Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu
katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC
Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia
saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji
mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mpaka
sasa wachezaji 60 wameshathibitisha kushiriki katika mashindano hayo na
wachezaji wengine wanaendelea kujisajiri ili kushiriki katika michezo
hiyo ya Gofu, Kapteni Japhet Masai ametoa mwito kwa wachezaji mbalimbali
kuendelea kujisajiri na amesema wanatarajia zaidi ya wachezaji 120
watashiriki katika mashindano hayo.
Shindano la NIC Corporate Golf Chalennge linaandaliwa na shirika la bima la taifa NIC na
linafanyika kila mwaka kuanzia tangu lilipoanzishwa mwaka 2013 na
linashirikisha wachezaji wa rika zote na jinsia zote NIC imeandaa zawadi
mbalimbali kwa washindi, ambapo mshindi wa kwanza atapata jiko kubwa la
umeme. Pia wshindi wengine watapata zawadi mbalimbali zilizotayarishwa
kwa ajili yao ambazo ni meza kubwa ya ofisini, mikoba ya akina mama,
mabegi ya wanafunzi, Feni , Friji, Microwave na zawadi nyingine
nyingi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta akikabidhi zawadi kwa ya jiko kubwa la umeme Japhet Masai
Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta na Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya
gofu vya TPDF Lugalo wakipiga picha pamoja na zawadi hizo. Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi
Shemweta akipiga picha mara baada ya kukabidhi zawadi hizo kwenye
viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo.
No comments:
Post a Comment