kuonyesha ushirikiano katika uzimaji wa moto huo usilete madhara zaidi “ alisema Akizungumzia hasara iliyosababishwa ni kiasi gani Komba alisema hadi sasa hawajapata tathmini kamili ya mali zilizoteketea ila baada ya kazi kukamilika itafahamika ni thamani ya vitu vilivyoungua na kuwekwa wazi kwa wanachi.

Mbunge
wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambako maafa hayo yametokea mbali ya kuwapa pore walimu na wananchi wa Idodi kwa tukio hilo bado aliwapongeza wananchi kwa umoja wao kwa kufika mapema
kuthibiti moto huo pamoja na kikosi cha Zimamoto kutoka mjiniIringa.
Tukio hilo kubwa kulikumba jimbo la Isimani linaloongozwa na mbunge wake Wiliam Lukuvi ambae ni waziri wa nyumba na ardhi
Akizungumza kwa niaba ya mbunge Lukuvi katibu wa mbunge huyo Thom Malenga alisema kuwa wananchi wamefanyajitihada kubwa katika kuthibiti
moto huo na kuwa mbali ya mali za wanafunzi hakuna madhara kwa binadamu.
Kuhusu thamani ya mali zilizoteketea kwa moto huo alisema kwa sasa bado mapema kujua ila uongozi wa shule hiyo pamoja na wazazi na
wananchi wa Idodi wapo katika kikao ili kujua madhara zaidi na hasara iliyojitokeza.
Agosti 25/ 2009 jumla ya wanafunzi 13 walipoteza maisha baada ya bweni hilo kuteketea kwa moto na baadhi yao kujeruhiwa kwa ajali kama hiyo ya moto ambayo kwa kipindi hicho moto huo ulisababishwa na mshumaa.
No comments:
Post a Comment