TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 25, 2015

WARSHA YA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUZUIA UKATILI DHIDI YA WATOTO NCHINI TANZANIA YAfanyika KILIMANJARO

 
 Julieth Swai Mwakilishi kutoka UNICEF akizungumza jambo
 Baadhi ya washiriki wa Warsha wakifuatilia kwa makini
 Mmoja wa  washiriki wakiuliza maswali katika warsha hiyo
 Kimela Bila Mwandaaji wa Kipindi cha Walinde Watoto akizungumza katika Warsha hiyo
 Mathias Haule, Afisa Maendeleo ya Jamii maswala ya Ukatili dhidi ya Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akielezea Sheria ya Mtoto
 Washiriki wa Warsha inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania
…………………………………….
 
Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto kwa ushirikiano na UNICEF wameandaa warsha ya siku tatu
inayohusu nafasi ya vyombo vya habari katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto
nchini Tanzania.
Warsha hiyo inayofanyika mjini Moshi inashirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wawakilishi kutoka Mkoa wa Kilimanjaro, Wawakilishi kutoka wilaya za Hai na Moshi Manispaa, wawakilishi kutoka UNICEF pamoja na wawakilishi wa redio 14 zinazorusha kipindi cha Walinde Watoto. Wengine ni wawakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania, mwakilishi kutoka Csema pamoja na waandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto kampuni ya True Vision Production.
Akifungua warsha hiyo,
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro, Paul Shayo alilishukuru
shirika la Watoto Duniani (UNICEF) kwa kazi nzuri ambazo wamekuwa wakizifanya
kwa kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa Haki za Watoto zinatekelezwa
hapa nchini. 
 
Paul alitaja aina za
ukiukwaji wa haki za mtoto hapa nchini kuwa ni pamoja na kuolewa katika umri
mdogo, kutumikishwa katika mashamba na ukatili dhidi ya watoto. Hata hivyo
aliendelea kuzitaja athari mbalimbali zinazotokana na ukiukwaji wa haki hizo
kuwa ni pamoja na watoto kukatishwa masomo na kukosa haki ya kuendelezwa
na kwamba ndoa za utotoni zina madhara kiafya hasa wanapopata ujauzito na
kujifungua katika umri mdogo. 
 
Paul alimalizia kwa
kutoa rai kwa washiriki wa warsha hiyo na kuwataka wakawe chachu ya kuzuia
ukatili dhidi ya watoto katika maeneo waliyotoka na kushirikiana na wadau
waliopo katika ngazi za vijijini, mikoani na mijini kadri inavyowezekana ili
kuwalinda watoto na kutokomeza ukatili dhidi ya watoto.
 
Vipindi vya Walinde
Watoto vinarushwa na redio 14 ambazo ni Radio Jamii Kilosa, Country FM, Boma
Hai FM, Radio Quran, ZBC pamoja na Redio Kitulo.
 
Nyingine ni TBC Taifa,
Bomba FM, Faraja FM, Uplands FM, Ice Fm, Radio Maria, Radio Kwizera na Zenj FM.
Vipindi hivi vinapatikana pia katika tovuti ya www.walindewatoto.org na
kupitia www.facebook.com/WalindeWatoto

No comments:

Post a Comment