Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen,
Christoph Gogler, (wapili kushoto0, akimkabidhi mfano wa hundi ya euro
2,000, mkurugenzi mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi katika hafla fupi
iliyofanyika makao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatanoi Feb 12,
2015. Benki hiyo YA kIJERUMANI NA tpb, pia wamesaini makubaliano ya
ushirikiano baina yao.
Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, (Kulia), na Ofisa Mtendaji
Mkuu wa Benki ya Kijerumani ya Kreissparkasse Tubingen, Christoph Gogler
wakitia saini makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili za
kifedha malao makuu ya TPB, jijini Dar es Salaam, Jumatano Feb. 11,
2015. Ujerumani itakuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa TPB ili
kuwajengea uwezo katika fani mablimbali hususan kitengo cha huduma kwa
wateja. Pia taasisi hiyo imeipatia TPB EURO 2,000 kwa madhumuni hayo
hayo.
Mwanasheria wa TPB, Mystica Mapunda Ngongi, (Kulia) na mwakilishi na
msauri wa taasisi ya Kijerumani ya SBFIC, Clause Thiele, wakisaini ili
kuthibitisha makubaliano hayo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi
(wapili kulia) akipokea hundi yenye thamani ya Euro 2,000 kutoka kwa
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman, Dk.
Christoph Gögler. Fedha hizo ni kwaajili ya kuendeshea mafunzo kwa
wafanyakazi wa Benki hiyo, kulia ni Mwakilishi wa Benki hiyo, Claus
Thiece na kulia kwae ni Meneja Rasilimali watu wa TPB, Peter Mapigano.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman,
Dk. Christoph Gögler (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi wakisaini hati ya makubaliano ya
ushirikiano wa taasisi hizo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Kreissparkasse Tübingen ya Ujeruman,
Dk. Christoph Gögler (kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla ya
ukabidhi hundi yenye thamani ya Euro 2,000 kwa Benki ya Posta Tanzania
(TPB) leo Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta
Tanzania, Sabasaba Moshingi.
No comments:
Post a Comment