Mkuu wa vipindi wa East Africa Radio, Nasser Kingu (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua kampeni ya Zamu yako 2015, Kulia kwake ni Mkuu wa Masoko Eatv & East Africa Radio, Alex Galinoma
KITUO cha Televisheni chenye ushawishi mkubwa kwa vijana nchini Tanzania, EATV, sambamba na kituo chake cha East Africa Radio, mapema leo wamezindua rasmi kampeni kubwa na ya aina yake ijulikanayo kwa jina la ZAMU YAKO 2015.
Akizungumza
na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa vipindi East Africa
Radio, Nasser Kingu alibainisha kampeni hiyo inamalengo mahususi kwa
Taifa ikiwemo vijana kwa ujumla juu ya kuwakumbusha na kuwaelimisha
vijana kuhusiana na umuhimu pamoja na uwezo walionao katika kufanya
maamuzi sahihi kwenye masuala makubwa ya kitaifa hususani yanayohusu
siasa za Tanzania.
“Kampeni hii ina dhamira ya kuhimiza vijana kutumia fursa waliyonayo katika kufanya maamuzi na mambo mbalimbali.
Kwanza
kushiriki kikamilifu katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la
kudumu la wapiga kura ya maoni katika mchakato wa kutafuta katiba mpya,
na mwisho kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura ili kuchagua
viongozi wao ambao ni madiwani, wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania” alibainisha Kingu.
Aidha
Kingu alisema EATV na East Africa Radio, imekuwa na mvuto mkubwa sana
kwa vijana hivyo lengo la kampeni hiyo itafanikiwa kwani inawalenga na
kuwagusa moja kwa moja vijana.
Kingu
pia aliweza kutoa takwimu kadhaa, ambapo alisema kwa Tanzania, umri
rasmi wa kupiga kura ni kuanzia miaka 18 na kuendelea, kwa mujibu wa
sense ya mwaka 2012, Jumla ya watu Milioni 22, (22,424,136)
wanatazamiwa kushiriki zoezi hilo kwa mwaka huu.
“Katika
idadi hiyo ya wapiga kura, vijana wenye umri wa miaka 18 mpaka 40 peke
yao ni 15,293,681. Idadi ambayo ni sawa na asilimia 68.20 ya wapiga
kura wote.
Hii
ina maanisha kwamba hatma ama mustakabali wa Taifa hili uko mikononi
mwa vijana. Na ndio maana vituo vyetu Tv na Radio vinaaminika zaidi na
vijana, hivyo tunaendesha kampeni hii kwa kutambua umuhimu na nguvu ya
vijana katika taifa letu.
Ikumbukwe
pia hii si mara ya kwanza kwa vituo vyetu kuwa na kampeni kama hii,
mwaka 2010, tulikuwa na kampeni ya kuwataka vijana kuacha kulalamika na
kutumia kura yao” alifafanua Kingu.
Kampeni
hiyo inatarajiwa kufanywa na vituo hivyo kupitia vipindi vyao
mbalimbali kila siku, ikiwemo kufanya mahojiano na wananchi, vijana,
vingozi wanasiasa, watu maalufu na wengineo wengi ambao pia watakuwa
wakialikwa kwenye studio za vipindi vya vituo hivyo, kwa zaidi ya mwaka
mzima.
No comments:
Post a Comment