TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 28, 2015

JAJI KIONGOZI ATOA SOMO KWA WATENDAJI WA MAHAKAMA YA KAZI, CHAMA CHA WAAJIRI NA WAFANYAKAZI.

MTEJA WA BENKI YA AFRIKA TANZANIA (BOA) ASHINDA GARI LA KISASA

Gari aina ya Toyota Brevis lililotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana.
 
Meneja Uendeshaji Biashara wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA), Bw. Wasia Mushi akiwaonyesha waandishi wa habari gari mpya aina ya Toyota BREVIS lililotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana. Wengine ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Bw. Emanuel Moya (kulia) na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mirisho Millao.

Friday, February 27, 2015

AJALI YA NDEGE YA JWTZ MKOANI MWANZA

jw2 jw3 jw4 jw5

SERIKALI NA WADAU MBALIMBALI KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA MAKUNDI YALIYO KATIKA HATARI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU.

 Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed akionyesha moja ya chapisho lenye taarifa za tafiti za watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7 lililotambulishwa leo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) chapisho lenye taarifa za utafiti  kwa watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7  leo jijini Dar es salaam.

RAIS KIKWETE AHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU LEO

kj1Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima
zao za mwisho kwa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa
Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Msaki jijini Dar es
salaam leo. kj2Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji
Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea Msaki jijini Dar es
salaam leo walipofika heshima zao za mwisho kwa mama yake mzazi
Marehemu Esther Gigwa Hosea huko Msaki jijini Dar es salaam leo. kj3Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na Makamu
wa Rais Dkt Mohamed Ghariv Bilali, Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni
Sefue wakiwa pamoja na wafiwa wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther
Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward
Hosea huko Msaki jijini Dar es salaam leo. kj4Sehemu ya wafiwa na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Marehemu
Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Nkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Msaki jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

mam12 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki.mam11Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA DKT. EDWARD HOSEA, JIJINI DAR.

1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha zote na OMR
3
Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko.

ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA WILAYANI KYELA

ky1Waziri Mkuu,Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Kyela baada ya kufungua ukumbi wa  Halmashauri hiyo wakiwa katika ziara ya wilaya  hiyo Februari 26, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) ky14Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, MizengoPinda wakati aliozungumza baada ya kufungua mashine ya kukoboa nakuchambua mpunga mjini Kyela Februari 26, 2015. (PIcha na Ofisi  yaWaziri Mkuu)

SERIKALI KUFUFUA BANDARI 14 ZA ZIWA NYASA – WAZIRI MKUU

bu1
*Apewa jina la Chifu wa Wanyakyusa, aitwa Mwakabulufu
WAZIRI MKUU Mizengo amesema Serikali imeamua kufufua bandari ndogo 14 kwenye mikoa mitatu inayozunguka Ziwa Nyasa ili kuimarisha usafiri wa majini kwa wakazi wa Ruvuma, Njombe na Mbeya.
“Tangu mwaka 2006 bandari za kwenye mikoa ya Ruvuma, Njombe na Mbeya zilikufa na hivyo kuleta shida ya usafiri kwa wakazi wa maeneo hayo lakini Serikali imeamua kuzifufua bandari hizo na Itungi itakuwa ndiyo kituo kikuu cha bandari zote katika Ziwa Nyasa,” alisema Waziri Mkuu.
Alikuwa akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Kyela kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni (Jumatano, Februari 26, 2015) kwenye uwanja wa michezo wa Mwakangale na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa wilaya hiyo.
Alizitaja bandari hizo kuwa ni Ndumbi, Lundu, Njambe, Mkili, Liuli, na Mbamba bay ambazo ziko mkoani Ruvuma. Nyingine ni Lumbila, Ifungu, Nsisi, Lupingu na Manda ambazo ziko Njombe wakati bandari za Mbeya ni Itungi, Kiwira na Matema.
Alisema ili kufanikisha hilo, Serikali imehamisha chelezo (Dry Dock) kutoka bandari ya Mwanza na kwamba mkandarasi kutoka Kampuni ya Songoro Marines, ameshaanza  ujenzi wa chelezo hiyo.
“Baada ya kukamilika, Chelezo hiyo, itatumika kutengenezea meli mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo na kufanya ukarabati wa meli pindi zinapohitaji matengenezo. Nimeambiwa na mkandarasi kutaka watamaliza hii kazi ifikapo Juni, mwaka huu,” alisema huku akishangiliwa na umati huo.
Waziri Mkuu alisema, mbali ya hilo, chelezo hiyo pia itatumika kutengeneza matishari mawili ya kubebea mizigo ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 1,000  kila moja.
“Yatatumika kusafirisha mizigo hiyo hususan mazao ya wakulima kupitia bandari ndogo zilizopo lakini pia yatasafirisha tani 60,000 za makaa ya mawe, tani 72,000 za saruji kutoka Mbeya kwenda Malawi na mikoa jirani; tani 10,000 za mbolea kutoka Dar es Salaam pamoja na chuma kutoka Liganga na Mchuchuma,” alisema.
“Chelezo hiki kitakapokamilika kitakuwa kikubwa na cha aina yake… hakuna kingine cha kulinganishwa nacho katika nchi jirani za Malawi, Zambia na Msumbiji. Itumieni fursa hii kwa kutunza ule mto kwenye mdomo wa kuingilia bandari ya Itungi, msilime kwenye kingo za mto,” aliongeza.
Mapema, akizungumza na wakazi wa kata ya Lusungo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Lusungo, Waziri Mkuu Pinda alisema daraja hilo ni kiungo muhimu kwenye barabara hiyo iendayo kwenye bandari ya Matema.
Aliwataka wakazi wa kata hiyo walitunze daraja hilo ili liweze kuwasaidia kusafirisha bidhaa na mazao wanayolima. Ujenzi wa daraja hilo, ambalo limejengwa kupitia mfuko wa barabara, lina urefu wa mita 50 na upana wa mita 7.3 pamoja barabara yenye urefu wa mita 600 kutoka kwenye maingilio ya daraja hilo, limegharimu kiasi cha sh. bilioni 3.7 huku ujenzi wake ukiwa umekamilika kwa asilimia 99.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Pinda alipewa jina la MWAKABULUFU na Chifu Ernest Mwailemale wakati akisimikwa kuwa kiongozi wa eneo hilo la Lusungo. Waziri Mkuu alivishwa mgolole na kupewa mkuki ili autumie kuilinda nchi dhidi ya maadui kutoka pande zote.
Akizungumza mara baada ya kumsimika Waziri Mkuu, Chifu Mwailemale mwenye umri wa miaka 91, alisema jina hilo ni la babu yake mzaa baba ambaye aliwahi kutawala eneo hilo. Hata hivyo, hakutaja ni mwaka gani.
Alipoulizwa maana ya jina hilo, Chifu Mwailemale ambaye wakati wote alikuwa akizungumza Kiswahili kwa ufasaha alisema: “Jina hili halina maana maalum bali na heshima kwa sababu lilikuwa la Chifu aliyetawala eneo hili,” alisema na kufafanua kuhusu umri wake: “Nina miaka 91 kwa maana nilizaliwa tarehe 25 Septemba mwaka 1924,” alisema Chifu huyo ambaye anaelezwa kupigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania ahimiza vyama vya siasa kuzipatia ufumbuzi kasoro zinazojitokeza Zanzibar

index
Na Masanja Mabula -Zanzibar.
…………………………………………………………….
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Fionnuala Gilsenan amevihimiza vyama vikuu vya siasa Zanzibar  kuendeleza utamaduni wa kuzungumza na kuzipatia ufumbuzi kasoro zinazojitokeza ili Zanzibar iendelee kubaki katika hali ya amani, umoja na mshikamano.
Ametoa ushauri huo alipofanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza was Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad yaliyofanyika nyumbani kwake Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Dr. Msengi awaasa wananchi kusoma vitabu na machapisho mbalimbali

MSE2
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi Akizindua Nakala ya Katiba Pendekezwa ili ziweze kugawiwa kwa Mkoa wa Katavi,kushoto kwa Mkuu wa Mkoa Ni Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Emanuel Kalobelo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa huo.
MSE1
Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Mlele Wilbroad Mayala akipokea Nakala ya Katiba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Hamis Msengi kwa  niaba ya  Mkurugenzi ili vikagawiwekwa  kwa wananchi wa Halmashauri yake waweze kuvisoma.
…………………………………………………………………
Na Kibada Ernest-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Hamisi Msengi  amewaasa wakazi wa Mkoa huo kujenga utamaduni wa kusoma nyaraka mbalimbali ili kujijengea uelewa wa mambo muhimu, na  amewasisitiza wananchi wa Mkoa huo kusoma nakala za Katiba inayopendekezwa ili siku itakapofika ya kwenda kuipingia kura wawe na umaamuzi sahihi.
Dkt Msengi ametoa Rai hiyo wakati wa kikao kati yake na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa,  Wataalamu wa Kada mbalimbali, Taasisi za Serikali zilizopo katika Mkoa huo,Kamati za ulinzi na usalama   Wilaya na Mkoa, Watendaji wa Mitaa,Wazee Mashuhuri na Viongozi wa Madhehebu ya dini kilichofanyika jana(juzi)kwenye ukumbi wa Mikutano  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
  Kikao hicho  kilichoambatana na uzindua  wa Nakala za Katiba pendekezwa zilizoletwa Mkoani  Katavi ili ziweze kugawiwa kwa wananchi waweze kuzisoma na kuzielewa kabla zoezi la kuipigia kura Katiba pendekezwa muda utakapofika.
Amesema watanzania wamekuwa na tabia ya kutopenda kusoma nyaraka muhimu hivyo kuwa na tabia ya kudharau mambo ambapo nyaraka hizo ni muhimu kama Katiba inayopendekezwa iwapo wataisoma wataweza kuelewa kwa undani kilichoandikwa na watakapokwenda kupiga kura watakuwa na uamuzi wa kufanya, kwa kuwa watakuwa wanafahamu kile kilichoandikwa ndani ya Katiba pendekezwa.pia unaweza kuisoma ukaelewa na ukashindwa kutoa maamuzi.
“Tuondokane na ugonjwa huu wa kutokusoma tuwe na tabia ya kujisomea ili tuwe na uhakika wa mambo tunayoyafanya”amesema Dkt Msengi.
 Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai kwa wakazi wote wa Mkoa huo kujenga tabia ya kusoma nyaraka, na waisome Nakala ya katiba iliyopendekezwa na kuielewa na muda ukifika wa kupiga kura wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura ili watumie haki yao ya kidemokrasia.
Akaongeza kuwa ili uwe na fursa ya kupiga kura lazima ujiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.ili uweze kupiga kura kwa mjibu wa sheria lazima ujiandikishe.
Wakati ukifika wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura  wananchi wajitokeze kwenda kujiandikisha  na wale ambao hawataweza kujiandikisha watakosa fursa hiyo ya kidemokrasia ya kuipigia kura Katiba pendekezwa na kuwachagua viongozi wao ambao ni Madiwani Wabunge na Rais katika uchaguzi Mkuu utakapofanyika Oktoba mwaka huo.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mhandisi Emanuel Kalobelo  ameeleza kuwa Mkoa wa Katavi umepokea jumla ya Nakala 15,640,za Katiba Pendekezwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili ziweze kugawiwa kulingana na maelekezo ya ugawaji wa nakala za katiba hizo.
Mhandisi Kalobelo ameeleza kuwa mgao wa Nakala hizo umegawanywa  kwa mpangilio kama ilivyoelekezwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  iligawiwa nakala 3,900,Halmshauri ya Nsimbo Nakala 3,600,Halmashauri ya Mji Mpanda Nakala 3,600,Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Nakala 4,500, na wamekabidhiwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa.ambapo kwa upande wa Mkoa na taasisizilizopo katika mkoa huo  ulipokea nakala 40 kwa ajili ya kuzigawa kwenye Taasisi zilizopo katika Mkoa huo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima akimkaribisha Mkuu wa Mkoa amewaeleza Viongozi wote kuwa wanatakiwa kufikisha ujumbe kwa wananchi wao na wawahamasishe wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kujianadikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
 Pia amewasisistiza wapeleke nakala hizo kwa wananchi wazisome ili waweze kuwa na uamuzi wa kuipigia kura Katiba pendekezwa wakiwa na uelewa kuhusu Katiba hiyo Pendekezwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi ambaye pia ni  Afisa Tawala wa Mkoa wa Katavi Salum Shilingi akawaasa Viongozi hao kuwa ni Nakala hizo haziuzwi zinagawiwa bure,na lengo lake ni kuwagawia bure wananchi wazisome ,atakayepatikana akiziuza hatua kali zitachukuliwa juu yake.
Katika Hatua nyingine akapongeza Gazeti la Mpandaleo kwa kueleimisha Jamii ya Mkoa wa Katavi na Mikoa jirani kutokana na habari zake zinazoandikwa humu akasisitiza wananchi waendelee kulisoma kwa kuwa ni kioo na kielelezo cha Mkoa.

Tigo Yatoa Udhamini Kwa Washindi wa Tigo Ngorongoro Run Kushiriki Tigo Kili Half Marathon 2015

WAKI1Mwanariadha Alphonce Felix akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha. WAKI2 Mwanariadha Mary Naali akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha na kushoto ni Meta Petro Mjumbe toka riadha Tanzania pia ni kocha wa wanariadha hao.
WAKI3Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni ya Tigo kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon, Kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha na Kulia kwake ni mwanariadha Mary Naali na Mjumbe toka Riadha Tanzania Meta Petro. Mkutano huo ulifanyika Mkoani Arusha jana. WAKI4Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles (nyuma katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanariadha walioshinda mbio za Tigo Ngorongoro Run Marathon mwaka jana mara baada ya kutangaza udhamini wa Kampuni ya Tigo kwa wanariadha hao kushiriki mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon zitakazofanyika tarehe 1 machi Moshi Mkoani Kilimanjaro. Pembeni kulia mstari wa nyuma ni John Wanyancha Meneja wa Mawasiliano wa Tigo.
WAKI5 WAKI6Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles akipeana mkono na Alphonce Felix mara baada kutangaza udhamini wa Kampuni ya Tigo kwa wanariadha walioshinda mbio za Tigo Ngorongoro Run Marathon mwaka jana waweze kushiriki mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon zitakazofanyika tarehe 1 machi Moshi Mkoani Kilimanjaro. Pembeni anayeshuhudia ni Mwanariadha Mary Naali.

WANANCHI MICHEWENI WATAKIWA KUTOKUWA NA TAMAA YA FEDHA NA KUUZA ASHAMBA YAO MARA MBILI

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana akila kiapo kuchukuwa majukumu ya kuwa mkuu wa wilaya ya Micheweni.
PICHA NA MAKTABA
……………………………………………………………………………
Na Masanja Mabula -Pemba .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana ameitaka jamii kuepukana na tamaa ya fedha kwa kuuza mashamba yao watu zaidi ya mmoja ili kuepusha kutokea kwa migogoro ya ardhi katika maneo yao .
Amesema kuwa migogoro mingi ya ardhhi inayojitokeza siku hadi siku inasababishwa na jamii kwua na tama ya fedha hali ambayo inawafanya kukosa uwaminifu na hivyo kujikuta wakisababisha kuwepo na migogoro .
Akizungumza na wananchi wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika shehia ya Makangale Jimbo la Konde , Mkuu huyo wa Wilaya ameshusha presha za wananchi hao baada ya kuahidi kuipatia ufumbuzi migogoro hiyo .

Wafanyakazi Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waelezea namna wizara yao inavyoweza kufanikisha Mkakati wa Kitaifa kuhusu matumizi ya Kondomu

hab1Afisa Tawala wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Mussa Varisanga akielezea jambo wakati wa kikao cha pamoja na washauri kuhusu masuala ya Kondomu wakati wakijadili Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Kondomu unaoratibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mshauri wa Kimataifa kutoka Uganda Bw.Moses Muwonge
hab2Mshauri wa Kimataifa kutoka Uganda Bw.Moses Muwonge akizungumza na baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao cha pamoja kujadili kuhusu Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Condom unaoratuibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mshauri kutoka taasisi ya AMCA Bw. Patrick Kauyamwenge.
hab3Mwakilishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Ngaiza Alex akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na washauri kuhusu masuala ya Kondomu wakati wakijadili Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Kondomu unaoratibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshauri wa Kimataifa kutoka Uganda Bw. Moses Muwoge na Mshauri kutoka taasisi ya AMCA Bw. Patrick Kauyamwenge.
hab4Mwakilishi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Ngaiza Alex akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina ya maafisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na washauri kuhusu masuala ya Kondomu wakati wakijadili Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Kondomu unaoratibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshauri wa Kimataifa kutoka Uganda Bw. Moses Muwoge na Mshauri kutoka taasisi ya AMCA Bw. Patrick Kauyamwenge.
hab5Afisa Habari wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Zawadi Msalla (katikati) akielezea jambo wakati wa kikao cha pamoja na washauri kuhusu masuala ya Kondomu wakati wakijadili Mkatati wa Taifa wa Matumizi ya Kondomu unaoratibiwa na TACAIDS leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija, WHVUM

NJOO UPUNGUZE ‘STRESS’ ZA WIKI NZIMA KWA BURUDANI YA ‘LIVE MUSIC’ NA SKYLIGHT BAND LEO @THAI VILLAGE-MASAKI

It’s Friday and its on #TGIF, Skylight friday, wadau na wapenzi wa muziki wa live na wa kiwango cha juu,wote tunakutana Thai village Masaki, jioni hii kwa burudani safii toka kwa wakali wa town vijana wa Skylight Band,
Karibuni sana tuanze weekend yetu na burudani ya muziki wa live#
Come and experience good music from our young talented singers #Aneth Kushaba #John music & #Ashura #Sony Masamba #Sam Mapenzi bila kumsahau baba lao Joniko Flower mkongwe kwenye burudani ya muziki wa Live…ni balaaaaa na si ya kukosaa..
See you there #goodmusic #goodpeople
DSC_0042
30Mashabiki wa Skylight Band wakichizika na burudani kali iliyoenda shule yenye viwango na ubora wa kimataifa ndani ya kiota cha Thai Village ni kila Ijumaa ya wiki kuanzia saa tatu usiku mpaka usiku mwingi.

WAKUTANA KUJADILI MKAKATI WA MRADI WA KIJIJI CHA DIGITALI

DSC_0113Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akiwasilisha mada ya mchanganuo wa ufumbi wa changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha kidigitali.
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
WADAU mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi ambao wamo katika mradi wa kijiji cha dijiti cha Ololosokwan kilichopo wilayani Monduli Arusha wanakutana kwa warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji hicho nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Al Amin Yusuph warsha hiyo imelenga kuangalia changamoto na namna ya kuzitatua ili mradi kuwa na tija kwa wananchi wake.
Yusuph alisema kwamba wadau hao wanapanga mkakati kuangalia vipaumbele na changamoto katika utekelezaji wa mradi huo wa miaka mitatu.

MKURUGENZI WA TAMWA ATUNUKIWA TUZO YA CEFM CHAMPION

DSC_01311-1024x681 (1)Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mh. Alexandre Lévêque akimkabidhi tuzo ya kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA,Bi. Valerie Msoka kwa kufanikisha kampeni dhidi ya ndoa za utotoni.(Picha zote kwa hisani ya mtandao wa hivisasa.co.tz).
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka, amekuwa mtu wa kwanza kutunukiwa tuzo ya CEFM Champion, na Ubalozi wa Canada nchini.
Katika sherehe fupi iliyofanyika Serena Hotel 24 Februari 2015, Balozi wa Canada nchini Bwana Alexandre Leveque alisema kuwa Valerie Msoka amekuwa mwanaharakati wa kwanza kutunikiwa tuzo hiyo na ubalozi wake kama ishara ya kukubali mchango wake kupiga vita ndoa za utotoni, za kulazimishwa na ukeketaji kwa watoto wa kike nchini.
“Watoto wa kike na wanawake wamevumilia machungu ya ndoa za utotoni na za kulazimishwa hivyo wanahitaji mtu wa kuwasemea: mtu ambae ataelezea taarifa zao zinakazosaidia kuwaweka watu pamoja na kuleta mabadiliko yenye tija,”amesema Balozi Lévêque. Valerie Msoka atakuwa mtetezi. Ninafuraha kumtangaza kuwa Mtetezi wa CEFM wa Ubalozi wa Canada nchini Tanzania.”
Valerie ametumia ujuzi wake kama mwanahabari aliyebobea, mwanaharakati na mpenda maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali bila kujali litakalomtokea au kueleweka vibaya na jamii.
Ameandika taarifa zenye kuvuta hisia, huruma na kuhamasisha kasi ya mabadiliko Katika jamii na watunga sera,” alisema Balozi Leveque.

Al Shaimar Kweigyir, amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino,Yohana Bahati

Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir,
amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi
albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.
Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini
Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa
wa Mwanza, Crencencia Joseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Bayport
Financial Services mkoani Mwanza.

ALEX MSAMA ALIPIA ADA ZA WATOTO YATIMA KATIKA VITUO MBALIMBALI NCHINI

1Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kuhusu malipo mbalimbali yaliyotolewa kwa vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kulipia karo za wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali nchini, Msama ameyasema hayo wakati akizunguzia maandalizi ya sherehe zakutimiza miaka 15 kwa Tamasha la Pasaka zinazotarajiwa kufanyika Aprili 7 mwaka huu jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali Kusini mwa Afrika, Ukanda wa Maziwa Makuu na Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja  na Ulaya kutoka kule nchini Uingereza wanaotarajiwa kutoa burudani katika tamasha hilo litakaloshirikisha michezo mbalimbali pia, Kushoto ni Bw. Khamis Pembe mmoja wa waratibu wa tamasha hilo.

Mashindano ya gofu NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 kufanyika kesho viwanja vya TPDF Lugalo

4Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC  Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu  vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mpaka sasa wachezaji 60 wameshathibitisha kushiriki katika mashindano hayo na wachezaji wengine wanaendelea kujisajiri ili kushiriki katika michezo hiyo ya Gofu, Kapteni Japhet Masai ametoa mwito kwa wachezaji mbalimbali kuendelea kujisajiri na amesema wanatarajia zaidi ya wachezaji 120 watashiriki katika mashindano hayo.