“NILIAMUA
kuanzisha Msama Promotions baada ya kuona muziki wa Injili umesahaulika
na unashuka thamani yake.“Hivyo kwa kushirikiana na wenzangu nikaona ni
busara kuuinua ili tuwe kama wenzetu Afrika Kusini ambao wana waimbaji
wa nyimbo za Injili wanaotamba kama Rebecca Malope, Itani Madima, Steve
Kekane, Vuyo Mokoena na wengine wengi,” hiyo ni kauli ya Mkurugenzi wa
Msama Promotions, Alex Msama.
Msama
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka,
anasema alitaka watu wajue na kutambua kuwa muziki wa Injili
unaweza kupigwa kama burudani katika kumbi mbalimbali za starehe na
kuondoa dhana potofu kwamba muziki huo wa Injili haufai kupigwa katika
kumbi hizo.
“Kupeleka
muziki wa Injili kwenye kumbi ambazo hupigwa muziki wa miondoko mingine
ya kidunia si dhambi kama baadhi ya watu wanavyofikiri,”
anasema.Anasema ni zaidi ya miaka 15 tangu walipoanzisha Tamasha la
Pasaka wakati wa sikukuu hiyo kila mwaka na sasa jamii imelikubali na
limekuwa gumzo kubwa kwa jamii.
Anasema
pia dhamira yao nyingine ya kuanzisha tamasha hilo ilikuwa kusaidia
jamii kwa namna mbalimbali kutokana na fedha za viingilio, lakini pia
kuwapa ajira vijana kutokana na tamasha hilo.“Ninachoweza kusema ni
kwamba mwaka huu tumedhamiria kwa dhati kusaidia jamii kwa namna
mbalimbali kutokana na fedha zitakazopatikana kwenye viingilio vya
tamasha.
“Haitakuwa
mara ya kwanza kwetu kusaidia, tumefanya hivyo miaka ya nyuma na
tutaendelea na juhudi hizo kila tutakapopata nafasi ya kufanya hivyo, “
anasema.Anatolea mfano kuwa miaka ya nyuma wamesaidia watu mbalimbali
ikiwemo waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la
Mboto, Dar es Salaam. Pia anasema wamepata kutoa fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.
Msama
anabainisha kwamba kutokana na dhamira hiyo, ndiyo maana wamekuwa
mstari wa mbele kuandaa matamasha ya muziki wa Injili, lengo likiwa ni
kusaidia masuala mbalimbali.Anasema mwanzoni wakati wanaanza tamasha
hilo mwaka 2000, wamewahi kuandaa matamasha kwenye ukumbi wa
Diamond Jubilee kwa ajili ya kuchangia watoto yatima wa mikoa ya
Morogoro na Pwani, ambao wazazi wao walifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi,
ambapo yote waliyopanga yalifanikiwa.
Pia
anasema fedha wanazopata wamekuwa wakitumia kusomesha yatima na
kuwatafutia ajira mbalimbali wasiojiweza ikiwa ni pamoja na wengine
kupata mafunzo ya kunadi vitu kupitia kampuni yake ya udalali ya Msama
Auction Mart. Mkurugenzi huyo anasema mpaka sasa wanasomesha wanafunzi
katika shule mbalimbali Dar es Salaam.
Pia
anasema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali wamekuwa wakitoa
semina za kusaidia wajane, yatima na vijana wasio na ajira ikiwa ni
pamoja na kuwapa mbinu za kufanya biashara na kuachana na dawa za
kulevya.
Anasema wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha huduma wanazotoa zinawafikia walengwa.
“Mimi naamini mtoaji wa vyote ni Mwenyezi Mungu, hivyo ni busara upatapo kidogo ugawane na wasiojiweza ili kuongeza thawabu zako.
“Ndiyo maana tumekuwa tukijitolea kuwasaidia wasiojiweza ikiwa ni pamoja na kuwasomesha yatima na wasiojiweza na tumekuwa mstari wa mbele kutoa ajira kwa baadhi ya vijana wa Tanzania,” anasema.
Mkurugenzi
huyo wa kampuni hiyo iliyo mstari wa mbele kuinua muziki wa
Injili nchini, anawaasa vijana kuwa na moyo wa ujasiri na uvumilivu na
wa kupenda kujituma kufanya kazi ili kufikia lengo la kupiga hatua
kimaendeleo.Anasema vijana wengi wamekuwa wakipenda kukaa na kubweteka
badala ya kufanya kazi na kuwa wabunifu.
“Binafsi sipendi maendeleo yangu peke yangu, bali napenda pia kuwa mstari wa mbele kushirikiana na wenzangu,” anasema.
Kuhusiana
na tamasha lenyewe anatamba kuwa wamewaandalia mashabiki wa muziki wa
Injili mambo mazuri yatakayowaburudisha na kuridhika.Anaeleza kuwa
tamasha la mwaka huu 2015 ambalo lipo katika hatua za awali za
maandalizi litafana kwa vile kutakuwa na waimbaji wengi wa muziki wa
Injili watakaowapa mashabiki vionjo mbalimbali.
Anasema
anatarajia tamasha hilo litahudhuriwa na maaskofu wa
madhehebu mbalimbali aliosema wameanza kufanya mazungumzo na baadhi yao,
ambao wapo katika kamati yake ya maandalizi.
Anajinasibu kuwa tamasha hilo litafana kwa vile kutakuwa na
waimbaji wengi wa muziki wa Injili watakaowapa mashabiki vionjo mbalimbali.
waimbaji wengi wa muziki wa Injili watakaowapa mashabiki vionjo mbalimbali.
Kwa
mujibu wa Msama, mpaka sasa wadau wa muziki wa Injili wa mikoa ya
Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma, Tanga, Dar es Salaam, Mtwara, Shinyanga
na Zanzibar ndiyo ambao wameomba kufanyika tamasha hilo mikoani mwao.
“Tutaheshimu
mno maoni ya wapenzi wa tamasha hili kutoka sehemu mbalimbali na kila
watakalotushauri tutalifanyia kazi, lengo kubwa ni kiboresha tamasha
letu,” anasema Msama.Pia Msama anasema, kampuni yake ipo katika mkakati
wa kujenga kiwanda cha kisasa kwa ajili ya kuzalisha bidhaa
zinazohusiana na kazi za wasanii.
No comments:
Post a Comment