Katika Miaka ya Nyuma Mkoa wa Dodoma, ambao ndio Mji Mkuu wa Tanzania, ulikuwa ukishangaza sana kutokana na Uchakavu wa Mitaa ya Barabara zinazoingia na kutoka kutokana na ukosefu wa lami, tofauti kabisa na Miaka hii kuanzia mwaka jana, ujenzi ambao umefanyika kwa haraka tpfauti na matarajio ya wengi, ikiwa ni kutokana na Juhudi za Waziri mwenye dhamana ya Barabara, Dkt, John Pombe Magufuli (Mb), ivi sasa Mji wa Dodoma pamoja na kwamba bado unaendelea kusua sua katika Uboreshaji wa Majengo yaliyopo Mjini lakini kwa asilimia kubwa tayari umeanza kuwa na sura ya tofauti yenye kupendeza na hata kustahili kuwa mji mkuu wa Tanzania. hata hivyo imechangiwa na uwepo wa Vyuo Vikuu Vingi ambavyo vimejengwa ikiwamo Chuo Kikuu cha Kimataifa cha (UDOM). Ongera sana Utawala wa Awamu ya Nne wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.(Picha kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania).
No comments:
Post a Comment