Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya
ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015
katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.
Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika
mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali
akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini
zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto.
Hata hivyo, rubani wa ndgevita
hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa
kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa
kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa
kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .
Wananchi wasiwe na hofu hii ni
ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu
ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo
mbinu.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
No comments:
Post a Comment