Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na wawakilishi kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mapema leo tarehe 23 Februari 2015 ofisini
kwake kujadili mchakato wa uanzishaji wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Mkoani Rukwa. Chuo Kikuu hicho kitaleta maombi maalum kwa uongozi
wa Mkoa wa Rukwa kuomba kupatiwa kambi ya Kianda iliyokuwa ikitumiwa na
Kampuni ya Aasleaf Bam International iliyokuwa ikijenga barabara ya
Laela – Sumbawanga kwa kiwango cha lami. Kwa upande wa Uongozi wa Mkoa
wa Rukwa unaona kuna haja kubwa ya kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Mkoani humo
kuweka chachu ya elimu na kusogeza huduma hiyo muhim zaidi kwa
wananchi. Kushoto kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ni Katibu Tawala Mkoa huo
Ndugu Smythies Pangisa.
Dkt.
Joseph Kihedu ambaye ni muhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema amefurahishwa na muamko wa
Serikali ya Mkoa wa Rukwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya
elimu pamoja na kiu yao kubwa ya kuona Mkoa unakua na Chuo Kikuu. Alisema
kuwa endapo Chuo Kikuu hicho kitapewa maeneo hayo bila shaka hakitasita
kuanzisha Tawi la Chuo hicho Mkoani Rukwa mbapo itakua ni fursa kubwa
kwa chuo hicho kujitanua zaidi katika kutoa elimu yenye ubora nchini.
Kutoka kushoto ni wawakilishi wengine kutoka chuo hicho ambao ni Ndugu
Michael John na Bi. Brenda Kazimili. Majadiliano
yakiwa yanaendelea. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella
Manyanya alisema Serikali ya Mkoa haitosita kutoa ushirikiano wa taasisi
yeyote ya elimu ya juu ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye lengo
la kuwekeza katika elimu Mkoani Rukwa. Amekitaka Chuo Kikuu hicho cha
Dar es Salaam kuendelea na nia yake ya kuomba maeneo hayo na kusema kuwa
Serikali ya Mkoa itatoa majibu sahihi kwa kile kitakachowezekana.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment