Mgeni
rasmi kwenye mafunzo ya stadi za kazi na utambuzi wa fursa za kiuchumi
zilizopo mkoa wa Lindi Naibu waziri wa kazi na ajira mhe.Dr. Makongo
Mahanga (MB) amewataka vijana wa mkoa wa Lindi kuyageuza mafunzo
watakayoyapata ya stadi za maisha sanjari na kuzitambua fursa zilizopo
ndani ya mkoa, waweze kujiajiri na kujikomboa kiuchumi,wakati wa
uzinduzi wa mafunzo hayo ambapo jumla ya vijana 360 kutoka halmashauri
sita zilizopo mkoani Lindi wameudhuria kwenye ukumbi wa kanisa katoliki
Mt.Kagwa
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza akiwaeleza washiriki wa mafunzo ya
stadi za maisha sambamba na kufahamu fursa za kiuchumu ambapo mpango wa
kuendesha mafunzo hayo umebuniwa na yeye mwenyewe,mbele ya mgeni
rasmi,wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Vijana
360 kutoka kwenye wilaya za Kilwa,Ruangwa,Liwale,Nachingwea,Lindi Mjini
na Vijijini ambao ni washiriki wa mafunzo wakimsikiliza kwa makini
mgeni rasmi naibu waziri wa kazi na ajira Mhe.Dr.Mkaongoro Mahanga
hayupo pichani.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza akiwaeleza waandishi wa habari jambo mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Katibu
tawala wa mkoa wa LindiNdg.Abdlla Chikot akijadiliana jambo na wakuu wa
wilaya ya Kilwa kushoto mhe.Abdallah H. Ulega,kulia ni Mkuu wa wilaya
ya Liwale mhe. Ephrem Mmbaga,nje ya ukumbi wa mafunzo wa Mt. Kagwa
Lindi.
Meneja
wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akitoa taarifa ya madhumuni ya
ofisi ya mfuko kushiriki kwenye mafunzo hayo kwa waandishi wa
habari,ambapo elimu ya faida na umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya
jamii.(CHF) itatolewa hapo kesho kwa washiriki vijana..
…………………………………………………………………………………
Na .Mwandishi wetu-LINDI
NAIBU Waziri
wa kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, amesema kuwa hali ya ukosefu wa
ajira nchini mpaka hivi sasa kwa mujibu wa utafiti wa nguvu kazi
uliofanyika mwaka 2006, jumla ya watu waliokuwa hawana kazi hapa nchini
ni asilimia 11.7.
Hayo
yamebainisha leo na Naibu huyo, kwenye ufunguzi wa semina ya vijana mkoa
wa Lindi, na kusema kuwa utafiti huo ulionyesha kuwa takribani asilimia
13.4 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 34 wa Tanzania hawana
kazi kabisa.
Alisema
ukosefu huo wa ajira kwa vijana ni kubwa zaidi asilimia 26.7
ukilinganisha na vijijini asilimia 7.9 ,imechangiwa kwa kiasi kikubwa
kwa kutofikiwa kikamilifu kwa malengo ya nchi ya kuinua uchumi katika
sekta za kilimo, uzalishaji na viwanda.
“Wimbi la
vijana ambalo ni nguvu kazi ukimbilia mijini na hivyo kupunguza
uzalishaji wenye tija kwenye sekta ya kilimo,hivyo kuchangia ongezeko la
ukosefu wa ajira mijini sambamba na ongezeko la wafanya biashara wa
sekta isiyo rasmi maarufu kwa jina la machinga..Kuendelea kupanuka kwa
sekta isiyo rasmi kutoka asilimia 8.8 mwaka 1990/01 hadi asilimia 11.3
mwaka 2005 na kupungua kwa nguvu kazi katika sekta ya kilimo kutoka
asilimia 83.7 hadi asilimia 74.6 ni dalili kuwa kuna uhamaji mkubwa wa
nguvu kazi kutoka vijijini kwenda mijini.
Kwa upande
wake Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza, alisema kuwa lengo la
semina hiyo ni kuwawezesha vijana hao kupata ufahamu na uelewa wa nafasi
yao katika jamii, wajibu wa kijana, haki zake na kuwajengea uwezo
ambapo watapata stadi za namna ya kutambua fursa zilizowazunguka, na
umuhimu wa kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii hususani mfuko wa
afya ya Jamii (CHF) kwani ndiyo mkombozi wa huduma za matibabu.
Mahiza
alisema, katika semina hiyo ya siku tano, vijana watapata fursa ya
kupitishwa katika mambo mbalimbali, ambapo taasisi mbalimbali zitapata
fursa ya kutoa elimu kwa vijana kuhusu,usalama wa raia na mali zao,
Katiba inayopendekezwa na kushiriki wa vijana katika kukuza uchumi.
No comments:
Post a Comment