WAANDAAJI
wa Tamasha la Pasaka wamesema wataendelea kusaidia jamii katika kila tamasha
lao litakapofanyika.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ilieleza kuwa kwa miaka
yote hiyo wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii.
"Tumedhamiria
kwa dhati kusaidia jamii kwa namna mbalimbali, hii haitakuwa mara ya kwanza
kwetu kufanya hivyo, tulisaidia matamasha yaliyopita, tutaendelea na juhudi
hizo kila tutakapopata nafasi, “ alisema Msama katika taarifa hiyo.
Alisema
katika miaka yao 15 wamesaidia sehemu mbalimbali ikiwemo waathirika wa mabomu
yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
Pia alisema Tamasha la Pasaka wamewahi kusaidia fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane. “Tangu mwanzo tulishajionesha kwamba tuna dhamira ya dhati na ndio maana tunafurahia sana kila mwaka kwamba nasi tunashirikiana na jamii na hata mwaka huu tutafanya hivyo,” alisema Msama.
Pia
alisema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali wamekuwa wakitoa semina za
kusaidia wajane, yatima na vijana wasio na ajira ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kufanya
biashara na kuachana na dawa za kulevya.
"Mimi naamini mtoaji wa vyote ni Mwenyezi Mungu, hivyo ni busara upatapo kidogo ugawane na wasiojiweza ili kuongeza thawabu yako.
No comments:
Post a Comment