MWAKILISHI
wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum pia ni Naibu Waziri wa
Ujenzi, Maliasili na Usafirishaji Zanzibar akizungumza na Msaidizi wa
Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour (kulia) kabla ya
kumkabidhi Msaada huo.
MWAKILISHI
wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum akimkabidhi fedha taslimu
(sh.1,300,000) Msaidizi wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla
Amour kwaajili ya ununuzi wa vifaa vya bomba la maji lilopasuka Mtaa
Mfenesi Mazizi Shehiya ya Gulioni Mjini Zanzibar.
MSAIDIZI
wa Sheha wa Shehiya ya Gulioni Amour Abdalla Amour akimshukuru
Mwakilishi wa Jimbo hilo mara baada ya kukabidhiwa msaada huo.
MWAKILISHI
wa Jimbo la Malindi Mohamed Ahamada Salum akijionea maji sehemu
inayovujisha Hapo Mfenesi Mazizi Shehiya ya Gulioni Mjini
Zanzibar.(picha na Abdalla Omar - Habari Maelezo Zanzibar
No comments:
Post a Comment