TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, June 11, 2016

Rais Magufuli afanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri

BoT yatoa Sh. Milioni 273 kuchangia ununuzi wa madawati nchini.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AONGOZA MATEMBEZI YA WAFANYAKAZI WA BENKI KUU.

WANACHAMA WA YANGA WAPIGA KURA HII LEO KUWACHAGUA VIONGOZI WAO KWA AMANI NA UTULIVU

BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA TTB YAFANYA MKUTANO KWA MARA YA KWANZA





MASAUNI ATOA RAMBIRAMBI KWA WAKE WA WALIOUAWA MSIKITINI.

 Mzee wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati (kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo makini na linaendelea kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

SERIKALI YATANGAZA UTARATIBU MPYA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, PIA YAFAFANUA FEDHA ZILIZOOKOLEWA KUTOKANA NA WATUMISHI HEWA

SERIKALI HAITAMVUMILIA KIONGOZI YEYOTE ATAKAYEDONOA FEDHA ZA MICHANGO YA MADAWATI-WAZIRI MKUU MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itamchukua hatua kiongozi yeyote atakayedonoa fedha za michango ya madawati inayotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo. Pia amewaagiza watendaji wote wa Serikali, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maofisa Elimu, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa, kuhakikisha michango hiyo inayotolewa inawafikia walengwa. Aidha, amezitaka wilaya zote nchini zianzishe mpango endelevu wa kuhakikisha kwamba upungufu wa madawati unasahaulika kabisa katika maeneo yao na kwamba utendaji wa viongozi wa elimu na Serikali katika ngazi mbalimbali utapimwa kutokana na jinsi ambavyo wametekeleza maagizo hayo. Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati wa matembezi ya hisani ya kukusanya fedha za kununulia madawati kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Katika maadhimisho hayo yaliyoanzia BOT hadi viwanjja vya Mnazi Mmoja, Gavana wa BOT, Profesa Benno Ndulu alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya shilingi milioni 263 zilizochangwa na benki hiyo pamoja na watumishi wake kama mchango wao kwa ajili ya ununuzi wa madawati. Waziri Mkuu aliwapongeza watumishi wa BOT kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto hiyo ambapo alitoa wito kwa taasisi zote katika sekta ya umma na binafsi pamoja na watu binafsi kuchangia uboreshaji wa elimu nchini kama sehemu ya “Majukumu ya Taasisi kwa Jamii” (Corporate Social Responsibility). Amesema kuwa na elimu bora, siyo tu faida kwa Taifa, bali kwa waajiri pia, kwani itahakikisha kwamba taasisi za umma na binafsi zinapata wafanyakazi ambao wameiva na wenye weledi wa kutekeleza majukumu mbalimbali ya uzalishaji katika taasisi hizo. “Nitoe wito pia kwa wanafunzi wote ambao watafaidika na kuboreshwa kwa mazingira ya kusomea, ikiwemo kupewa madawati na mahitaji mengine, kuhakikisha wanasoma kwa bidii kwa faida yao na Taifa kwa ujumla na kwa kufanya hivyo, wanafunzi watakuwa wanaenzi jitihada za Serikali, taasisi za umma, taasisi binafsi na watu binafsi katika kuboresha elimu nchini,” amesema. Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kupambana na changamoto za sekta ya elimu na kwamba tangu Uhuru, Serikali za Awamu zote zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali katika kuboresha elimu kwa wananchi wake. IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU 2 MTAA WA MAGOGONI, S. L. P. 3021, 11410 DAR ES SALAAM

Wabunge watakiwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji na usimamizi wa matumizi ya fedha za Umma.











WAZIRI MKUU MAJALIWA: UHABA WA SUKARI KUMALIZIKA NCHINI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali inaendelea na jitihada za kuondoa tatizo la uhaba wa sukari nchini ambapo jumla ya tani 20,000 zilisambazwa jana katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema shehena nyingine ya tani 35,000 inatarajiwa kusambazwa hivi karibuni katika kanda zote nchini hivyo amewataka wafanyabiashara watakapoipokea kuiuza kwa wananchi bila ya kuificha na bei isizidi shilingi 2,200.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jana jioni ( Ijumaa, Juni 10, 2016) wakati akizungumza na Masheikh na Viongozi wa Kamati ya Amani ya mkoa wa Dar es Salaam alipowaalika katika futari aliyoiandaa nyumbani kwake.

Amesema tayari viwanda vimeanza kufunguliwa na tani 300 zilizotoka katika kiwanda cha Sukari cha Kagera zitasambazwa katika wilaya za Kakonko, Kibondo, Kasulu, Uvinza na Kigoma ili kutosheleza maeneo hayo.

Hata hivyo amewataka Maofisa Biashara katika Halmashauri zote nchini kuendelea kufanya ufuatiliaji katika maduka ili kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana na hakuna mfanyabiashara atakayeificha.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwataka wafanyabiashara kote nchini kutopandisha bei za vyakula katika kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza kuhusu tabia za baadhi ya wafanyabiashara wanaopandisha bei za bidhaa hasa vyakula katika kipindi hiki cha mfungo amewataka kumuogopa Mwenyezi Mungu kwa sababu kitendo hicho kinawapa wafungaji wakati mgumu.

“Kufunga Ramadhani si jambo la anasa, si matashi binafsi bali ni jambo la kiimani hivyo tusipandishe bei ya bidhaa kwa lengo la kuwaadhibu Waislam kwa sababu tu wamefunga.

“Katika Quran surat Baqarah aya ya 183 inasema kwamba enyi mlioamin imefaradhishwa kwenu kufunga kama walivyoamrishwa kufunga kwa waliopita kabla yenu ili muwe wachamungu, hivyo hatuna budi kufunga” alisisitiza.

Alisema tabia hiyo si nzuri na imekuwa ikijitokeza mara kwa mara unapofika wakati wa mfungo kwa wafanyabiashara kuamua kupandisha bei hivyo aliwataka waiache kwani Serikali haitawavumilia na atakayethubutu hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU 2 MTAA WA MAGOGONI, S. L. P. 3021, 11410 DAR ES SALAAM

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUTARISHA

JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KODI VYUONI YAFUNGULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

UCHAGUZI WA YANGA- HAPA WANANCHAMA WAKIWA WANAENDELEA KUSUBIRI KUWACHAGUA VIONGOZI WAO WAPYA KWENYE UKUMBWA DIAMOND


MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, ATEMBELEA KITUO CHA POLISI KILICHOLALAMIKIWA BUNGENI

LWENGE ATAKA WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA MAJI WASHTAKIWE KWA KOSA LA UHUJU UCHUMI

Keri Hilson Atua nchini Nigeria kwa fainali za mashindano Airtel Trace Music Stars Afrika

MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

Friday, June 10, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI PAMOJA NA JAJI KIONGOZI, PIA AAGANA NA BALOZI WA OMAN ANAYEMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI.

UPINZANI WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ZA KUBANA MATUMIZI

Watanzania waombwa kushiriki siku ya Mtoto wa Afrika.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI DODOMA

NIDA YAANZA KUTOA VITAMBULISHO VYENYE SAINI

Picha na Fatma Salum (MAELEZO).


Frank Mvungi-Maelezo

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kutoa vitambulisho vya Taifa vyenye saini ya mwombaji kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. 

Makonda kuzindua maonyesho ya kwanza ya simu Original (Simu Expo).

MPALULEBLOGS:Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda atazindua maonyesho ya kwanza ya simu original katika viwanja vya Posta jumamosi ya Tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni.

Lengo kuu la kufanyika kwa maonyesho hayo ni kuwapa elimu wateja wa simu kujua ipi ni simu fake na ipi ni original kutoka kwa makampuni hayo ya simu,pia kwa kushirikiana na TCRA watatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya simu na mitandao ya kijamii.

Lengo la tatu ni kuhakikisha wateja wanajipatia simu original kwa bei nafuu kabla ya simu fake kuzimwa tarehe 16 mwezi huu.Nae Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano(TCRA-CCC),Mary Msuya amewashauri watumiaji wa simu nchini kununua simu katika maduka ya simu na kuomba risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.

Halmashauri ya Mji wa Kibaha yakamilisha miradi mitano ya maji






BEST -"NASSO UKWELI UKO WAPI"?


INTERNEWS yawafunda waandishi sheria ya ardhi




BARABARA DODOMA MAYAMAYA KUKAMILIKA OKTOBA MWAKA HUU

Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja nchini (PBPA) yazinduliwa jijini Dar leo

SERIKALI: MFUMO WA MALIPO YA UZEENI UPO MBIONI KUANZA

Naibu Waziri akutana na Ujumbe wa UNDP

MPI2Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya mazungumzo baina yao.
…………………………………………………………………………………………………
Na Lulu Mussa
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. Luhaga Mpina hii leo amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo pamoja na ujumbe aliombatana nao, Ofisini kwake Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao ujumbe huo umeonyesha nia ya kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Makamu wa Rais hususan katika nyanja ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kupambana na mabadiliko ya Tabianchi na nishati mbadala.

UZINDUZI WA HOTEL YA KISASA KUSILE RESTAURANT AND LODGE MJINI MBINGAULIOFANYIKA NA MWENGE WA UHURU 2016.

WATOTO WALIOZALIWA NA MAMBUKIZI YA VVU MATUMAINI DODOMA, WAITAKA JAMII KUWAKUMBUKA

AMKA NA BBC Juni 10, 2016......Obama atangaza rasmi kumuunga mkono Hillary Clinton

SERIKALI YA TANZANIA NA ZAMBIA ZASAINI MAKUBALIANO YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MISITU NA MAGOGO KUPITIA MIPAKA YA NCHI HIZO

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA UTAPELI WILAYANI NYAMAGANA.