Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ametoa wito kwa waandaaji wa Tamasha
la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions kuongeza ufanisi kwa kuongeza
chachu kwa waimbaji kuiombea amani Tanzania hasa katika kipindi hiki cha
kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kinana sambamba na
hilo kwa pamoja tuiombee nchi yetu umoja, amani, mshikamano ambako
tamasha hilo litumike kumuomba Mungu kufanikisha umoja kwa Watanzania
ulioasisiwa na baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Kinana alitumia fursa hiyo
kuwatakia heri na fanaka Wakristo wote duniani heri na fanaka katika
sherehe hizo ambazo ni kumbukumbu kubwa kwao ambayo haifanani na
nyingine za kijamii.
Aidha Kinana alimpongeza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama kwa kuwaunganisha
Watanzania wa madhehebu mbalimbali na kuwa kitu kimoja na kudumisha
mshikamano katika jamii.
Kinana alitumia fursa hiyo kutoa
wito kwa mashabiki na wapenzi wa tamasha hilo kujitokeza kwa wingi ili
kufanikisha mipangilio ya Msama katika kuisaidia jamii ya Watanzania.
Kinana ni mmoja wa Makatibu wa
CCM wanaotekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kuweza kurudisha heshima
ya chama kilichopoteza mwelekeo, hivi sasa CCM imerudisha heshima kama
ilivyokuwa kwenye uongozi wa baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere.
No comments:
Post a Comment