TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, December 11, 2015
ASKARI 482 WA JESHI LA ZIMAMOTO WAHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA FANI HIYO
TANGAZO
UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
WASHINGTON, D.C.
TANGAZO
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi anawakaribisha Watanzania wote na Wamarekani wenye asili ya Kitanzania kwenye mkutano mfupi wa kufahamiana utakaofanyika tarehe 12 Desemba, 2015.
Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Tabeer uliopo 1401 University Boulevard, Hyattsville Maryland 20783, kuanzia saa tisa hadi saa kumi na moja jioni (3:00pm – 5:00pm).
Wote mnakaribishwa, na tafadhali zingatieni muda.
MISSY TEMEKE ALIVYONOGESHA USIKU WA ANNE KANSIIME
Mbunifu wa vivazi vya KWETU Fashion Missy Temeke (kati) akipata ukodak moment na walimbende wake siku ya Ijumaa Novemba 27, 2015 alipofanya onensho la vivazi vya kampuni yake na kunogesha show ya mchekeshaji maarufu kutoka Uganda Anne Kansiime alipowavunja mbavu wanaDMV katika kusherehekea wiki ya Thanksgiving.
BARAZA JIPYA LA MAWAZI LA RAIS MAGUFULI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.
BARAZA LA MAWAZIRI
MWANAMUZIKI ROBERTO AMARULA KUTOKA ZAMBIA KUTUMBUIZA DAR ES SALAAM, DODOMA KATIKA TAMASHA LA INSTAGRAM
Mwanamuziki na mtangazaji wa redio, Roberto Chindaba Banda 'maarufu Roberto Amarula kutoka nchini Zambia (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu onyesho lake atakalolifanya leo katikka fukwe za Escape One Mikocheni jijini Dar es Salaam na kesho ukumbi wa Ngalawa Pub mkoani Dodoma katika Tamasha la Instagram Party Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Freconic Ideaz, Fred Ngimba ambao wamemleta msanii huyo hapa nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya C&G Solutions na kulia ni Mwanamuzi David Banda 'General Ozzy kutoka Zambia.
Na Dotto Mwaibale
MWANAMUZIKI wa Zambia anayetamba na wimbo maarufu wa Amarula, Robert Banda ‘Roberto Amarula’, kesho anatarajia kufanya shoo kubwa na ya aina yake katika Ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya hivyo mjini Dodoma kesho kutwa.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR, BALOZI SEIF ASIMAMISHA UJENZI WA NYUMBA YA GHOROFA MJINI UNGUJA, ZANZIBAR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemuagiza Mmiliki wa Kiwanja kinachotaka kujengwa Nyumba ya Ghorofa katika Mtaa wa Mlandege Bwana Anuari Abdulla kusitisha mara moja ujenzi huo. Hatua hiyo ya Balozi Seif imekuja kufuatia malalamiko makubwa yaliyotolewa na wakaazi wa Mtaa huo wakimshutumu Mmiliki huyo kuvamia pia .Balozi Seif akipokea malalamiko ya Wakaazi wa Mtaa wa Mlandege wakimshutumu Mmiliki wa Kiwanja cha jengo la Ghorofa Bwana Anuari Abdulla anayejenga pamoja na eneo la wazi.
DROO YA PILI YA PROMOSHENI YA "JAZA MAFUTA NA USHINDE" KUTOKA GAPCO YACHEZESHWA
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Rashid Khalfan (kulia) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya pili ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo na kusimamiwa na Mkaguzi wa Michezo ya kubahatisha nchini, Abdallah Hemedy (kushoto). katikati ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.
Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za SADC wahitimishwa jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Bw. Assah Mwambene akifunga Mkutano wa 10 wa uhamaji kutoka mfumo wa Analogia kwenda Digitali kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo. Tanzania imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada ya kuonekana kufanya vizuri katika uhamaji wa matumizi ya mfumo wa analogia kwenda digitali kwa wakati.
Rebeca Malope kutikisa Diamond Tamasha la Krismasi
Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili barani Afrika, Rebecca Malope ambaye ni raia wa Afrika Kusini anatarajia kuongeza nguvu katika Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama muimbaji huyo atakuwa jukwaa moja na wenzake Sarah K wa Kenya na Ephraim Sekeleti wa Zambia ambao watafikisha shukrani za Watanzania baada ya kufanya uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Kinondoni Revival yachomoza Tamasha la Krismasi
Na Mwandishi Wetu
KWAYA mahiri ya nyimbo za Injili, Kinondoni Revival ni mojawapo ya watakaosindikiza Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea kufanyika kupitia kamati yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)