TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 24, 2015

SERIKALI NA WADAU MBALIMBALI KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA MAKUNDI YALIYO KATIKA HATARI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VVU.

fat1 Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed akionyesha moja ya chapisho lenye taarifa za tafiti za watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7 lililotambulishwa leo jijini Dar es salaam. fat2Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) chapisho lenye taarifa za utafiti  kwa watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7  leo jijini Dar es salaam.
fat4Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Meneja  Mpango wa Tume ya Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) Dkt. Robert Josiah (kushoto) chapisho lenye taarifa za utafiti  kwa watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7  leo jijini Dar es salaam. fat5Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya  Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akiwa ameshika chapisho lenye taarifa za utafiti  kwa watu walio katika makundi maalum  na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7  akiwa na baadhi ya watendaji wanaoongoza taasisi za kupambana na Ukimwi nchini . fat6 
Picha ya pamoja ya washiriki hao baada ya uzinduzi wa chapisho.
………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
SERIKALI imesema kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya kutoa elimu kwa makundi ya watu wanaotumia dawa za kulevya na wale wanaojihusisha na biashara ya ngono katika maeneo mbalimbali nchini  ili kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi .
Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Udhibiti na Usalama wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Mohamed Ally Mohamed wakati wa kutambulisha matokeo ya tafiti za watu walio katika makundi maalum yaliyo katika hatari ya kuambukizwa  Virusi vya Ukimwi  katika mikoa 7 iliyofanyiwa utafiti ambayo ni Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Iringa, Mara, Tabora na Shinyanga.
Akitambulisha matokeo hayo Dkt. Mohamed amesema kuwa hali ya maambukizi  mapya miongoni  mwa wanaume na wanawake katika maeneo yaliyofanyiwa utafiti imekuwa ikipungua kwa kasi ndogo licha ya juhudi kubwa  zinazofanywa na Serikali kwa na wadau mbalimbali kukabiliana na maambukizi hayo kutokana na makundi hayo kutobadili tabia.
Amesema maeneo mbalimbali yaliyofanyiwa utafiti na wataalam wa Wizara ya Afya, taasisi za kitaifa na Kimataifa zinazojihusisha na Ukimwi yameonesha uwepo wa tabia hatarishi zinazochangia maabukizi mapya ya VVU yakihusisha  makundi watu walio katika makundi maalum ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono, wanaume wanaofanya ngono ya jinsia moja pamoja na watu wanaojidunga dawa za kulevya.

Amefafanua kuwa katika mikoa 7 ambayo imefanyiwa utafiti huo hali ya maambukizi ya VVU kwa wanawake imeonekana kuwa kubwa pamoja na ongezeko la wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao huku idadi ya wanaojidunga dawa za kulevya ikikadiriwa kuwa kati ya 7,000 hadi 10,000.
“Hali ya maambukizi katika mikoa ulikofanyika utafiti ni kubwa, wanawake wana maambukizi makubwa,  idadi ya wanaojidunga dawa za kulevya inakadiriwa kuwa kati ya 7,000 hadi 10,000 huku kiwango chao cha maabukizi ya VVU kwa asilimia kikiwa asilimia 15.5 kiwango hiki ni kikubwa” Amesema Dkt. Mohamed.
  Kwa upande wake Meneja  Mpango wa Tume ya Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) Dkt. Robert Josiah akizungumzia kuhusu tafiti hizo amesema kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za taifa na kimataifa ilifanya tafiti tatu za makundi yaliyo katika hatari ya kuambukizwa VVU ili kubaini makisio ya idadi ya watu walio katika makundi hayo.
Dkt.Robert ameeleza  kuwa tafiti hizo zilifanyika katika vipindi tofauti kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 kwenye mikoa yenye viwango vya juu vya maabukizi ya VVU na kueleza kuwa mkoa wa Iringi unaongoza kwa kuwa na asilimia 9.1, ukifuatiwa na Mbeya 9.0%, Shinyanga 7.4%, Dar es salaam 6.9%, Tabora 5.1%, Mara 4.5% na Mwanza 4.2.
Amesema kwa kutumia matokeo hayo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweza kubaini changamoto mbalimbali na hali ya maambukizi ya VVU miongoni mwa makundi ya watu walio katika makundi hatarishi kwa lengo la kubaini mbinu mbalimbali za kutoa huduma za kinga, tiba na matunzo kwa watu walio katika makundi hayo.
“Kwa upande wetu tutatumia takwimu hizi kuboresha huduma ztu na kupanga mipango mbalimbali ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi nchini, lengo la NACP ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaondokana na maambukizi ya VVU” Amesema.
Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumzia matokeo ya tafiti hizo amesema kuwa ipo haja ya tafiti zinazofanyika nchini kuendelea kutazama jinsia zote ili kupata uhalisia katika jamii kwa makundi maalum.
Ametoa wito kwa Serikali na wadau mbalimbali kuzitumia takwimu zilizopatikana ili kufanya mabadiliko ya mbinu na njia za kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment