Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana akila kiapo kuchukuwa majukumu ya kuwa mkuu wa wilaya ya Micheweni.
PICHA NA MAKTABA
……………………………………………………………………………
Na Masanja Mabula -Pemba .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu
Khamis Mbwana ameitaka jamii kuepukana na tamaa ya fedha kwa kuuza
mashamba yao watu zaidi ya mmoja ili kuepusha kutokea kwa migogoro ya
ardhi katika maneo yao .
Amesema kuwa migogoro mingi ya
ardhhi inayojitokeza siku hadi siku inasababishwa na jamii kwua na tama
ya fedha hali ambayo inawafanya kukosa uwaminifu na hivyo kujikuta
wakisababisha kuwepo na migogoro .
Akizungumza na wananchi wakati
wa ziara yake ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika shehia
ya Makangale Jimbo la Konde , Mkuu huyo wa Wilaya ameshusha presha za
wananchi hao baada ya kuahidi kuipatia ufumbuzi migogoro hiyo .
Amekiri kuwa shehia ya Makangale
na Tondooni zinakabiliwa na migogoro mingi ya ardhi na kuwataka
wananchi wa shehia hizo kumpa ushirkiano ili aweze kutekeleza azma yake
ya utatuzi wa migogoro kwa lengo la kulinda amani na utulivu uliopo hapa
nchini .
“Migogoro ya ardhi inaweza
kuepukika iwapo kila mmoja atajiepusha na vitendo vya tamaa ya fedha na
kuuza maeneo kwa zaidi ya mtu mmoja , lakini cha msingi naomba mnipe
ushirikiano ili niweze kufanikisha leng la kuimaliza migogoro hii ”
alifahamisha .
Katika hatua nyingine Mkuu huyo
wa Wilaya ameitaka kamati ya maadili pamoja na polisi Jamii katika
shehia ya Makangale kufuata taratibu za kisheria katika kukusanya mapato
yatokanyo na ada ya magari yanayoingia kwenye ufukwe wa Vumawimbi kwa
kuhakikisha wanatoa risiti .
Amesema kuwa ni vyema Kamati ya
Maadili pamoja Polisi Jamii kushirikiana na taasisi za serikali
zinazohusika na masuala ya ukusanyaji wa mapato ikiwemo Halmashauri ya
Wilaya na kupanga mikakati ya mapato katika ufukwe huo .
“Tayari tumepokea taarifa kutoka
kwa wananchi kwamba hawapewi risiti wanapo fedha katika ufukwe huo na
kwamba hali inaweza kuitia dosari Serikali hiyo ni vyema wanaohusika na
ukusanyaji wa mapato kushirikiana na taasisi husika ” aliongeza .
Kwa upande wake Katibu
Tawala Wilaya hiyo Ahmed Khalid Abdalla amefahamisha kwamba ili
kuepusha migogoro ya ardhi Serikali ya Wilaya itaendelea na utaratibu wa
kukutana na wananchi pamoja na wawekezaji ili kutafuta suluhu kwa faida
ya umma .
Katibu Tawala
amewataka wawekezaji kuacha kupora ardhi za wananchi , na badala
wawashauri na kuwepo makubaliano ya pande zote zinazohusika .
“Pamoja na jamii kuwa
na tama ya fedha lakini kwa upande mwengine wawekezaji nao wamekuwa
wakisababisha migogoro kwa kuchukua maeneo ya wananchi bila ya ridhaa za
wenyewe” alifahamisha .
Uchunguzi uliofanywa
na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwepo na migogoro ya ardhi zaidi
ya tano (5) katika shehia ya Makangale na Tondooni ikiwemo inayohusu
wawekezaji na jamii , Viongozi wa Serikali na wananchi pamoja na
wananchi wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment