Posted: 30 May 2013 10:51 PM PDT
Dereva wa pikipiki ya kubeba abiria 'Bodaboda' 'akiuchapa' usingizi baada ya kukosa abiria kwa muda mrefu, kama alivyokutwa Mtaa wa Samora Posta Dar es Salaam jana. Kuendesha vyombo vya moto bila kupumzika husababisha uchomvi ambao huchangia kutokea kwa ajali. (Picha na Charles Lucas)
|
Posted: 30 May 2013 10:47 PM PDT
Baadhi ya wakazi wa jiji wakimuangalia mtu ambaye hakufahamika jina aliyekuwa akitafuta kiatu kilichotumbukia katika mfereji wa majitaka, kama alivyokutwa Ubungo, Dar es Salaam juzi. (Picha na Prona Mumwi)
|
Posted: 30 May 2013 10:46 PM PDT
Meneja wa Vodacom Tanzania Mkoa wa Kigoma, Bw. Kasinde Umella, akisalimiana
na Baba wa mshindi wa sh. Milioni 100, katika 'Promosheni ya Vodacom
Mahela', Bw. Nicodemus Nalisis (kushoto), alipofika uwanja wa ndege kumlaki mtoto wake
Bw. Valerian Kamugisha (katikati) alipowasili Kigoma kutoka Dar es Salaam alikokabidhiwa 'kitita' hicho juzi. (Na Mpigapicha Wetu)
|
Posted: 30 May 2013 10:44 PM PDT
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) Dar es Salaam jana, wakati akitangaza matokeo mapya ya mtihani wa Kidato cha Nne (CSSEE) uliofanyika Oktoba mwaka jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Profesa Rwekaza Mkandara. (Picha na Prona Mumwi)
|
Posted: 30 May 2013 09:45 PM PDT
Na Mwajuma Juma,
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali amesema kuwa kuanzia sasa mashamba yote ya karafuu na minazi yaliyokuwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati yatakuwa yakishughulikiwa na Wizara ya Kilimo na Maliasili, ili kuondoa mvutano wa kiutendaji baina ya wizara hizo mbili.
Balozi Seif alitoa uamuzi huo katika Chuo cha Amali vitongoji Chake Chake Pemba wakati akizungumza na masheha wa mikoa miwili ya kisiwani Pemba.
Alisema udhibiti wa mapato yanayotokana na mazao yaliyomo kwenye baadhi ya mashamba ya Serikali yalikuwa yakileta mgongano kutokana na mashamba hayo kushughulikiwa na Wizara mbili tofauti.
Hivyo aliwaomba Masheha ambao maeneo yao yamo mashamba ya
Serikali ya karafuu na minazi na hadi sasa hayajahakikiwa watoe taarifa kwa Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Kilimo Pemba au kiongozi yeyote atakayewekwa kwenye kanda hiyo.
Akizungumzia suala la udhibiti wa ukataji ovyo wa misitu,Balozi Seif aliwakumbusha Masheha hao kuhakikisha kwamba wimbi la ukataji ovyo wa miti unadhibitiwa.
'Kijani ya Pemba tunataka ibakie kama kawaida na hili litafanikiwa iwapo wana jamii pamoja na masheha watashirikiana katika udhibiti wa ukataji ovyo wa misitu' alisisitiza Balozi Seif.
Wakielezea changamoto zinazowakabili baadhi ya Masheha hao walisema mazingira duni wakati wanapostaafu utumishi wao pamoja na mfumuko wa hujuma wanazofanyiwa masheha limekuwa tatizo kubwa linalopunguza ari ya utekelezaji wa majukumu yao.
Masheha hao waliiomba Serikali Kuu kujenga mazingira yatakayowawezesha kupatiwa mikopo ya vyombo vya usafiri ili kurahisisha kazi zao masuala ambayo Balozi Seif aliahidi kwamba Serikali itayazingatia na kuyapatia ufumbuzi unaofaa.
|
Posted: 30 May 2013 09:44 PM PDT
Na Said Hauni, Lindi
WA Z A Z I Wi l a y a y a Masasi mkoani Mtwara wamesisitizwa kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kupata haki zao za msingi katika kupata elimu itakayoweza kuwasaidia kuendesha maisha yao ya sasa na ya baadaye
Rai hiyo ilitolewa na Kaimu Ofisa Elimu shule za msingi wilayani humo, Said Nanjayo, alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Walemavu wa ugonjwa wa Ukoma katika kijiji cha Mkaseka, Jimbo la Lulindi, wakati wa uzinduzi wa jengo la darasa moja la awali lenye thamani ya sh.milioni 9.
Akizungumza baada ya ufunguzi wa darasa hilo, Nanjoyo alisema ni vema wazazi walio na watoto walio na umri wa kuanza masomo ya awali kuwapeleka mara moja kwenye shule hiyo ili waweze kuanza kupata elimu itakayowawezesha kuingia darasa la kwanza kwenye shule ya
msingi.
Nanjayo alisema ni vema kwa wazazi walio na watoto wenye umri unaostahili kuanza masomo wakafanya hivyo mara moja ili vijana wao walio bado waipate haki yao ya msingi ya elimu ikiwa ni pamoja na kulitunza jengo hilo.
"Kujengwa kwa jengo hili ni si dogo, kwani ni mwanzo wa maendeleo kwenye maeneo yao kwani uwezi kupata maendeleo bila ya kuwa na elimu," alisema Nanjayo.
Pia,aliwasisitiza wananchi wa Kijiji cha Mkaseka kujenga ushirikiano mzuri na shirika la kuondoa unyanyapaa na kuzuia ulemavu utokanao na Ukoma kwa ajili ya maendeleo yao.
Nanjayo aliwataka walimu w a l i o c h u k u a j u k umu l a kuwasomesha vijana hao kufanya kazi zao kwa moyo mmoja ili kuwatia moyo wazazi kwamba watoto wao wanaowafundisha wanapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadaye na Taifa kwa ujumla wake.
Kaimu Ofisa elimu huyo kwa shule za msingi alisema ujenzi wa chumba cha darasa hilo,ni mwanzo wa kuweza kupata shule ya msingi, ikiwemo ya Sekondari katika kijiji chao na kata kwa ujumla wake.
Diwani wa Kata hiyo ya Lulindi, Mussa Mtanga amelishukuru shirika hilo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya ujenzi wa chumba hicho cha darasa katika kijiji hicho,kwani kumewapunguzia vijana wao wadogo kutembea mwendo mrefu wa kilomita nne hadi Kijiji cha Ndwika kufuata shule.
Mwanzoni akitoa taarifa fupi,mwakilishi wa Shirika la GLRA l a Uj e r uma n i , t awi l a T a n z a n i a , B u c h a r d Rwamtoga,alisema Jengo hilo lenye chumba kimoja na Ofisi zake mbili, limegharimu sh. milioni 6 kati ya milioni 9 kama ilivyokadiriwa hapo mwanzoni kabla ya ujenzi wake, ambapo kwa upande wa Shirika la (GLRA) likichangia Sh,4.0 milioni ambapo upande wake jamii ikichangia sh.milioni 2.
Alisema ujenzi wa darasa hilo la awali ni sehemu ya uendelezaji wa uhusiano mzuri kati ya wananchi wa Kijiji cha Mkaseka na shirika hilo la Kijerumani lenye tawi lake hapa nchini.
Naye Mtendaji wa kijiji hicho ambaye pia ni mmoja wa walimu wa watoto hao, Juliana Ajetu alisema kituo hicho cha shule ya awali kina wanafunzi wapatao 47 wakiwemo 27 wavulana na wasichana 20.
|
Posted: 30 May 2013 09:43 PM PDT
Na Mwa j uma J uma ,
Zanzibar
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakar, amesema kuwa katika kutafuta amani na utulivu ni lazima pawepo na msimamo wa pamoja ili kuweza kufanikiwa kumaliza tofauti.
Waziri huyo aliyaeleza hayo katika uzinduzi wa kitabu cha Mizozo na namna ya kuitambua na kuitatua kisha kuichambua mizozo ya Zanzibar hafla iliyofanyika mjini Unguja.
Alisema kuwa katika kufikisha suala hilo pamoja na kuwepo na msimamo lakini hekima na busara itumike ili kufikia lengo la kupatikana kwake.
Hata hivyo alisema kuwa si njia sahihi ya kufikiria kuwa njia pekee ya kumaliza tofauti baina ya pande mbili ni kumshinda unaepambana nae bali ni kumshawishi ili akubaliane na mtazamo pamoja na unayoyasema.
Aidha, alisema kuwa kwa vyovyote vile kiini cha migogoro huwa ni
namna ya kutotendewa haki waonavyo upande mmoja au mabishano ya kidini, kutotimiziwa kwa matakwa yao muhimu ya kimaendeleo pamoja na suala zima la kudhibiti hali ya uchaguzi katika nchi husika.
Alisema kuwa mizozo ya aina hiyo huchukua aina ya ugomvi wa kiraia na kuanza kutengana baina ya kundi fulani na lingine ndani ya jamii, ambayo ndio yanayoifanya dunia kutafuta njia za usuluhishi baina ya watu hao wanaoishi ndani ya nchi moja.
"Zanzibar nayo haijakuwa nje ya matatizo hayo, ndio tukapata misukosuko mingi tu katika visiwa vyetu kuanzia mwaka 1995," alisema.
Mapema mjumbe wa Kamati ya Amani na Utulivu, Mchungaji Lusungu Leonard Mbilinyi alisema kuwa amani ndio nguzo ya kuleta maendeleo ya taifa lolote duniani, hivyo alisema kuwa Wazanzibari hawana budi ya kuungana na kutatua migogoro yanayojitokeza katika jamii yao iliyowazunguuka.
|
Posted: 30 May 2013 09:42 PM PDT
Na Said Hauni, Lindi
WAKAZI wawili katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na shtaka la kujihusisha na masuala ya ujambazi kwa kutumia silaha mbalimbali ikiwemo bunduki ya kienyeji na kufanikiwa kupora bidhaa na fedha taslimu jumla ya sh milioni 1.2.
Washtakiwa hao ambao kesi yao ipo kwa Hakimu Aluu Nzowa wa Mahakama ya wilaya hiyo ni, Hamisi Athumani Mbuhi na Rajabu Juma Ndete wote ni wakazi wa mtaa wa Kongo mjini Lindi na wamelazwa hospitali ya mkoa huo Sokoine.
Akiwasomea shtaka lao katika wodi namba sita walikokuwa wamelazwa Mwanasheria wa
Serikali, Juma Maige alidai Mei 20 mwaka huu usiku washtakiwa wote kwa pamoja walifika dukani kwa Hamisi Hassani Bakari lililopo Kijiji cha Mkwajuni Wilaya ya Lindi na
kupora bidhaa na fedha taslimu.
Maige aliiambia mahakama hiyo kwamba siku hiyo washtakiwa wakiwa na bunduki moja aina ya Shotgun iliyofutwa namba zake pamoja na panga walifanikiwa kupora simu sita za mkononi za watu waliozipeleka kwa ajili ya kuchaji na fedha taslimu Sh.900,000/-na kufanya jumla ya sh.milioni 1.2.
Alidai mahakamani hapo kwamba siku hiyo washtakiwa wakiwa na silaha hizo walifika dukani kwa mlalamikaji huyo na kuanza kupiga risasi hewani ikiwa na lengo la kutisha majirani wasitoke nje nyumba zao kisha kuvunja mlango
wa duka lake na kupora bidhaa na fedha hizo na kutoka nazo nje ambapo waliendelea kupiga risasi hewani hadi kuishiwa.
Mwanasheria huyo wa Serikali alidai kwamba washtakiwa wamefanya kosa chini ya kifungu cha 287 kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Pia aliiambia mahakama hiyo kwamba kitendo cha watuhumiwa hao kuishiwa risasi kwenye bunduki yao kulitoa mwanya kwa wananchi ambao walijitokeza na kufanikiwa kuwatia mikononi na kuanza kuwapiga hadi kuishiwa nguvu.
Alidai kitendo cha kuishiwa nguvu kuliwafanya wananchi hao kuendelea kujichukulia sheria mikononi ikiwemo kuwafunika nyasi na kuwachoma moto kabla ya kuokolewa na Polisi waliofika kijijini hapo muda mfupi.
Washtakiwa wote kwa pamoja wamekana shtaka lao na kesi yao,namba 49/2013,imepangwa kusikilizwa tena mahakamani hapo Juni 06 mwaka huu na wote wapo chini ya uangalizi wa askari magereza katika hospitali ya Sokoine.
|
Posted: 30 May 2013 09:38 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Muheza
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Julius Mtatiro anatarajiwa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata za Genge na Tingeni zilizoko wilayani Muheza Mkoa wa Tanga.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi CUF Taifa, Nuru Awadh Bafadhili alisema jana kuwa uzinduzi huo utafanyika siku mbili ambapo katika Kata ya Genge utafanyika kesho na Kata ya Tingeni itakuwa Juni 2.
Alisema mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu huyo yatafanyika katika Kijiji cha Kerenge Kata ya Tingeni na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki kiongozi huyo.
Wakati huo huo,Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Muheza mkoani
Tanga kimepata pigo baada ya wanachama wake 72 wa Kata ya Pande Darajani kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).
Wanachama hao walikabidhiwa kadi hizo juzi na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake CUF Taifa, Nuru Awadh Bafadhili katika mkutano wa kuhamasisha uhai wa chama hicho uliofanyika katika kata hiyo.
Akikabidhi kadi kwa wanachama hao wapya aliwataka wasiogope vitisho kwani vitakuwa vingi hasa nyakati hizi za chaguzi ndogo, lakini aliwataka waendelee na kuunga mkono CUF yenye ‘Dira ya mabadiliko’na kusisitiza kuwa hataweza malaika kuwaambia kuwa CCM imeshindwa kuwaletea Watanzania maisha bora.
Alisema katika kipindi cha miaka 52 ya uhuru bado Watanzania hawana uhakika wa maisha yao ya kila siku na kuwataka kuunga mkono hicho ili kilete mageuzi ya kweli ndani ya taifa.
Bafadhili aliwataka wanachama hao kuendelea kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kushinda katika chaguzi ndogo za udiwani na uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Katibu wa CUF Wilaya ya Muheza, Juma Nindi na Mwenyekiti wa Chama hicho wilaya, Omari Sesunga waliwataka wanachama hao kuendeleza mshikamano kwani dhamira ya chama hicho ni kushika dola mwaka 2015.
|
Posted: 30 May 2013 09:36 PM PDT
USHIRIKIANO na mwamko wa wakulima walioungana katika vikundi kutekeleza mradi wa Mpango wa Maendeleo vijijini; katika mwambao wa Pwani ya Tanzania (CRSPT); unaotekelezwa na Aga Khan Foundation, katika Wilaya ya Newala, umewafurahisha, viongozi katika kata ya Mcholi ya kwanza, walioshiriki siku ya wakulima kijijini, Chiunjila, anaripoti Godwin Msalichuma, Newala.
Hayo yalijitokeza kijijini hapo hivi karibuni, ambapo diwani Selemani Kaisi, alipopewa fursa ya kuzungumza na vikundi vya wakulima takribani 87, wanaume 61 na wanawake 26, walikusanyika katika siku yao, ili kujifunza pamoja mambo muhimu na changamoto zinazowakumba katika mradi huo wa kilimo cha mpunga na ufuta.
“Nimeridhishwa sana na utekelezaji wenu wa mradi huu kwa ushirikiano na kwa kweli unanitia moyo kuona haya yakifanyika kwa umoja na nguvu ya pamoja, niseme kuwa mmeshakuwa wataalamu sasa, ninaimani mnaweza kuendelea hata bila ya wafadhili kuwepo” alisema Kaisi na
kuongeza kwa kuwaasa:
Waendelee na utaalamu huo walioupata kuboresha kilimo cha mpunga na ufuta na pia kuhifadhi elimu hiyo kwa faida ya vizazi vyao vijavyo.
Alisema, amefurahishwa na kusikia kuwa awali kabla ya mradi wakulima walikuwa wanavuna mpunga katika hekta moja magunia manne mpaka matano, lakini sasa wanafikisha magunia 25 mpaka 40.
Aidha, aliwaomba kuwa macho na walanguzi wa mazao wakati wa mavuno; kwani mbinu wanazopewa na asasi hiyo ya kimataifa, ni nzuri ya kukusanya na kuhifadhi pamoja, wakisubiri bei nzuri itakapofika katika zao hilo la mpunga.
“Nawaomba muwe macho na walanguzi wa mazao yenu, wasije wakawarubuni wakati wa mavuno tukauza mpaka mbegu; nawasihi mtumie hivyo vikundi vya kuweka na kukopa (Vicoba), yaani ‘wekeza boresha maisha’ hapo tukiweka akiba nadhani kilimo kitakuwa na manufaa zaidi,” alisema diwani huyo.
Naye, Ofisa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo katika Wilaya ya Newala (DALDO), Alford Mpanda, alisema, baada ya kuona maendeleo mazuri ya kilimo cha mpunga kijijini Chiunjila, alidai amegundua kuwa kumbe kuna mazao ambayo wakulima, wanaweza kuzalisha bila mikikimikiki kama ilivyo kwa zao la korosho, ambapo lina gharama kubwa katika kuandaa shamba na kupata mapato yake.
“Inanipa moyo sana na nguvu kuona kuwa kumbe kuna mazao kama mpunga na ufuta yanachukua muda mfupi na gharama ndogo k u y a z a l i s h a , h a t a h a k u n a mikikimikiki ukilinganisha na zao la korosho,” alisema Mpanda.
Hata hivyo alifurahishwa na kuridhishwa kuona kuwa hata mapato kwa wakulima yameongezeka kutoka magunia matano kwa hekta mpaka magunia 40, ambapo aliwashauri kuongeza bidii katika uzalishaji, kwani pia uzalishaji wao unaongeza pato la halmashauri na Taifa kwa ujumla wake.
|
Posted: 30 May 2013 09:35 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Kigoma
MZAZI wa kija naaliy eshindash.milio ni10 0katika promosheniya VodacomMahela, Bw .Nicodemus Nalisis am etoawit okwawa kaziw a Mkoaw aKigo mak ujen gatabia yakushiriki mash in danomba lim bali yanayotolewanakamp unizasimuza mkononi hapanchini.
Bw.Nicodemus alisemahayo juzi mkoaniKi gomaw akat ialipowasili kumpok eakijana wakeB w.ValerianKamugish aaliyewasilimkoani hapa marab aada ya kuka bidhiwakiasi chash .mi lioni10 0m wanzoni mwawik ihiibaad ay akuibukamshindiwashindanoh ilo .
Alisem a k uwa hatua yakushiriki ma shindanoha yoyatatoa fursayaushindi k wawa nanchiwengi mkoani Kigoma hivyo kuongeza uwezekano wa mkoa wa Kigoma kutoa washindi wengi katika mashindano yanayoendeshwa na Vodacom na kubadilisha maisha yao ya kiuchumi na
kimaendeleo kiujumla.
Bw.Ni c o d emu s a l i e l e z a kufurahishwa na hatua ya mwanae kushinda katika shindano hilo na kwamba mbali na hiyo kuwa fedha hizo ni msingi mzuri wa maisha ya kijana huyo lakini pia ushindi huo ni fahari kwa wananchi wa Kigoma na historia kubwa ya kijana huyo na familia.
Alisema ingawa yeye alishiriki katika promosheni hiyo, bila mafanikio lakini anampongeza mwanaye kushinda kwani sawa kama yeye ameshinda tu.
Licha ya kuipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa mashindano mbalimbali likiwemo la Vodacom Mahela na kwamba hatua hiyo inachangia katika kukuza na kupanda uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na familia kwa ujumla.
Aidha mmoja wa majirani wa familia ya mshindi huyo Bw. Jackson Kakwaya mfanyabiashara wa bidhaa madukani alisema hatua ya ushindi wa kijana huyo inapaswa kuwa hamasa tosha kwa watu wengi wa mkoa huu kushiriki katika shindano hilo kikamilifu.
Alisema ushindi huo umemfanya aamini kuwa hakuna upendeleo katika shindano hilo na hakutarajia kama ingewezekana mkazi wa Kigoma kushinda shindano tena la fedha nyingi kiasi hicho.
Alisisitiza Vodacom kuendeleza program kama hizo hatua ambayo alisema inawapa fursa washindi kuboresha maisha yao ghafla kutoka katika hali ya chini au ya kawaida nakuwa tajiri kwa muda mfupi.
Kwa upande wake mshindi wa Vodacom Mahela Bw. Valerian Kamugisha mbali na kupongeza Vodacom kwa kumkabidhi zawadi hiyo alikiri shindano hilo kutokuwa na mianya yoyote ya rushwa nakusema kuwa hana ndugu katika kampuni hiyo lakini ameshinda.
Aliwataka wananchi kuamini mashindano yanayoendeshwa na Vodacom na kushiriki mara kwa mara jambo ambalo litaongeza idadi ya washindi mkoani Kigoma na kuondoa dhana kuwa Kigoma haiwezi kutoa mshindi.
|
Posted: 30 May 2013 09:33 PM PDT
Na Elizabeth Joseph, Dodoma
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amewatahadharisha watu wanaopenda kuwaita wenzao mafisadi pindi wanapowaona wamepata mafanikio kwa kuwa na yeye anatarajia kunufaika na ufugaji wa nyuki.
Alisema hivi karibuni anatarajia kuvuna asali karibu tani moja na mara akianza kuiuza lazima apate faida kutokana na asali hiyo, hivyo Watanzania wenye dhana ya ufisadi kwa wanaopata faida au maendeleo katika shughuli za kujiinua kiuchumi waache tabia hiyo.
Pinda alibainisha hayo juzi mjini hapa wakati akifungua semina ya wakuu wa mikoa na wilaya nchini iliyohusu utoaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima.
Aliwataka wakuu hao kutafuta njia ya kuwasaidia wafugaji nchini kwa
kuwapa fedha kwakuwa nao ni sehemu ya kilimo pamoja na kuwataka kuwawezesha vijana nchini kwa kuwashauri kuhusu kilimo na ufugaji ili kuwapa ajira na kuwaongezea kipato.
"Lazima tuwatengenezee utaratibu vijana kwa kuwapa ardhi kwa kutenga maeneo maalumu,mbegu na fedha kwa ajili ya kilimo na ufugaji ili vijana waweze kujiajiri na kujipatia kipato," alisema Pinda.
Aliwataka wakuu hao kujiuliza kama kuna mabadiliko ya kipato na kimaendeleo kwa wananchi katika wilaya na mikoa yao tangu walipokabidhiwa kushika madaraka.
"Jiulizeni mmefanya nini katika kuwapandisha kimapato wananchi wenu tangu tumewakabidhi kuwaongoza katika hali moja kwenda hali nyingine na lazima muwe wabunifu katika kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi wenu," alisema Pinda.
Hata hivyo aliwataka kuangalia kwa makini suala la mfumo wa malipo ya vocha kwa wasambazaji kwa kuwapatia vocha kwa wakati na kuhakikisha wanasimamia vizuri vocha hizo kwakuwa serikali iliona mfumo huo ndio njia nzuri ya kumwezesha mkulima kupata mbegu bora na kumfikia mkulima bila kuchelewa pamoja na kuhakikisha wanaviingiza vikundi vinavyotambuliwa katika utoaji ruzuku ili kuondoa udanganyifu katika malipo hayo.
|
Posted: 30 May 2013 09:32 PM PDT
Na Rachel Balama
KAMPUNIzakuten genezadawa za b ina damunchini zimetak i wakutumia teknolojiampya ijulikanayo“hakikisha d awa156 29 ”iliyoanzishwan akampu ni yadawa yaG laxoSmithKline ili kudhibiti da w abandia.
Mwit ohu ou litolew a Dar es Salaamja nan aNaibuWaziriwaAfyanaUstawiwaJamii , Dkt.Seif Rashi d, wakati a kiz induaprogramuyamtanda owah a kikisha dawahal isi kwaku tum aujumbemfupi wamaneno kwen da1 5629 .
A lisemak uwanjia hiyoitasaidia kudhibitida waba ndiakw ak uwa changamo tokub wailiyo pokw asasaniuwepo wadaw a band iapamoja na watukuu zadawazi sizofaakutibumago njwa.
Alis emaSerikali itajitahidi kufanyauhakik iilikuhakikisha
kwamba dawaz ote zinazotokanjeyanchi zinakuwa halisi na si ban dia .
Al ionge zakwa mbaku tamb uahilo,ndioma anaBoha riKuuya Da wa(MSD) pam ojana MamlakayaCh akulanaDaw a(TFDA) zimekuwaz ikishiriki anakikazi kuhakikish akwambadaw a zotezin azoingia nchini zinahakikiwa naTFDA.
Akizung umziaprogra mu hiyoyaHakikishaDawa, MkuuwaM asua la yaUdhibiti wa Nchi zinazoendel ea, Dk t WilliamMwatu, alisemanihuduma ya k utumaujum bemfupikupitias imuinayow apawat umiaji wadawanjiayakuhaki kishadaw a wan azonu nua zim etokakampu niyaGSKnani halisi.
Ali sem ahuduma hiyo inapatikana kwada watembeya Au gm entin625m gpam oja na tembezadawa ya min yooyaZante l400mg, ambapopake ti ya dawait akuwa nakibandikochakumuulizamtumiaji atafute nam ba ya uhakiki sho.
Ali semakilapak itiyadawa juuyakeimeb andik waki ban dikocha usa lama,a mbachokina namba yauhakik iiliyofich wa,a mbapomnunuzi ataikw ang ua nak isha kuandikanambahiyokweny esimunakuitum akwen dan amba15629na kishaku patajib ukama dawa hiyoni halis i kutokaGS K .
Al isemahudum ahiyo ni bureitatole waku pitiamta ndao. Alio ngezakuw ahudu mahiyoitaendelea kwa dawa za magonjwa mengine kama Kifua Kikuu (TB), UKIMWI pamoja na Malaria.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari nchini (MAT), Dkt. Primius Saidia, alisema katika nchi zilizopo Jangwa la Sahara asilimia 30 ya dawa ni bandia na nyingi hasa za malaria.
Alisema njia hiyo itaisaidia Serikali kuhakikisha wauzaji na watengenezaji wa dawa bandia wanapatikana na kuwataka madaktari kutoa dawa ambazo zinaweza kutibu magonjwa.
|
Posted: 30 May 2013 09:30 PM PDT
Na Rehema Mohamed
Mohamed (25), amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya sh. milioni tatu baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka matatu.
Mashtaka hayo ni kutoa taarifa za uongo katika mitandao ya simu za mkononi na kutuma ujumbe wa maudhi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema.
Mshtakiwa huyo alisomewa hukumu hiyo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na Hakimu Hellen Liwa ambapo upande wa mashtaka uliwakilishwa na wakili Bw. Ladslaus Komanya.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Liwa alisema hayo ni makosa mapya yaliyo katika Sheria Mpya ya Mawasiliano na Mitandao.
“Kwa kitendo ulichokifanya kuwatumia ujumbe viongozi wa juu wa
serikali unahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kutoa faini ya sh. milioni tatu iwe fundisho kwa wengine, kama hujaridhika na adhabu unaweza kukata rufaa,” alisema.
Katika maelezo ya awali, ilidaiwa Mei 20 mwaka huu katika Makao Makuu ya jeshi hilo, zilipelekwa taarifa za kiintelejentsia kwa maofisa wa ngazi za juu kuwa kuna mtu ambaye namba yake ya simu imesajiliwa kwa mitandao tofauti.
Namba hizo ni 0687 521947 na 0687 521948 za Airtel na 0759 799956 ya Vodacom zilizokuwa zikitumika kutoa ujumbe kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na IGP.
Baada ya upelelezi kufanyika, ilibainika namba hizo zilisajiliwa kwa majina tofauti ambayo ni Fadhili Issah, Fadhili Issa na Godfrey Joseph ambazo alikuwa akizitumia mshtakiwa.
Baada ya mshtakiwa kukamatwa Mei 25 mwaka huu na kuhojiwa polisi, alikiri kutumia namba hizo na kuzisajili kwa majina tofauti kwa lengo la kufanya uhalifu na kuficha utambulisho wake.
Mei 27 mwaka huu, mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yanayomkabili na kukiri kutenda makosa hayo
|
Posted: 30 May 2013 09:29 PM PDT
Grace Ndossa na Goodluck Hongo
KIWANGO cha ufaulu kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012, kimeongezeka kwa asilimia 43.8 tofauti na yale yaliyotangazwa awali ambayo ni asilimia 34.5.
Matokeo hayo yametangazwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa ambaye alisema kuwa, kati ya wanafunzi 397,138, waliofaulu ni 159,609.
Kati ya wanafunzi hao, wavulana 98,858, wasichana ni 60,751, sawa na asilimia 43.8 tofauti na matokeo ya awali.
Alisema waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 35,349 ambapo kati yao, wavulana ni 24,425, wasichana ni 10,924, sawa na asilimia 9.55. Waliopata daraja la
nne ni 124,260 sawa na asilimia 33.54 ambapo jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani huo mwaka 2012, walikuwa 480,029 katika vituo 5,058 vilivyosajiliwa.
Aliongeza kuwa, wanafunzi 210,846 walipata sifuri sawa na asilimia 56.2. Dkt. Kawambwa alisisitiza kuwa, matokeo hayo ni halali na hayajachakaliwa.
“Matokeo yaliyofutwa yalikuwa yamechakatwa kwa kutumia utaratibu wa “fixed grade ranges”, ambapo viwango vya aina moja hutumika kuchakata matokeo kwa masomo bila kujali kiwango cha ufaulu wa masomo husika.
“Matokeo ya sasa yamefanywa vivyo hivyo, lakini yamefanyiwa Standardlization (kuongezwa) ambapo kimataifa kuna aina kuu mbili za kuchakata matokeo ya mtihani,” alisema Dkt. Kawambwa.
Aliongeza kuwa, kwa miaka mingi Baraza la Mitihani limekuwa likitumia mfumo wa “flexible grade ranges” ambapo mwaka 2012 mfumo wa “fixed grade ranges”, ulitumika kuchakata matokeo kwa mara ya kwanza.
Hata hivyo, Dkt. Kawambwa alisema kuanzia mwaka huu, wataanza kuchakata matokeo kwa mfumo wa “fixed grade ranges” kuanzia kidato cha nne hadi sita kama nchi nyingine zinavyofanya.
Alisema ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha daraja la kwanza hadi la mwisho na shule zimegawanywa katika makundi mawili la kwanza ni zile zenye wanafunzi zaidi ya 40 na nyingine zenye wanafunzi chini ya 40 kulingana na idadi ya wanafunzi.
Shule 10 bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi zilizoongoza ni St. Francis Girls (Mbeya), Marian Boys (Pwani), Feza Boys (Dar es Salaam), Marian Girls (Pwani), Canossa, Fedha Girls zote za (Dar es Salaam), Rosmini (Tanga), Anwarite Girls (Kilimanjaro), St. Mary Mazinde Juu (Tanga) na Jude Mushono Arusha.
Alizitaja shule 10 za mwisho zenye watahiniwa 40 na zaidi, Mibuyuni (Lindi), Mamndimkongo (Pwani), Chitekete (Mtwara), Kikale (Pwani), Zirai (Tanga), Matanda (Lindi), Kwamndolwa (Tanga), Chuno na Mbembaleo zote za (Mtwara) pamoja na Maendeleo ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Dkt. Charles Msonde, alisema baraza lilipewa jukumu hilo na kulifanyia kazi ambapo wanafunzi 10 bora wa mwanzo, wataonekana kwenye tovuti za baraza hilo.
Februari 18,2013 wakati Dkt. Kawambwa akitangaza matokeo hayo, alisema watahiniwa 23,520 walifaulu katika daraja la kwanza hadi tatu kati yao wasichana 7,178, wavulana 16,342
Alisema waliopata sifuri 240,903m, kati yao wavulana 120,664, wasichana 120,239 na waliopata daraja la nne 103,327.
|
Posted: 30 May 2013 09:28 PM PDT
Mashaka Mhando na Rachel
Balama
TUKIO la kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini, limechangiwa na kazi yake ya uandishi wa habari likihusisha vyombo vya dola na vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya uchunguzi wa tukio hilo, Bw. Deodatus Balile, aliyasema hayo mjini Tanga jana wakati akiwasilisha ripoti ya uchunguzi uliofanywa na watu watano.
Alisema kamati hiyo imebaini halina uhusiano wowote na masuala ya rushwa au mapenzi bali ni mpango maalumu ambao uliandaliwa na baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wasio waaminifu ili kutekeleza matakwa ya kisiasa.
“Kamati imebaini kuna kutupiana mpira kati ya vyombo vya dola na vyama vya siasa katika kuandaa mpango wa kuteswa kwa Bw. Kibanda hatua ambayo uchunguzi huo umebaini kuwepo kwa sababu ya kutokea tukio hili,” alisema Bw. Balile.
Katika taarifa hiyo yenye kurasa 10 ambayo aliwasilishwa kwenye
Mkutano wa pili wa mwaka wa mashautiano kati ya Baraza la Habari nchini (MCT) na TEF,Bw. Balile alisema uchunguzi huo ulijikita katika mazingira ya tukio hilo kabla na baada ya kutokea.
Pia uchunguzi huo uliangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006), na kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua.
Kamati hiyo ambayo ilitoa wito kwa Serikali kufuatilia kwa karibu na kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kupata ukweli na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya wote waliohusika kumtesa Bw. Kibanda.
I l i p e n d e k e z a k u f a n y i k e marekebisho makubwa ya haraka katika mifumo ya uendeshaji wa vyumba vya habari ili kurejesha misingi ya uandishi wa habari inayokubalika.
Usalama wa wanahabari upewe kipaumbele na wamiliki, wanahabari wenyewe na jamii kwa ujumla pamoja na kuwepo mafunzo ambayo yatawawezesha wanahabari kutambua viashiria vya hatari na kuchukua hatua mara moja.
Ripoti hiyo ilizitaka taasisi za habari zifanye juhudi za makusudi kukutana na vyama viwili vya siasa vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), haraka iwezekanavyo ili kuzungumzia viashiria vya hatari vinavyoelekea kuvuruga amani ya nchi.
Bw. Kibanda aliumizwa kichwani na kusababisha baadhi ya mifupa yake kuvunjika, kutobolewa jicho lake la kushoto, kung’olewa meno na kucha bila ganzi na kumkata pingiri ya kidole cha pete chini ya kucha na kuondoka nayo.
Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Bw. Rashid Kejo (Katibu), Pili Mtambalike, Jane Mihanji na Tumaini Mwailenge,
|
Posted: 30 May 2013 09:27 PM PDT
*HOTUBA YAKE YALETA UTATA KWA WABUNGE CUF
*AKATAA KUOMBA RADHI, ASEMA KADHALILISHWA
*KAMATI KUMJADILI, NDUGAI AAHIRISHA BUNGE
Na Waandishi Wetu
KWA mara nyingine, Naibu Spika wa Bunge, Bw. Job Ndugai, jana amelazimika kuahirisha kikao baada ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), kupinga baadhi ya maneno yaliyopo katika hotuba ya Kambi ya Upinzani.
Hotuba hiyo ilisomwa bungeni mjini Dodoma na Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Ezekiel Wenje, ambaye ni Mbunge wa Nyamagana, Mwanza.
Wakati Bw. Wenje akiendelea kusoma hotuba hiyo, mbunge wa Jimbo la Mtambile, Bw. Masoud Salim (CUF), Zanzibar, alisimama na kuomba mwongozo wa spika na kutaka hotuba hiyo isitishwe akidai imejaa uzushi, uwongo na ushenzi.
Katika hotuba yake, Bw. Wenje alisema Chama cha CUF itikadi zake ni
za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji pamoja na ushoga.
“Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wa umoja wa Maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa nchini Uingereza, Lynn Featherstone, kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho kikipitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu,” alisema.
Katika mwongozo wake, Bw. Salim alitumia kanuni ya 68 (1) (a) inayosema, bila kuathiri masharti ya ibara ya 100 ya katiba inayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, mbunge hatatoa taarifa ambazo si za kweli, hatatumia lugha ya matusi na inayodhalilisha wengine.
“Natoa hoja kwamba, hotuba hii ni ya kizushi...huu ni uhuni, uwongo, ushenzi na uzandiki, hotuba hii si ya kusomwa bungeni,” alisema Bw. Salim akinukuu maneno yaliyopo kwenye hotuba ya Bw. Wenje.
Bw. Salim alikitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiombe radhi kutokana na kauli hiyo akiiomba Kamati ya Maadili ya Bunge iifanyie kazi kauli yao.
Kutokana na maelezo hayo, Bw. Ndugai alimuuliza Bw. Wenje kama
na kumjibu kuwa;
“With due respect, ningeomba wabunge wenzangu wanisikilize kwa n z a . . . h a p a t ume e l e z a CHADEMA, CCM pamoja na CUF, juu ya uhusiano wao na mataifa ya nje.
“Ni ukweli kwamba CCM wako mrengo wa kushoto, CHADEMA mrengo wa Kati na CUF mrengo wa Kiliberali,” alisema Bw. Wenje, ambaye baada ya kutoa majibu hayo, wabunge wa CUF walisimama, kushika kitabu cha hotuba na kumfuata Bw. Wenje mbele ya Bunge.
Hali hiyo ilisababisha utulivu kutoweka bungeni ambapo Bw. Ndugai alilazimika kuahirisha Bunge hadi jioni na kuitaka Kamati ya Maadili ya Bunge, ikutane kwenye kikao cha dharura ili kuipitia hotuba hiyo.
Baada ya Bunge kuahirishwa, Bw. Wenje alitoka haraka akikimbia huku akisindikizwa na polisi hadi nje ya ukumbi wa Bunge ambako kulitokea zogo kubwa kati ya wabunge wa CHADEMA na CUF, kila upande ukitupiana maneno na vijembe vya hapa na pale.
Wabunge wa CUF walitishia kuwapiga wabunge wa CHADEMA, kama wataendelea na msimamo huo.
“Lazima waombe radhi na waache kuzushia chama chetu mambo ya uongo na kihuni,” alisikika akisema mbunge wa CUF ambapo wabunge wa CHADEMA, walisisitiza hawatafuta kauli yao kwa sababu wana uhakika na mambo waliyoyasema.
Kikao cha jioni
Kikao cha jioni kilianza kwa Bw. Ndugai kumpa nafasi Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge, Bw. John Chiligati, aeleze uamuzi uliofikiwa na kamati yake kuhusiana na sakati hilo.
Bw. Chiligati aliliambia Bunge kuwa, kamati yake ilikutana na Bw. Wenje ambaye ni mlalamikiwa na Bw. Salim (mlalamikaji), ambapo walimtaka Bw. Wenje afute kauli zake kwa maandishi, aombe radhi na kamati itoe adhabu.
Hata hivyo, Bw. Wenje aligoma kuomba msamaha akidai hakukosea bali katika hotuba yake alieleza itikadi ya vyama vya mrengo wa Kiliberali na hakulenga chama chochote.
Pia Bw. Chiligati alisema, Bw. Wenje alikubali kuondoa maneno hayo kwenye hotuba yake, lakini hotuba hiyo iliporudi haikutofautiana na ile ya kwanza bali kilichobadilika ni maneno kuwa ya Kiingereza ambayo ni ya usagaji na ndoa za jinsia moja.
Baada ya kutoa maelezo hayo, Bw. Ndugai alimpa dakika tano Bw. Wenje atumie fursa hiyo kufanyia kazi ushauri wa kamati iliyomtaka aombe radhi na kuondoa maneno hayo kwenye hotuba yake, lakini alikataa na kuhoji aombe msamaha kwa kosa lipi?
Alisisitiza kuwa, hawezi kufuta maneno ya ukweli na kudai hata yeye alitukanwa na kudhalilisha asubuhi kiasi cha kushindwa kumaliza hotuba yake.
Baadaye Bw. Ndugai alimpa nafasi mlalamikaji Bw. Salim ambaye naye alisisitiza kuwa, msimamo wake uko pale pale; hivyo ni vyema Bw. Wenje aombe radhi, kuondoa maneno hayo kwa maandishi na kamati ichukue hatua, vinginevyo hotuba isisomwe na CUF itamuunga mkono.
Akitoa uamuzi wa kiti, Bw. Ndugai alimtaka Bw. Wenje aombe radhi na akubali kuondoa maneno yote yaliyokuwa yakikataliwa ili aweze kuendelea na hotuba yake.
Bw. Wenje aliinuka na kukubali kuondoa maneno hayo na kutaka kuendelea na hotuba yake bila kuomba radhi ambapo Bw. Ndugai alimkatisha kwa kumtaka akae chini na kutangaza kuahirisha kikao cha Bunge hadi leo asubuhi.
Alisema suala hilo linarudishwa tena kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge kwa ajili ya maamuzi zaidi.
Habari hi i imeandikwa na Gladness Theonest, Kassim Mahege na Rachel Balama.
|
Posted: 30 May 2013 09:23 PM PDT
Na Mwandishi Wetu, Ludewa
MBUNGE waLu dewa, mkoaniNjombe, Bw. D eoFilikunjombe, ameipo nge za safumpyawaChamaChaMapindu zi (CC M), kwakazi kub wa wanayo endeleakuif anyailikukijengachama hichokuanzia ngazi ya shina hadi T aifa.
Bw .Filikunjomb eali yasemahayom jini humoja nawakati akihutub iawananc hikwenyemkutanowa hadharauli ofanyika katikaKatayaLupinguna kuonge za kuw a, y eyote mwe nyendotoyakushi ndanana CCM anapot eza mudawake.
“KatibuMkuu wa chamach etu, Bw. Abdu lrahmanKinan a,pianinai manik ub wanaKatibu wa NEC ,Itikad inaUen ez i, Bw. NapeNnauye,k azi wanayoifanyayakupigani awanyonge inaone sha kiwan gocha uzalendo walichnachohiv yot uwaungem kono.
“Kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010/2015, kusimamia
shughuli za maendeleo nchini ni dhahiri umasikini utaondoshwa katika nchi yetu kwa kasi kubwa,” alisema.
Alisema ahadi zote zilizotolewa 2010, atahakikisha zinatekelezwa kwa kiwango cha juu ili kuwajengea imani wananchi hao na kudai kuwa, atahakikisha anafanikisha ujenzi kwa Barabara Kuu ya Njombe- Ludewa kwa kiwango cha lami.
Pia aliahidi kuanzisha mchakato wa ujenzi wa barabara itokayo Ludewa Mjini kwenda Mwambao wa Ziwa Nyasa ikiwemo Kata ya Lupingu.
Akizungumzia maboresho ya mawasiliano ya simu, mbunge huyo alisema tayari maombi yake ya minara mitano yameanza kutekelezwa ambapo hivi sasa amepata minara mitatu ambayo itapanua huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi katika maeneo mbalimbali wilayani humo na Kata hiyo ya Lupingu.
Kwa upande wake, Bw. Kinana alipongeza jitihada zinazofanywa na Bw. Filikunjombe katika kutetea na kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
|
Posted: 30 May 2013 09:21 PM PDT
Na Mosi Mrisho
RAIS Jakaya Kikwete, amewapandisha vyeo baadhi ya maofisa wa polisi akiwemo Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Michael Kamuhanda, kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, uteuzi ambao unaanza mara moja.
Katika uteuzi huo, Kamanda Kova na Isaya Mngulu, wote wamekuwa Makamishna wa Polisi (CP).
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, ilisema maofisa wengine waliopandishwa vyeo katika ngazi hiyo ni Thobias Andengenye na Simon Sirro.
Msemaji wa Wizara hiyo, Bw. Isaac Namtanga, aliwataja maofisa wengine kuwa ni Elice Mapunda, Brown Lekey, Hamdani Omar Makame, Kenneth Kasseke, Abulrahman Kaniki, Adrian Magayane, Sospeter Kondela na Ernest Mangu. Wengine ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, Hussein Laisseri, Anthony Mwami, Adolfina Chialo, Mpinga Gyumi, Ally Mlege, Hezron Gyimbi na Jonas Mugenzi ambao kabla ya uteuzi huo walikuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi.
|