TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, June 8, 2016
Mwarobaini wa kukatika kwa umeme Arusha wapatikana Ni baada ya kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA, Wateja zaidi ya 89,000 waunganishwa
Na Greyson Mwase, Arusha
Imeelezwa kuwa kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA kilichopo karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kilimanjaro International Airport) kumepelekea tatizo la kukatika kwa umeme kuisha katika mkoa wa Arusha na baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro na kuongeza kipato kwa wakazi wa mkoa huo.
Kauli hiyo ilitolewa na Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mkoa wa Arusha Mhandisi Gaspa Msigwa, kwenye ziara ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini katika miradi ya TEDAP na mradi wa usafirishaji umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga katika msongo wa kilovolti 400 (BITP) inayofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB).
Sehemu ya kituo cha kupoza umeme cha KIA 132/33kV kilichopo mkoani Kilimanjaro kama kinavyoonekana pichani.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuona hatua za utekelezaji, mafanikio na changamoto za miradi hiyo pamoja na kupata maoni ya wanufaika wa miradi hiyo.
Akielezea mradi huo Mhandisi Msigwa alisema ujenzi wa kituo hicho uliogharimu Dola za Marekani Milioni 7, ulianza mwaka 2011 na kukamilika mapema Desemba mwaka 2013.
Alisema kabla ya ujenzi wa kituo hicho, umeme ulikuwa unasafirishwa kutoka katika kituo cha Kiyungi kilichopo mkoani Kilimanjaro hadi jijini Arusha umeme ambao ulikuwa hautoshelezi katika matumizi ya majumbani na katika viwanda vidogo.
Meneja Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mhandisi Emmanuel Manirabona (wa pili kutoka kulia) akielezea mafanikio ya kituo cha kupoza umeme cha KIA 132/33kV kilichopo mkoani Kilimanjaro.
Aliongeza kuwa pia kulikuwepo na tatizo la kupotea kwa umeme mwingi kutokana na kusafirishwa katika umbali mrefu.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment