Na Masanja Mabula -Pemba .
Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni Jabu Khamis Mbwana amewataka masheha kutoingia mikataba ya
uuzaji au utoaji wa ardhi katika maeneo yao bila ya kuiarifu Serikali
ya Wilaya lengo ni kuzuia migogoro ya ardhi .
Akizungumza na masheha
wa Wilaya hiyo huko Ofisini kwake Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa
iwapo masheha watajiepusha na mikataba hiyo migogoro ya ardhi ambayo
inaikabili jamii inaweza kupungua .
Amefahamisha kwamba ni
kosa kwa Sheha kujichujkulia uwamuzi wa kuingia mkataba wa kuuza ardhi
na kufahamisha kuwa Serikali ya Wilaya haitokuwa tayari kumvulia Sheha
ambaye atasababisha mgogoro kwa kuingia mtakaba ya aina hiyo .
“Ili kujiepusha na
migogoro ya ardhi katika shehia zenu , jiepusheni kuingia mikataba ya
kuuza au kutoa ardhi na kwa ahili Serikali ya Wilaya haitakuwa kubeba
mzigo kwa kumtetea sheha atakayesababisha mgogoro ya ardhi ”
alifahamisha .
Aidha Mkuu wa Wilaya
amewataka masheha katika Wilaya hiyo kufanya kazi kwa mujibu wa sharia
na kuhakikisha kwamba wanawatumikia wananchi wote bila ya kujali itikadi
za vyama , rangi , dini wala kabila .
Amesema kuwa sheha
anajukumu la kutenmda haki kwa wananchi katika shehai yake na
kuwasisitiza kutumia lugha ya hekima na busara wakati wanapo watumukia
wananchi ili kujenga imani na matumani kwa raia na Serikali yao .
“Fanyeni Haki na
Uadilifu kwa wananchi wote katika shehia zenu , pia tumieni lugha za
hekima na busara wakati mnapotoa huduma na hii itawafanya wananchi
waongeze imani na matumani kwa Serikali yao ” alieleza Jabu .
Naye Afisa Tawala wa
Wilaya hiyo Ahmed Khalid Abdalla amesema kuwa ni vyema masheha
kuwasiliana na Ofisi ya Wilaya ili kupata maelekezo yanayofaa na kuacha
kukurupuka kuingia mikataba ambayo inakuwa na athari kwa siku za baadaye
.
“Acheni kukurupuka
kuingia mikataba , ni vyema mkawasiliana na Ofisi ya Wilaya ili kupata
maelekezo sahihi ambapo kwa kufanya hivyo kutazuia kutokea migogoro ya
ardhi katika Shehia zenu ” alisisitiza Ahmed .
Akiizungumzia hotuba
hiyo Sheha wa Shehia ya Mihogoni Salim Said amewataka masheha kuwa
waadilifu kwa kujiepusha na vitendo ambavyo zinaweza kusababisha
migogoro ikiwemo masuala ya uuzaji wa Ardhi hasa za mashamba ya Serikali
.
No comments:
Post a Comment