Na Fidelis Butahe, Mwananchi
- Amesema sheria ya maadili ya viongozi wa umma haina nguvu ya kukabiliana na mmomonyoko huo na inakosa meno kwa sababu inasimamiwa na watu walewale wasiotaka ‘kuguswa’.
Akigusia suala la maadili na sakata la mabilioni
ya fedha yaliyochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow alisema, “Katika
suala la escrow niliuliza nani msafi…, we subiri tu si tunakwenda katika
uchaguzi mkuu viongozi watakuwa na fedha nyingi sana.”
Kura ya maoni isubiri 2016
Akizungumzia daftari wa wapigakura na upigaji wa
Kura ya Maoni kupitisha Katiba Inayopendekezwa, alisema, “Nia ya
kupitisha Katiba mpya mapema ilikuwa na lengo la kuitumia katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, lakini inahitaji maandalizi. Mfano Katiba
Inayopendekezwa ina sehemu ya Tume ya Uchaguzi na kama ukiipitisha,
utaunda upya tume hiyo na suala hilo linahitaji muda.”
Alisema ili kufanikisha uundwaji wa tume hiyo ni
lazima Bunge likutane, lakini mpaka itakapofika siku ya kuipigia kura
Katiba hiyo na kuipitisha, Bunge litakuwa limekwishakaa na hakutakuwa na
uwezekano wa kubadili lolote.
“Hakuna haja ya kuharakisha, ni vizuri twende taratibu ili tusije tukafanya makosa ambayo yatatuletea matatizo,” alisema.
Aliongeza, “Itakuwa vizuri kama kura ya maoni
ikasitishwa mpaka mwaka 2016. Inaonekana tutalazimika kusubiri na hii
inatokana na matatizo tu ya kawaida ya kutokuwa na daftari la
Wapigakura.
Mgongano wa maslahi
Jaji Warioba pia aligusia kitendo cha wajumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba kuruhusiwa kugombea nafasi za kisiasa baada ya
kumalizika kwa Bunge hilo, akisema kuwa hilo lilikuwa kosa kubwa.
“Uganda tume ilipomaliza kazi, wananchi walichagua
Bunge la Katiba na sharti moja ni kwamba ukiingia katika Bunge hilo
hauruhusiwi kugombea uongozi. Walijua kazi yao ni kupitisha Katiba tu,”
alisema.
Alisema kosa lililofanyika nchini ni kuruhusu
wabunge waliopitisha Katiba kugombea, hivyo kuwafanya baadhi kuondoa
masuala ya msingi waliyoona kuwa ni kikwazo kwao katika uchaguzi.
“Nadhani hiyo ni kasoro tuliyokuwa nayo na tulipeleka watu ambao wana malengo na Katiba kwa manufaa yao binafsi,” alisema.
Kuhusu maridhiano kuelekea upigaji wa Kura ya
Maoni alisema, “Suala la maridhiano lilipofika kwenye vyama vya siasa
likabadilika na sasa tunazungumzia maridhiano ya vyama vya siasa.
Maridhiano ya vyama vya siasa siyo lazima yawe maridhiano ya wananchi.”
No comments:
Post a Comment