Sambamba
na hilo, ameweka azma ya kukifanya kituo chake kuwa na wigo mpana wa
kuwawezesha vijana wa kutoka nje ya Tanzania kuja kujifunza soka
katika kituo hicho na kuwapeleka vijana wawili kila mwaka kwenda
kujifunza zaidi mchezo huonchini Ubelgiji.
Hayo
yamebainishwa na baba wa mwanasoka huyo wa kimataifa, Ali Samtta
alipozungumza kwa niaba ya mwanae, katika halfa ya kukabidhiwa ekari
tano za eneo la ujenzi wa kituo hicho kulikofanywa na Mtandao wa
Wasanii na Wanamichezo nchini, (SHIWATA.).
Hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika juzi katika kijiji cha wasanii kilichopo Mwenzanga, wilayani Mkuranga.
Akizungumza
kwa niaba ya mwanae, baba wa nyota huyo alisema, azma ya Samatta
(Mbwana) ni kujenga kituo kikibwa cha kimataifa ambacho, moja ya
madhumuni ni kuendelea kuwaibua na kuwakuza akina 'Samatta' wengine
wajao.
Alisema,
Salamu alizoziacha Mbwana kwa wasanii kwanza ni kuishukuru SHIWATA kwa
hatua ya kutambua mchango wake kitaifa, hivyo, katika kulipa fadhila ni
kujenga uwanja utakaokuwa na hadhi ya kimataifa kwa taifa.
"Niliongea
na Mbwana amenituma niwakilishe salamu zake kwa kwanza kwa kuishukuru
SHIWATA na kisha kueleza nia yake ya kutaka kuendelea kuibua vipaji
vya soka la vijana kupitia kituo kitakachojengwa hapa katika kijiji cha
wasanii Mwenzange" alisema Ali Samatta na kuongeza.
"Engekuwapo
hapa leo, lakini alilazimika kusafiri mara tu baada ya kumalizika kwa
mechi ya Stars dhidi ya Misri, kurejea Ubelgiji kwa wito wa haraka,
lakini anatarajia kurejea tena nchini kwa mapumziko, na mimi amenituma
nimwakilishe kwa kauli zake hizi"
Katika
hatua nyingine, mwakilishi wa mgeni rasmi, Nape Mnauye, Bi Leah Kihindi
aliipongeza SHIWATA kwa hatua yake ya kuwawekea misingi wanachama wake
ili wawe na makazi ya kudumu kupitia kijiji hicho.
Sambamba
na hilo, alilipongeza shirikisho hilo kwa kutambua mchango wa Mbwana
Samatta katika soka ambako katika sherehe hizo wanachama 35
walikabidhiwa nyumba na misingi ya kujenga nyumba.
SHIWATA inayomiliki ekari 300 za makazi katika kijiji hicho jumla ya wanachama 185 wamnejenga nyumba kwa njia ya kuchangishana.
No comments:
Post a Comment