BoT yatoa Sh. Milioni 273 kuchangia ununuzi wa madawati nchini.
Fedha
hizo zilikabidhiwa leo kupitia hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa baada ya matembezi ya hisani yaliyolenga kuchangia madawati,
yaliyoanzia Ofisi za BOT hadi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar
es Salaam.Akizungumza kabla ya kukabidhi fedha hizo, Gavana wa BOT
Prof. Benno Ndulu alisema lengo la mchango huo ni kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano katika kuongeza ubora wa elimu kupitia
upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini.
“Tunatambua
kwamba changamoto hiyo (uhaba wa madawati) ni kubwa, lakini tunaamini
mchango wetu utasaidia kupunguza makali ya tatizo hilo na kuongeza idadi
ya watoto wetu ambao wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati” alisema
Gavana Prof. Ndulu.
Alitaja
mikoa hiyo na fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa BOT wa matawi ya
mikoa hiyo kuwa ni Makao Makuu Dar es Salaam waliochangia Shilingi
Milioni 22, Mwanza (Milioni 1.24), Chuo cha Benki Mwanza (680,000)
Arusha (Milioni 1.23) Mbeya (Milioni 1.186), Mtwara (850,000) na Dodoma
(Milioni 1.18).
Alisema taasisi zilizochangia fedha hizo ni Benki
ya India Shilingi Milioni 5, Benki ya Habib (Milioni 5), Benki ya Exim
(Milioni 5), Benki ya UBA (United Bank for Africa, Milioni 2), Tanzania
Mortgage Refinance (Milioni 2), China Community Bank (Milioni 2) na NIC
Bank aliyotoa Milioni 1.
Kwa upande wa kampuni za simu zilizotoa
fedha ni kampuni ya Vodacom iliyotoa Dola za Kimarekani 10,000, kampuni
ya Tigo Dola za Kimarekani 10,000 na kampuni ya Selcom iliyotoa Dola za
Kimarekani 5,000.
Akizungumza baada ya kupokea hundi ya mfano,
Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza fedha hizo zitumike kama
zilivyokusudiwa na yeyote atakayetumia fedha hizo kinyume na malengo
achukuliwe hatua mara moja.Katika kuthamini sekta ya elimu nchini,
Gavana Prof. Ndulu alisema benki hiyo ilianzisha Mfuko wa Udhamini wa
Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo hadi sasa umetoa ufadhili kwa
wanafunzi 22 kusoma shahada za kwanza na za uzamivu katika vyuo vikuu
hapa nchini katika masomo ya sayansi, hisabati, uchumi, fedha, uhasibu
na TEHAMA.
No comments:
Post a Comment