SERIKALI YAPATA GAWIO LA SH. BILIONI 23 KUTOKA KAMPUNI ZA PUMA ENERGY, TIPER (T) na NMB BANK PLC
hazitoi
gawio zikisingizia kupata hasara kwenye biashara wakati hawafungi
biashara hizo" Alisisitiza Dk. Mpango Dk. Mpango pia amevitaka vyombo
vya dola kufanya uchunguzi, ili kubaini mianya ya upotevu wa mafuta
bandarini na kuagiza wale wote walihusika na upotevu huo wachukuliwe
hatua. " Haiwezekani wajanja wachache wanafaidika halafu wananchi
wanyonge wanalala chini hospitalini, Nilisema jana na leo narudia yeyote
anayetukwamisha kwenye maendeleo ni msaliti lazima washughulikiwe kwa
mujibu wa sheria bila huruma,” alisema. Awali Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dk. Medard Kalemani, amezipongeza kampuni hizo kwa kutoa gawio
hilo na kumhakikishia Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango,
kuwa gawio litaongezeka kwa kasi kubwa katika miaka ijayo ili kuiwezesha
serikali kuwa na uwezo zaidi wa kuwahudumia wananchi. “Mwaka 2014
tulipata gawio la Sh bilioni 3 kutoka Kampuni ya PUMA Energy, mwaka huu
tumepata bilioni 4.5 ni matarajio ya Serikali kwa mwendo huu mwakani
tunaweza kupata bilioni 6" alisema Dkt. Kalemani. Alitoa wito pia kwa
kampuni nyingine zenye ubia na Serikali ambazo hazitoi gawio zianze sasa
kutoa akieleza kuwa mantiki ya gawio ni kwamba kampuni inafanya kazi na
inapata faida, inapokuwa haitoi gawio mantiki yake ni kwamba kampuni
inafanya kazi haipati faida. “Lakini ni vigumu kuamini kama kampuni
hazipati faida kwa mfululizo wa miaka 10 na inafanya kazi, sisi
tunaamini wanapata faida, na zipo kampuni nyingi ambazo si busara
kuzitaja hapa zinadai kupata hasara kila mwaka,” alisema. Kuhusu upotevu
wa mafuta bandarini, Dk. Kalemani alisema tatizo hilo hivi sasa
limedhibitiwa, baada ya Serikali kuanzisha chombo maalumu kinachoratibu
na kudhibiti upotevu huo. Alikuwa akijibu changamoto iliyotolewa na
Mwenyekiti wa Bodi ya Puma Energy, Dkt. Ben Moshi, aliyeelezea kuwa
katika kipindi cha mwaka 2014/2015 kampuni hiyo imepata hasara ya Dola
za Marekani milioni 1.4 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 2.5 kutokana na
upotevu huo wa mafuta. Kwaupande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Kampuni ya Tiper (T), inayojihusisha na uhifadhi wa mafuta, ambapo
amesema tangu mwaka 2010, kampuni hiyo imetoa gawio la shilingi Bil. 6.4
kwa serikali na kuahidi kuwa gawio hilo litaongezeka siku za usoni.
Naye Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, amesema kuwa benki
yake inajisikia fahari kubwa kugawa faida iliyopata katika biashara zake
kwa mbia wake ambaye ni serikali. Amesema kuwa pamoja na serikali kuwa
mbia kwa hisa ya asilimia 31.8, lakini pia ni mteja mkubwa wa benki hiyo
ambayo hurudisha faida ya uwekezaji kwa wananchi kupitia gawio hilo na
kutoa wito kwa watanzania kuitumia benki hiyo kuweka amana na kukopa
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji,
Charles Mwijage ambaye ametoa wito kwa wawekezaji wakiwemo wale
wanaofanya biashara zao kwa kushirikiana na serikali kufanyakazi zao kwa
uaminifu kwa kutangaza faida wanazopata kihalali ili serikali iweze
kupata mapato yake yatakayosaidia kuboresha maisha ya wananchi Naye
Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru, ameahidi kuyafuatilia na kuyasimamia
mashirika yote ya umma na yale ambayo serikali imewekeza, ili
kuhakikisha kuwa hawakwepi kulipa gawio ili kuiwezesha serikali kupata
mapato yake Imetolewa na Benny Mwaipaja Kaimu Msemaji wa Wizara ya Fedha
na Mipango 0787087878
No comments:
Post a Comment