MWIMBAJI chipukizi wa nyimbo za
injili Victor Mbagga, amesema anatamani kupata kibali cha kuimba kwenye
miaka 15 ya Tamsha la Pasaka linalotarajia kufanyika hivi karibuni
mikoa zaidi ya mitano.
Mbagga alilieleza kuwa endapo
atapata nafasi hiyo atakuwa amepata bahati ya kipekee ya kujitangaza kwa
kuwa watanzania watapata nafasi ya kujua anachokifanya.
Akizungumza katika ofisi za
gazeti hili Mbagga alisema kuwa ameanza kuimba tangu mwaka 2002 ambako
hadi sasa ana albamu ya Usilipize Kisasi, Furaha kuwa na Yesu na Utawale
Yesu ambayo itazinduliwa siku ya Pasaka. Lakini bado hajatambulika kuwa
yeye ni muhubiri wa injili kwa njia ya uimbaji.
Alisema kipaji chake
hakijulikani kwa sababu ya changamoto za kiuchumi hivyo anaamini kupitia
Tamasha la Pasaka linaloandaliwa na magwiji wa tamasha hilo Kampuni ya
Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam ataweza kujulikana kwa kuwa
linakusanya Watanzania na waimbaji wengi.
Mwimbaji huyo ambaye amekusudia
kufanya kazi na Msama Promotions huku akisisitiza kuwa ameona ni
kimbilio kwa waimbaji wengi kwa kuwa inafanya kazi vizuri ambapo
inasamabaza kazi nyingi ambazo zinafika mbali.
“Napenda kufanya kazi na mtu
mwenye hofu ya Mungu jambo lingine ni kwamba sisi waimbaji tunapata
changamoto kubwa ama hatujatoka kwa hiyo wanipatie kibali cha kushiriki
katika tamasha la mwaka huu waone nafanya huduma gani,” alisema Mbagga.
No comments:
Post a Comment