Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer), Bw. Ahmed Mgoyi kwa ushindi wa jumla wa mabao 12- 9 dhidi ya timu ya Taifa kutoka nchini Kenya.
Timu ya Taifa ya Tanzania ya Sola
la Ufukweni, mwishoni mwa wiki iliibuka na ushindi wa mabao 7-6 katika
mchezo uliofanyika kwenye Ufukwe wa klabu ya Escape 1 eneo la Msasani
Jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake Bw. Malinzi
amesema ushindi walioupata timu ya soka la Ufukweni mwishoni mwa wiki,
umeitangaza vizuri nchi ya Tanzania na kuwataka Viongozi wa soka la
Ufukweni, makocha, wachezaji kutobweteka na ushndi huo, zaidi kujipanga
kwa maandalizi ya mchezo utakaofuata.
Baada ya kuitoa timu ya Taifa ya
Kenya, Tanzania watacheza na timu ya Taifa ya Misri mapema mwezi ujao
ambapo mchezo wa awali utafanyika jijini Dar es salaam kati ya mwezi
Machi 7, 8 na marudiano kufanyika baada ya wiki moja nchini Misri.
Endapo timu ya Taifa ya Tanzania
itaiondoa timu ya Taifa ya Misri, moja kwa moja itakata tiketi ya
kushiriki Fainali za Mataifa Afrika kwa Soka la Ufukweni 2015
zinazotarajiwa kufanyika Visiwa vya Shelisheli kuanzia April 14 – 19
mwaka huu.
Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa ujumla
wanawapa pongezi timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni kwa
ushindi huo na kuwatakia maandalizi mema kwa ajili ya mchezo unaofuata
dhidi ya Misri.
No comments:
Post a Comment