Na Mwandishi Wetu
WAKAZI wa Mkoa wa Dodoma wametoa
wito kwa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, kuweka mkazo kwa
waimbaji watakaopanda jukwaani kwenye tamasha hilo mwaka huu ili
kuendana na miaka 15.
Kwa mujibu wa Katibu wa Kwaya ya
Mtakatifu Andrea ya mkoa ni humo, Wilson Hoya waimbaji wakiimba live
kwenye Tamasha hilo itakwenda sambamba na miaka 15 ya tamasha hilo la
kumuabudu na Kumtukuza Mungu.
Hoya alitumia fursa hiyo kutoa
wito kwa waandaaji wa tamasha hilo kuukumbuka na kuuweka katika orodha
ya mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo mwaka huu.
“Mwishoni mwa mwaka jana, Kamati
ilielekeza neno la Mungu katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea kwenye
Tamasha la Krismasi, tunaomba Tamasha la Pasaka Dodoma iwepo kwenye
orodha ya mikoa itakayopata upako kupitia tamasha la Krismasi,” alisema
Hoya.
Hoya alisema Dodoma ni mkoa
wenye fursa nyingi ambazo zinapatikana kwenye Tamasha la Pasaka ambalo
linasaidia maisha ya wakazi wengi wa mkoa huo.
No comments:
Post a Comment