Mhe.
Samwel Sitta amewasili nchini Marekani siku ya Jumapili Februari 22,
2015 na baadae jioni kukutana na Watanzania wa DMV na kuwafafanulia
vifungu vya katiba iliyopendekezwa hasa kwenye swala la Serikali tatu na
kueleza ni kwanini CCM ilipendelea serikali 2 na pia kufafanua swala la
uraia pacha ambalo ndio kilio cha Diaspora na kuelezea kwa kina kifungu
hicho ndani ya katiba iliyopendekezwa Mtanzania yeyote mwenye uraia wa
nchi nyingine atakua na haki kama Mtanzania mwingine ikiwemo kumiliki
ardhi na kutochukua VISA anaporudi nyumbani. Jambo ambalo hataruhusiwa
ni kupiga kura au kugombea uongozi katika maswala ya siasa.
Baada
ya maelezo marefu na yenye ufasaha ya katiba iliyopendekezwa, Mhe.
Samwel Sitta pia aligusia shughuli za Wizara yake na mipango
anayotarajia kuifanya ikiwemo kuimarisha Reli ya kati, viwanja vya
ndege, Mwanza, Mbeya na Musoma na baadae kulikua maswali na majibu
ambayo watu wengi walionekana kuridhishwa na majibu mazuri na
yaliyowafumbua macho wanadiaspora huku Mhe. Samwel Sitta akisisitiza kwa
wasaidizi wake wawe wakitoa maelezo ya kina kwa Diaspora ili wasiwe
nyuma na nyumbani. AUDIO ya mkutano wote yakiwemo maswali na majibu
tutawawekea kesho msikie nini kimezungumuzia kwa wale ambao
hawakubahatika kuhudhuria mkutano huo wakiwemo Watanzania wa majimbo
mwengine. na wengine waliopo nje ya Tanzania.
Mwasho
Mhe. Samwel Sitta alimshukuru dada Loveness Mamuya kwa kuwasiliana na
ofisi yake na kuja na wazo la yeye kuja kufafanua vifungu vya katiba
iliyopendekezwea,
Waziri
wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta (kati) akiambatana na mwenyeji wake Balozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe.
Liberata Mulamula kuingia kwenye ukumbi wa Tabeer uliopo Hyattsville,
Maryland nchini Marekani.
Mhe.
JOhn Sitta akiwa na mwenyeji wake Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Liberata Mulamula, Mbunge wa
viti maalum CHADEMA Mhe. Leticia Nyerere pamoja na mmoja katika msafala
wa Mhe.Sitta wakiwa wamesimsma kwa ajili ya wimbo wa Taifa.
WanaDMV wakiimba wimbo wa Taifa mara tu baada ya mgeni rasmi kuingia ukumbini.
Mchungaji John Mbatta akiongea machache na kumshukuru Mhe. Samwel Sitta kuja kuifafanua katiba iliyopendekezwa kwa wanaDiaspora.
Rais wa
DMV Bw. Iddi Sandaly akitoa shukurani zake kwa Waziri wa Uchukuzi Mhe.
Samwel Sitta kwa kukubali kwake kuzungumuzia katiba iliyopendekezwa na
kuitolea ufafanuzi.
Mhe. Liberata Mulamula akiwashukuru wanaDMV kwa kujitokeza kwa wingi.
Waziri
wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta akisoma vifungu kwenye katiba
iliyopendekezwa na kuvitolea ufafanuzi. Wengine katika picha toka
kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani,
Mhe. Liberata Mulamula, Rais wa Jumuiya DMV Bwn. Iddi Sandaly na Mbunge
viti maaluum CHADEMA Mhe. Leticia Nyerere.
WanaDMV wakifuatilia mkutano.
Mhe. Samwel Sitta akiongea na mwenyeji wake jambo Mhe. Liberata Mulamula.
Mhe. Samwel Sitta akiongea jambo na mbunge wa viti maalum CHADEMA Mhe. Leticia Nyerere.
Benja
Mwaipaja akimpongeza Mhe. Samwel Sitta baada ya kujibia maswali yake kwa
ufasaha ikiwemo kama nayeye ataingia kwenye kinyang’anyiro cha urais na
Mhe. kujibu inategemea na wananchi wakijitokeza kumshawishi na Benja
kunyanyuka na kumpongeza na huku akisema nimekuotea ndoto tayari
Mheshimiwa huku wanaDMV wakivunjika mbavu kutokana na kitendo cha Benja
kumfagilia Mhe. Samwel Sitta.
Kwa picha zaidi bofya Bofys HAPA
No comments:
Post a Comment