RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASMI UENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na
Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia
kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International
Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Kenyatta International Convention
Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20,
2015
2015

Rais Jakaya
Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa
wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya
wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20,
2015
Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa
wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya
wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20,
2015
.jpg)
Kutoka
kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais
wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho
Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni
(Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni
(Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki
.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa EAC kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari
20,2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi. Picha na IKULU
=======================================================
Tanzania inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na
muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jijini
Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita “Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla” Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika,miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo wala ya baadaye.
Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita “Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla” Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika,miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo wala ya baadaye.
Rais Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia
utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa
kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha
wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya
kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda,Tanzania na Uganda.
utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa
kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha
wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya
kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda,Tanzania na Uganda.
Rais Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara
imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona matunda hayo.
Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC
imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6
ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia
6.“Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika,
ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia
wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano
wetu” Rais amesema na kuongeza kuwa ” kwa njia hii serikali
zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika
kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea
mazingira mazuri”.
imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona matunda hayo.
Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC
imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6
ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia
6.“Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika,
ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia
wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano
wetu” Rais amesema na kuongeza kuwa ” kwa njia hii serikali
zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika
kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea
mazingira mazuri”.
Rais
Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa
na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan
Kusini ambaye amehudhuria ka ma mualikwa maalum katika kipindi
hikiambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza
kupatauanachama katika EAC yanaendelea.
CHUO CHA MAENDELEO YA UTALII ZANZIBAR CHAFANYA MAHAFALI YA SITA
……………………………………………………………
Na Faki Mjaka- Maelezo Zanzibar
Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Saada Mkuya amewataka Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar kutoitegemea Serikali katika kupata ajira badala yake wajikite katika kujiajiri wenyewe.
Amesema nafasi za Ajira Serikalini ni chache hivyo Wahitimu hao wanapaswa kujishughulisha ili wajiajiri wenyewe au kupitia Taasisi Binafsi.
Waziri Mkuya ameyasema hayo alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wahitimu wa Mahafali ya Sita ya Chuo cha Maendeleo ya Utalii yaliyofanyika leo kati viwanja vya Chuo hicho Maruhubi Mjini Zanzibar.
Amesema dhana ya kuitegemea Serikali katika ajira kwa sasa haina nafasi kutokana na uchache wa Ajira na kwamba anaamini Elimu waliyoipata Wahitimu inaweza kuwasaidia katika kujiajiri.
Ametoa Rai kwa Wahitimu hao kujiunga na Kampuni za Ulinzi ambazo zinatarajiwa kuanzishwa Zanzibar kutokana na kuripotiwa kwa matukio mbalimbali ya kihalifu nchini.
Aidha Waziri Mkuya amewashauri Wahitimu hao kutotosheka na kiwango cha Elimu walichofikia badala yake wajiendeleze mbele ili kupata ufanisi katika kazi zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chuo hicho Bi Zulekha Khamis Omar amesema Chuo hicho kinazidi kupiga hatua kimaendeleo nakwamba Wanatarajia kuanzisha Masomo ya Shahada ya Kwanza mwaka 2017-18.
Amesema mipango ipo mbioni kukamilika kuhusu kuanzishwa kwa Masomo ya Shahada ambapo Chuo hicho kitakuwa Chini ya Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA
Hata hivyo Bi Zulekha alizitaja Changamoto zinazokabili Chuo hicho kuwa ni pamoja na Uhaba wa Vifaa katika Jiko, na Mmommonyoko wa Ardhi unaotishia Mazingira ya Chuo hicho.
Chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 1992 ili kuongeza ukuaji na Maendeleo ya Utalii Zanzibar kimefanya Mahafali yake ya sita ambapo Jumla ya Wahitimu 511 wa Ngazi za Stashahada na Cheti katika Fani mbalimbali wamehitimu.
RAIS DR. SHEIN AFUNGUA MSIKITI MAKUNDUCHI
MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE SHEREHE YA MAULID YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) HUKO WETE-PEMBA
Na Anna Nkinda – Pemba
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanawake wa mkoa wa Kaskazini Pemba kuhakikisha watoto wao wanasoma kwa bidii hadi elimu ya juu kwa kufanya hivyo wataweza kuzitumia fursa zilizopo na kushika nafasi mbalimbali za uongozi na hivyo kufika ngazi ya maamuzi.
Mama Kikwete alitoa rai hiyo jana wakati wa sherehe za Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizoandaliwa na wanawake wa madrasa ya Jabal – Hiraa na kufanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Utaani Kaskazini Pemba.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema Mtume Muhammad S.A.W. alisimamia umuhimu wa elimu kwa kuona kuwa ili kuweza kuishi na kustawi katika dunia hakuna budi kupata elimu zote ya ahera na ya duniani ambayo itawezesha kufungua milango ya fursa za duniani na za akhera.
“Sisi waislamu tumekuwa tukilalamika kuachwa nyuma kimaendeleo na wenzetu. Sababu kubwa ni kutotia mkazo kwenye elimu na hata pale tunapowasomesha watoto wetu skuli basi tunapuuzia ile ya watoto wa kike. Hili bahati mbaya liko kwetu sisi waislamu wa Afrika”.
Mimi nimebahatika kutembea duniani, nimeona wanawake wa kiislamu, tena kutoka nchi za kiislamu wakifanya mambo makubwa, wana vyeo na daraja kubwa kutokana na elimu na ustadi wao. Hawajaacha kuswali, hawajaacha kuolewa, wala kuacha kuwa wake wa kiislamu”, alisema Mama Kikwete.
Alitoa mfano wa nchi ya Misri ambapo asilimia 49 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni wanawake na ni waislamu. Iran asilimia 60 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni wanawake.
Alisema wasiposomesha watoto wao haswa watoto wa kike wataendelea kujitumbukiza katika umasikini na hatimaye kuchuma dhambi kwa kuwaonea husda waliofanikiwa. Mtoto wa mama wa kiislamu aliyesoma, naye ana nafasi kubwa ya kuwa na mafanikio katika maisha.
Kwa upande wa malezi aliwasihi wanawake hao kuwa chanzo cha mabadiliko kwani wao ndiyo walezi wa watoto na Taifa, wawalee watoto katika unyenyekevu, kwa imani na kuhakikisha wanavaa mavazi ya heshima yanayokubalika katika jamii yao.
Mama Kikwete pia aliwahimiza wanawake hao kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu kwakuwa maisha ya binadamu yanasiasa ndani yake na siasa huleta maendeleo. Kwa wale watakaojitokeza wawaunge mkono na kuchagua amani, usalama na maendeleo.
Alihimiza, “Jitokezeni kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura zoezi la kujiandikisha litaanza wakati wowote. Safari hii vitatumika vitambulisho vipya vya kisasa. Wasiojiandikisha na kupata vitambulisho hivi hawataweza kupiga Kura ya Maoni ya Katiba inayopendekezwa wala kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu”.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla alimshukuru Mama Kikwete kwa kukubali kwake kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo na kumuomba Mwenyezi Mungu amzidishie kheri katika maisha yake.
Aliwasisitiza kina mama waliohudhuria sherehe hizo kutenga muda wao kwa ajili ya kwenda madrasa kupata elimu ya ahera na pia wajifunze elimu ya dunia ambazo zitawasaidia katika maisha yao .
“Katika suala la elimu wanawake tuko nyuma kwa madai kuwa tunashughuli nyingi za kifamilia na hivyo kukosa muda wa kujifunza, nawaomba tengeni muda wenu mkajifunze kwani kutokuwa na elimu ya dini na dunia kutakufanya siku moja ukashindwa kufanya mambo ya maana pale utakapokutwa na tatizo ukiwa peke yako”, alisema Mwanajuma.
Akisoma risala ya madrasa Jabal – Hiraa Khadija Suleiman Muhammed alisema ilianza na wanawake watatu na mwanaumme mmoja ambaye ni Mwenyekiti hadi sasa ina wanafunzi 104 kati ya hao wanawake 63 na wanaume 41.
Khadija alisema walimu wa madrasa hiyo wanafundisha kwa njia ya kujitolea hujipatia kipato kwa kualikwa katika shughuli za Maulid na katika shughuli hizo hutumia mashine za kukodi lakini kama watakuwa na mashine zao zitawasaidia kutatua matatizo waliyo nayo.
Alizitaja mashine hizo kuwa ni boxi mbili za spika, pawa yenye warts 2000, wireless mic mbili na mixer thamani yake ikiwa ni shilingi milioni tatu na laki moja.
“Tunawakumbusha viongozi wa dini tutumie nafasi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu kuielimisha jamii kuacha kuuza au kutumia madawa ya kulevya na kujilinda na ugonjwa wa Ukimwi kwasababu ndiyo janga kubwa kwa taifa letu”, alisema Khadija.
Aliyataja mafanikio waliyoyapata kuwa ni wakati madrasa hiyo inaanza walikuwa wanatumia jengo la mtu lakini hivi sasa wamefanikiwa kupata kiwanja na kujenga jengo la vyumba vinne ambalo halijakamilika lenye madarasa ya kusomea mawili, chumba cha wageni kimoja, ofisi moja na vyoo viwili.
Mama Kikwete aliipatia madrasa hiyo mifuko 25 ya saruji ambayo waliihitaji kwa ajili ya kumalizia ujenzi, vitabu vya kusomeshea vya Mas-hafu na juzuu. Pia aliahidi kuziunga mkono madrasa nyingine sita zilizohudhuria sherehe hiyo.
WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU UKARABATI MAABARA ZA ZAMANI
*Asema ni lazima zijengwe mpya, akataa kutoa mchango
……………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amepiga marufuku ukarabati wa maabara za shule za sekondari na kusisitiza kwamba ni lazima zijengwe mpya kama ambavyo Serikali ilielekeza.
Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Februari 21, 2015) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Ilula, mara baada ya kukagua ukarabati wa maabara za sayansi kwenye shule ya sekondari Ilula, wilayani Kilolo, mkoani Iringa.
“Mmefanya ukarabati kwenye jengo lililojengwa zaidi ya miaka 20 iliyopita. Kuna chumba nimekuta ni kidogo mno sababu hakiendani na specifications za sasa… chumba kimoja kimepasuka ukuta, hapana! RC kama kuna nyingine ya aina hii kazi isiendelee,” alisema.
“Huu ukarabati mliofanya ni kinyume na maelekezo ya Serikali ya kutaka zijengwe maabara mpya. Tulisema zijengwe maabara mpya ili ziweze kudumu kwa miaka mingi kidogo. Kuna chumba ceiling board iko chini kwa sababu ujenzi ni wa zamani. Ujenzi wa sasa mapaa yako juu zaidi ili kuruhusu hewa ya kutosha,” aliongeza.
“Ningeweza kusema vunjavunja lakini haitakuwa haki kwa sababu kuna fedha za watu zimetumika… kwa sasa yatatuhifadhi kwa muda kidogo, lakini haya majengo hayatadumu hata kidogo,” alisema.
Waziri Mkuu pia alikataa kuahidi mchango aliiombwa achangie na kuwaeleza kwamba atakuwa tayari kuchangia ujenzi wa jengo jipya na siyo ukarabati kwani huo utakuwa ni upotevu wa fedha. Majengo aliyoonyeshwa Waziri Mkuu Pinda yalijengwa mwaka 1995 na yalikuwa yakitumika kama maabara kwenye sekondari hiyo.
Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Amina Masenza asimamie watu wake ili ujenzi wa maabara uweze kukamilika kwa muda uliopangwa. Mkoa huo unahitaji mabaara 72 na zilizokamilika ni maabara tano tu huku nyingine 53 zikiwa kwenye hatua mbalimbali za ujenzi na 13 bado ziko kwenye msingi na moja iko kwenye linta.
Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mtendaji wa Kata ya Ilula, Bw. Titus Katemo alisema shule ya sekondari Ilula ilijenga maabara zake mwaka 1995 kwa nguvu za wananchi na kwamba zilikuwa zikitumika toka kipindi chote hicho.
Alisema ili kuendana na matakwa ya Wilaya, ukarabati wa vyumba vitatu ulianza Novemba 15, mwaka jana kutokana na vyumba hivyo kutumiwa na watahiniwa wa kidato cha nne wa mwaka 2014 kwenye mitihani ya vitendo.
“Makisio ya gharama za ukarabati wa vyumba vitatu yalikuwa ni sh. 38,294,775.00 na tunatarajia ukarabati utakamilika ifikapo tarehe 30 Machi 2015,” alisema na kumuomba Waziri Mkuu awasaidie awaunge mkono kwa mchango kwani kasi ya wananchi kuchangia imekuwa ndogo.
Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Kilolo na mchana huu anaenda kukagua mradi wa umwagiliaji wa Nyanzwa na pia atazungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara.
Solly Mahlangu achomoza Tamasha la Pasaka
Na Mwandishi Wetu
MASHABIKI wa muziki wa Injili nchini wameomba
waandaaji wa Tamasha la Pasaka wahakikishe msanii Solly Mahlangu
‘Obrigado’ wa Afrika Kusini anakuwepo kwenye tamasha la mwaka huu.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema jana
katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa wamepokea simu nyingi
kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki huo wakitaka msanii huyo aalikwe
katika miaka 15 ya Tamasha la Pasaka mwaka huu.
“Inaonekana
Watanzania walifurahia sana kazi ya Solly Mahlangu mwaka juzi katika
Tamasha la Krismasi, karibu kila anayepiga simu ya kupendekeza msanii,
jina hilo lazima.
“Sasa bado
tunaendelea kupokea ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali, ambapo mpaka
sasa Rebecca Malope na huyo Mahlangu wamekuwa wakipigiwa kura sana kwa
waimbaji wa nje,” alisema Msama.
Mahlangu ni
muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa Injili Afrika
ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa baadhi ya nyimbo zake.
Mbali ya kuwa
maarufu katika nyimbo za Iinjili nchini mwake, pia ni Mchungaji ambaye
ana uwezo wa kufanikisha muziki wa Injili na kanisa lake ambalo ni Word
Praise Christian Centre Intenational lililoko Tembisa.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA MWANZILISHI WA USKAUTI DUNIANI, LORD ROBERT STEVENSON SMYTH BADEN-POWELL, JIJINI DAR.
FAINALI DARAJA LA KWANZA KUCHEZWA CHAMAZI .
Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), inatarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TTF imepelekea mchezo huo kuhamishiwa Chamazi.
Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.
Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia.
Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.
Wakati huo huo, Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo (Jumamosi) katika viwanja vitatu tofauti, Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ndanda FC ya Mtwara watawakaribisha Wagosi wa Kaya timu ya Coastal Union kutoka jijini Tanga katika mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Ngwanda Sijaona.
Huku wakata miwa wa Kagera Sugar wanaoutimia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakiwakaribisha Maafande wa Jeshi la Polisi kutoka mjini Morogoro timu ya Polisi.
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea tena kesho jumapili katika viwanja vitatu tofauti, Uwanja wa Chamazi wenyeji Azam FC wataikaribisha timu ya maafande wa Jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons, mchezo utakaonza majira ya saa 2 kamili usiku.
Mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United wataikaribisha Simba SC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City wakicheza na timu ya Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI KUHUSU MAOMBI YA TPDC YA TOZO ZA HUDUMA ZA KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI ASILIA
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi Na. TR-G-14-039 kutoka kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni ya kukokotoa tozo za huduma ya kuchakata na kusafirisha Gesi Asilia, na mapendekezo ya bei ya uchakataji na usafirishaji wa gesi asilia. 2. Kati ya Septemba 2014 na Januari 2015, EWURA ilifanya uchambuzi wa kupitia gharama za ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia, muundo wa mtaji (capital structure) na faida ya mtaji, gharama za uendeshaji wa mradi, pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC. 3. Kwa mujibu wa ombi husika, TPDC waliiomba EWURA kuidhinisha vipengele vifuatavyo: (a) kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034;(b) tozo kwa huduma ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iwe Dola za Marekani 4.178 kwa uniti (MMBtu) kwa muda wa miaka mitatu ya kwanza;(c) faida kwenye mtaji ya asilimia kumi na nane (18%) na muundo wa mtaji wa asilimia hamsini mkopo na asilimia hamsini fedha za TPDC (50:50); na (d) mwezi Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA. 4. Kwa mujibu wa kifungu 19(2)(b) cha Sheria ya EWURA (Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 27 Novemba 2014, EWURA ilianza mchakato wa taftishi kukusanya maoni na hoja za wadau kuhusu uhalali wa ombi lililowasilishwa na TPDC. Wadau waliowasilisha maoni na hoja mbalimbali ni Baraza la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (CCC), Baraza la Ushauri la Serikali kuhusu Huduma za Nishati na Maji (GCC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kampuni ya Saruji Tanzania (TPCC), PanAfrican Energy Tanzania Limited, Songas Limited, Maurel & Prom, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji, na Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, hoja za wadau na ufafanuzi uliotolewa na TPDC vimezingatiwa na EWURA katika kutoa uamuzi wa ombi hilo. 5. Tarehe 8 Januari na 6 Februari 2015, EWURA ilifanya mikutano na wadau wa karibu (Exit Conference) ambapo EWURA ilisambaza rasimu ya Agizo la EWURA (Draft Order) ili ijadiliwe na kupata maoni ya mwisho; na mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha, CCC, GCC, TANESCO, TPDC, PAT, Songas, na TPCC. Asasi zote hizo zilitoa maoni ya mwisho kwenye rasimu ya Agizo la EWURA. Kwa ujumla, EWURA imezingatia maoni yaliyopatikana katika mikutano hiyo na hatimaye kufikia maamuzi kwenye Ombi la TPDC. 6. Katika kikao chake cha tarehe 19 Februari 2015, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, ilijadili Ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha miezi mitatu (Interim Tariff) ambacho TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA iliyahoji. Maamuzi yaliyotolewa ni kama ifuatavyo: (a) kanuni ya kukokotoa tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia iliyoombwa ilirekebishwa na kupitishwa ili itumike kwa miaka 20 kuanzia mwezi Aprili 2015, na kurekebishwa kila baada ya miaka mitano; (b) gharama za Mradi wa Bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara-Dar es Salaam zilizopitishwa ni sawa na Dola za Marekani 1,331.51 milioni, ambapo gharama hizi zitabaki hivyo hadi mwezi Juni 2015 ambapo gharama halisi za mradi zitakapojulikana na kufungwa;
Continue reading →
DR. SHEIN AZINDUA MADRASA MAKUNDUCHI
Vijana wa Halmashauri za Kibondo na Kakonko waishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Picha na Frank Shija, WHVUM
No comments:
Post a Comment