TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 15, 2014

Wanawake wa kenya kufanya maandamano

Mwanamke aliyevuliwa nguo na makondakta katika kituo kimoja cha kuegesha magari nchini kenya kwa kudaiwa kuvaa nusu uchi.
Kundi la akina mama wa kilimani waliopo katika mtandao wa facebook nchini Kenya limeapa kufanya maandamano katika bustani ya Uhuru Park tarehe 17 mwezi huu ili kuungana na mwanamke aliyevuliwa nguo hadharani siku ya jumatano kwa kuvaa nusu uchi mbali na kupinga unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.
Katika kisa hicho kilichofanyika katika kituo cha kuegesha magari cha Embassava jijini nairobi,wanaume wanaodaiwa kuwa makondakta wa matatu walimvua nguo mwanamke huyo na kusema kwamba alikuwa anawasisimua kwa mavazi yake.
Wanawaake hao wameapa kuelekea katika kituo hicho cha magari ya uchukuzi ili kuwaambia makondakta hao kwamba wanawake wana haki ya kuvaa wanavyotaka.
Kanda ya video ya kisa hicho ilichukuliwa na baadhi ya wasafiri na kuwekwa katika mtandao wa jambo net.
Wakenya pia wamepinga tukio hilo kupitia neno MyDressMyChoice katika mtandao wa twitter.
Wanaume wengi wamesema kuwa watajiunga na wake zao pamoja na wana wao wa kike kupinga uhalifu huo siku ya jumatatu.

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABULRAHMAN KINANA AANZA ZIARA YAKE MKOANI LINDI, APATA MAPOKEZI MAZURI SOMANGA KILWA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa Skafu na vijana na wa Chipukizi wakati alipowasili eneo la Somanga wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi akianza ziara yake ya siku 16 katika mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza sughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi, Katibu Mkuu huyo anaongozana naNape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi pamoja na Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Wilaya  ya Kilwa na Mkoa wa Lindi waliofika katika eneo la Somanga kwa ajili ya mapokezi Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Ali Mtopa. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kumpokea katika eneo la Somanga wilayani Kilwa kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndugu Abdallah Ulega wakati akielekea kushiriki ujenzi wa jengo la VICOBA  Mwamko Somanga. 6Mmoja wa wasanii Ali Said Abubakary akicheza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa VICOBA Mwamko Somanga. 8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua ukumbi wa VICOBA Mwamko Somanga. 10Mjumbe wa NEC mkoa wa Lindi na Mbunge jimbo la Mtama Mh. Bernald Membe akizungumza na wananchi katika mji wa Somanga mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 11Mkuu wa mkoa wa Lindi Magalula Sid Magalula akiwasalimia wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM akinyanyua mkono wake juu kuashiria kupokea salamu zao.

MUSEVENI URGES AFRICAN COUNTRIES TO PROMOTE TOURIST ATTRACTIONS.

Minister for Natural Resources and Tourism
Hon. Lazaro Nyalandu (left) discussing a point with Permanent
Representative of the African Union Mission to the USA, Ambassador
Amina Salum Ali during the ongoing 39th World Congress of Africa Travel Association
(ATA) in Kampala, Uganda.
Minister for Natural Resources and Tourism
Hon. Lazaro Nyalandu (second right) stands during the playing of the
Ugandan and East African anthems before the official opening of the
39th World Congress
of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda.
Part of the Tanzanian delegation attending
the 39th World
Congress of Africa Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda. They
are from left: Asantael Melita (Ngorongoro Conservation Area
Authority); Philip Chitaunga (Tanzania Tourist Board); Kelvin Nkulila
(Tanzania National Parks); Uzeel Kiangi; Lilian Nyaki and Imani Nkuwi
from the Ministry of Natural Resources and Tourism.
Tanzanian delegation standing during the
playing of the Ugandan National Anthem: From right is Dr. Ladislaus
Komba, Tanzanian Ambassador in Uganda; Hon. Grace Kiwelu (MP), Member
of the Parliamentary Committee on Lands, Natural Resources and
Environment; Hon. James Lembeli, Chairman of the Parliamentary
Committee on Lands, Natural Resources and Environment and Ibrahim
Mussa, Director of Tourism and Marketing from Tanzania National
Parks.
High
table stands during the playing of the Ugandan and EAC
anthems
  1. Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni
    delivering his Keynote speech during the 39th World Congress of Africa
    Travel Association (ATA) in Kampala, Uganda.

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro
Nyalandu (right) addressing the participants during the 39
th World Congress of Africa Travel
Association (ATA) in Kampala, Uganda.  With him is the Executive
Director of ATA Edward Bergman

Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni shaking hands with
the Tanzanian Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Lazaro
Nyalandu after the official opening of the 39
th World Congress of Africa Travel
Association (ATA) in Kampala, Uganda

Ugandan President Yoweri Kaguta Museveni in a group picture
with some of the participants of the 39
th World Congress of Africa Travel Association (ATA) in
Kampala, Uganda.

Taswira ya Ziara ya Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe Mikoani

Wananchi wa kijiji cha Igalula mkoani Kigoma, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wakati alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akisalimiana na Bi. Mariamu Ramadhani (86), baada ya kuwasili katika kijiji cha Kapalamsenga mkoani Katavi, ambako alihutubia mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Zanzibar), Salumu Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kazuramimba mkoani Kigoma, katika mkutano wa hadhara wa Oparesheni Delete CCM juzi.
Badhii ya waliokuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa serikali ya kijiji cha Kapalamsenga katika jimbo la Mpanda Vijijini, wakimkabidhi kadi za CCM Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, walipoamua kujiunga na Chadema, baada ya mkutano wa Oparesheni Delete CCM, uliofanyika kijijini Hapo juzi.

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR MAHMOUD THABIT KOMBO AZUNGUMZA NA WANAHABARI JUU YA MADHIMISHO YA SIKU YA KISUKARI DUNIANI

2
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
…………………………………………………………………………..
NA RAMADHANI ALI
Wananchi wameshauriwa kujiepusha na vihatarishi vinavyoweza kupelekea kupata ugonjwa wa kisukari na kujenga tabia ya kupima afya zao ili kujuwa matatizo yanayowakabili.
Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ametoa ushauri huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mnazimmoja katika kuadhimisha siku ya kisukari Duniani.
Alisema tatizo la ugonjwa wa kisukari na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo limekuwa kubwa na inakisiwa zaidi ya watu milioni 346 duniani wanasumbuliwa na ugonjwa huo.
Alisema ongezeko   kisukari katika nchi nyingi linasababishwa  na  watu kubadili mfumo wao wa  maisha na mabadiliko ya kijamii na kiutamaduni.
Naibu Waziri ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2011 hapa Zanzibar, unaonyesha kiwango cha ugonjwa wa kisukari ni asilimia 3.7 ambayo ni sawa na watu 50,000.
Alisema kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa  katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja pekee kunawastani wa wagonjwa wapya wa kisukari 300 kila mwaka na zaidi ya watu 180,000 wapo hatarini kupata maradhi hayo kutokana na uzito uliokithiri.
Amewakumbusha wananchi kuwa ugonjwa wa kisukari hauponi na mtu akishaupata hulazimika kutumia dawa katika uhai wake wote na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya.
“Jambo la msingi ninalosisitiza ni kwamba ugonjwa wa kisukari hauponi, mtu anapothibitika kuwa nao inamaana ataendelea kuwa nao katika maisha yake yote na atalazimika kutumia dawa ama sindano katika uhai wake wote,” alieleza Naibu Waziri.
Katika kujikinga na ugonjwa huo Naibu Waziri amewasisitiza wananchi kufanya mazoezi, kujiepusha na matumizi ya pombe na matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku pamoja na kuzingatia umuhimu wa lishe bora.
Amewashauri wananchi kuweka umuhimu wa kuchunguza afya zao kama ni njia moja wapo ya kinga kwani inakadiriwa kuna zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ambao hawajijui.
Akizungumzia kadhia ya kisukari Mkuu wa Kitengo cha ugonjwa wa kisukari Dkt. Faiza Kassim Suleiman alisema tatizo kubwa linalowapata wenye maradhi hayo ni ganzi, kupoteza nuru ya macho na kupungua nguvu za kiume.
Hata hivyo amesema bado hakujawa na mikakati imara iliyoandaliwa kukabiliana na ongezeko kubwa la ugonjwa huo licha ya kuwepo dawa katika Hospitali na vituo vya Afya.
Mwenyekiti  wa Jumuiya ya watu wanaoishi na ugonjwa wa kisukari Zanzibar Waziri Said Othman amesema dawa za ugonjwa huo zinapatikana lakini tatizo linalowakabili ni  dawa  za maradhi mengine ambayo yanaenda sambamba na kisukari ikiwemo sinikizo la damu.
Amewashauri madaktari kuongeza juhudi katika kuwashughulikia wagonjwa wa kisukari wenye vidonda kwani tiba yake huchukua muda mrefu kabla mgonjwa  kupona.

WANA CCM BEIJING WAKUTANA

Wanachama wapya wa Tawi la CCM China waliopo Beijing wakikabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa Tawi Ndugu Boniphace Shija Nobeji.
Kada na Mtumishi wa CCM Makao Makuu Ndugu Suleiman Serera akitoa semina
iliyohusu itikadi na imani ya CCM kwa wanachama wa CCM Beijing.
Sehemu ya wanachama waliohudhuria wakiuatilia kwa makini semina iliyokuwa ikitolewa.
Wanachama wa mashina ya CCM Beijing wakiwa kwenye picha ya pamoja baada
ya kumaliza Mkutano wao uliofanyika katika Chuo cha Beijing Normal.

WANAFUNZI WA KENYA WATEMBELEA MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU YA AFRIKA KUJIFUNZA

unnamedNaibu Msajili wa Mahakama ya Kiafrika ya Haki za Binadamu(AfCHR)Nouhou Dialo akizungumza na wanafunzi  wanaosoma  Sheria  katika Chuo cha  African Nazarine University , Nairobi nchini Kenya  waliofanya ziara ya kujifunza juu ya  utendaji kazi wa Mahakama hiyo yenye makao yake Jijini Arusha jana,wengine ni Mhadhiri wa Chuo hicho,Nyamweya Mamboleo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa AfCHR,Sukhdev Chatbar.1 Baadhi ya Wanafunzi  wanaosoma  Sheria  katika Chuo cha  African Nazarine University , Nairobi nchini Kenya  walimsikiliza  Naibu Msajili wa Mahakama ya Kiafrika ya Haki za Binadamu(AfCHR)Nouhou Dialo . 2Wanafunzi  wanaosoma  Sheria  katika Chuo cha  African Nazarine University , Nairobi nchini Kenya  walimsikiliza  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa  AfCHR,Sukhdev Chatbar wakati akiwatambulisha maeneo mbalimbali ya Mahakama hiyo. unnamed3Mmoja wa wanafunzi akifurahia kitabu kwenye Maktaba ya Mahakama hiyo lana unnamed5 Wanafunzi  wanaosoma  Sheria  katika Chuo cha  African Nazarine University , Nairobi nchini Kenya  wakiangalia baadhi ya Kesi zilizowahi kufunguliwa  katika Mahakama hiyo.
 

Rais Kikwete atoka Hospitalini Baada ya KUPATA NAFUU

 unnamed.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  akisindikizwa na Daktari Bingwa
Edward Schaeffer kutoka
Hospitali ya Johns Hopkins alipokuwa amelazwa baada ya kufanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya
kupata nafuu.Kulia nia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Hali ya Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapumzikoni akiuguza kidonda kilichotokana na upasuaji aliofanyiwa, kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza.
1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Daktari Edward Schaeffer
muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya Johns
Hopkins huko Baltimore, Maryland nchini Marekani ambapo alifanyiwa
upasuaji wa kuondoa tezi dume mwishoni mwa wiki iliyopita. Hali ya
Rais Kikwete imezidi kuimarika baada ya kutoka wodini na kuwa mapummzikoni akiuguza kidonda kabla ya kwenda kuondolewa nyuzi siku chache zijazo. Huku akiendelea kufanya mazoezi kila siku, Rais Kikwete pia ameendelea kupokea salamu za Watanzania kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kila pembe ya dunia pamoja na salamu za kumtakia nafuu mapema kutoka kwa viongozi mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa nchi za nje. Naye amekuwa akizijibu kwa kadri anavyoweza  (Picha naFreddy Maro)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) afanya ziara kwenye vitengo vya Mawasiliano Serikalini

1
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuangalia utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano.
2
Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi akimueleza Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mikakati ya ofisi hiyo ya kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma wakati wa ziara ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari katika vitengo cha mawasiliano.
3Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kushoto) akizungumza na Katibu, Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Exavier Daudi wakati alipotembelea ofisi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa Idara ya Habari kutembelea vitengo vya mawasiliano kwenye taasisi za serikali ili kuangalia utendaji kazi wa vitengo hivyo.
4Afisa Habari wa Ofisi ya Rais Sekretariet ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Kassim Nyaki (kulia) akieleza kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene kuhusu mafanikio ya kitengo cha mawasiliano cha ofisi hiyo katika kutoa taarifa kwa umma ambapo alisema hadi sasa tovuti yao ina zaidi ya watu Elfu 8 wanaotembelea kwa siku.
5Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati alipotembelea Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kujionea utendaji kazi wa kitengo cha mawasiliano serikalini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa ofisi hiyo Bw. Gerard Mwanilwa.
6Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (kulia mwenye Kaunda Suti) akiwaeleza baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuboresha mawasiliano ya serikali kwa umma. Katikati ni Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Francis Mwakapalila.

SEKTA BINAFSI IHUSISHWE KUTOA HUDUMA ZA AFYA – PINDA

 unnamedWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa Afya (Annual Health Summit ) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 14, 2014. (Picha na Ofisi ya Wazri Mkuu) unnamed2 Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Afya (Annual Health Summit ) wakimsikiliza Waziri Mkuu,Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba14, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………….
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ipanue wigo wa utoaji huduma za msingi kwa kuishirikisha zaidi sekta binafsi nchini.
 “Ninawasihi Waziri wa Afya na Naibu wake kwa vile ni wapya bado wabadili mtizamo wa wizara hii kwa kushirikisha zaidi wadau wa sekta binafsi kwenye utoaji wa huduma ili wasaidie kupunguza mzigo mkubwa ilionao Serikali,” alisema.
 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 14, 2014) wakati akifungua Mkutano wa wa Kwanza wa Kitaifa wa Sekta ya Afya wa mwaka 2014 ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu ambaye amefungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliyeko nje ya nchi kwa matibabu alisema: “Kuna tatizo la kukumbatia utoaji wa huduma … tunazo hospitali kubwa za wilaya zinazomilikiwa na taasisi za dini. Hivi ni kwa nini kama Wizara msiwasaidie kuwahudumia watumishi wao au kuwapa ruzuku kwenye dawa ili kuwawezesha kutoa huduma kwa ufanisi zaidi?,” alihoji Waziri Mkuu na kushangiliwa na washiriki wa mkutano huo.
 “Hata ukiangalia takwimu kwenye utoaji wa huduma za afya kupitia mifumo ya bima ya afya utabaini kuwa ni asilimia 18 tu wananchi wanatumia bima ya afya na kati ya hao, asilimia 15.3 ni mifuko ambayo imeanzishwa na Serikali. Ni kwa nini basi msiwasaidie wadau wa sekta binafsi ili wachangie huduma hii na idadi wa watumiaji wa mfumo huu iongezeke haraka?,” alihoji.
 Akizumgumzia kuhusu uwiano kati ya daktari na mgonjwa, Waziri Mkuu alisema uwiano uliopo ni mbaya na kwamba hakuna njia ya haraka ya kupunguza tatizo hilo isipokuwa kwa kuishirikisha sekta binafsi kwenye ujenzi wa vyuo vikuu vya elimu ya tiba na sayansi za jamii.
 “Uwiano wa sasa hapa nchini ni daktari mmoja kwa wagonjwa 75,000 wakati viwango vya kimataifa vinataka daktari mmoja awahudumie wagonjwa 7,000. Kwa wauguzi, hapa nchini muuguzi mmoja anahudumia wagonjwa 6,000 wakati viwango vya kimataifa vinataka muuguzi mmoja ahudumie wagonjwa 500,” alisema.
 “Kwa uwioano huu safari bado ni ndefu. Tunapaswa tuangalie tutafanyaje ili watu binafsi waje kuwekeza kwenye elimu ya juu ya sayansi na tiba, wajenge vyuo vya tiba, wajenge hospitali kubwa, na sisi pia kwa upande wa Serikali ni lazima tuseme tunawapa vivutio gani hawa wawekezaji hadi wakubali kuwekeza kwenye eneo hilo,” alisema.
 “Tunataka mkutano huo uje na mapendekezo ambayo mnataka Serikali iyafanyie kazi na hatimaye isaidie kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi,” alisema Waziri Mkuu.
 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo, Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kudhibiti ugonjwa wa ebola kwenye vituo vya mipakani na kwenye viwanja wa ndege.
 “Mpaka sasa hatujapata kesi ya ugonjwa wa ebola hapa nchini… changamoto kubwa ni ukubwa wa mipaka yetu. Si wageni wote wanaoingia nchini wanapita kwenye vituo rasmi, wapo wanaotumia njia za vichochoroni. Rai yangu ni kuwaomba Watanzania wawe waangalifu kutambua ni wageni gani wanaingia kwenye maeneo wanayoishi,” alisema.
Mkutano huo wa siku mbili unamalizika kesho (Jumamosi, Novemba 15, 2014).
Waziri Mkuu amerejea mjini Dodoma kuendelea na kikao cha Bunge.

KUBUNI JEZI MPYA YA TIMU ZA TAIFA MWISHO LEO

index17
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekaribisha wabunifu, kubuni mwonekano wa jezi mpya za timu ya Taifa kwa mechi za nyumbani na ugenini ambapo mwisho wa kufanya hivyo ni leo (Novemba 15 mwaka huu). Ubunifu ni lazima uzingatie rangi za bendera ya Taifa.  
Mshindi wa jezi ya nyumbani atapata sh. 1,000,000 (milioni moja), na mshindi wa jezi ya ugenini atapata pia sh. 1,000,000 (milioni moja).
Ubunifu utumwe kwenye anwani ya barua pepe: info@tff.or.tz au uwasilishwe kwa CD au flash zikiwa katika mfumo wa PDF katika ofisi za TFF zilizopo ghorofa ya tatu katika Jengo la PPF Tower, Mtaa wa Ohio na Garden Avenue.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba; 0713 210242 au 0714 634838.

MISS TANZANIA 2013 AAHIDI MAKUBWA MASHINDANO YA UREMBO YA DUNIA

unnamed2Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kuhusu safari ya Miss Tanzania 2013 nchini Uingereza kwenda kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Urembo wa Dunia yatakayoanza mapema tarehe 14 Desemba, 2014.
…………………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
 
MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2013, Happiness Watimanywa ameahidi kuing’arisha Tanzania katika mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko nchini Uingereza.
 
Akiongea na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo amewaeleza waadishi kuwa, kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali anayoipata toka  Bodi ya Utalii Tanzania pamoja na wahisani wengine nchini amewaahidi Watanzania kuibuka na ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko nchini Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
 
Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya ulimbwende yatakayowahusisha walimbwende toka Ulimwengu  mzima.
 
“Nimejifunza mambo mengi hasa kipindi wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi watanzania ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
 
Naye Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania, alisema kuwa mashindano ya Urembo wa Dunia ni mashindano ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.
 
Mashindano ya Urembo ya Dunia yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

indexTarehe 17 Novemba, 2014 saa 4:00 asubuhi Jeshi la Magereza litapokea msaada wa vifaa vya ujenzi na vitendea kazi vitakavyotumika katika ujenzi wa makazi ya Maafisa na Askari wa Gereza Wazo. Tukio ambalo litafanyika katika Viwanja vya Gereza Wazo, Wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana na Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini msaada huo umetolewa na Kampuni ya Twiga Cement ya Jijini Dar es Salaam kufuatia kusainiwa kwa Makubaliano ya kuiuzia Kampuni hiyo madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo.
Mgeni rasmi katika tukio hilo atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias M. Chikawe(Mb). Aidha, Wadau mbalimbali toka nje ya Jeshi la Magereza watakuwepo katika hafla hiyo.
Kuanza kwa mradi wa ujenzi wa nyumba hizo utapunguza tatizo la muda mrefu la uhaba wa Nyumba zenye hadhi kwa ajili ya makazi ya Maafisa na askari wa Gereza hilo.
Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye shughuli hiyo katika muda ulioelezwa.
Imetolewa na; Lucas A. Mboje, Mkaguzi wa Magereza; Afisa Habari wa Jeshi la Magereza; Makao Makuu ya Jeshi la Magereza; DAR ES SALAAM. 14 Novemba, 2014.

KINANA KUANZA ZIARA YA MIKOA YA MTWARA NA LINDI

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti,CCM Ofisi ndogo Lumumba.
……………………………………………………………………………..
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana anatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti,Lumumba jijini Dar es salaam Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye alisema kuwa Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za Sekretarieti ya Halmashauri Kuu Taifa katika mikoa mbali mbali nchini kwa ajili ya kujenga na kuhimiza uhai wa chama na kukagua utekelezazaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015.
Ziara hiyo itakuwa ya siku 16 na itaanza Novemba 15,2015 ,Katibu Mkuu ataambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye.
Ziara hiyo ya Katibu Mkuu itamwezesha kutembelea  na kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara  katika majimbo yote ya mikoa ya Lindi na Mtwara  ikiwa pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015, kukutana na wananchi, kuwasikiliza na kwa kushirikiana nao kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili.

SERIKALI YA TANZANIA NA MAREKANI ZATILIANA SAINI MKATABA YA KUANDAA MIRADI YA SEKTA YA NISHATI

images
Na:Beatrice Lyimo- Maelezo-DSM.
 
Serikali ya Marekani na Tanzania zimetiliana saini kwa ajili ya kuandaa miradi katika sekta ya nishati itakayofadhiliwa katika awamu ya pili ya Mkataba wa Millennium Challenge Corporation (MCC).
Utiaji saini wa mkataba huo ulifanyika katika Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais wa MCC Bw. Kamran Khan  anayeshughulikia Mikataba na Uendeshaji wake pamoja na Waziri wa Fedha  wa Tanzania , Mhe. Saada Mkuya ukishuhudiwa na Balozi wa Marekani nchini Mark Childress.
Akiongea wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya alisema kuwa MCC imeipatia Serikali ya Tanzania shilingi bilioni 17 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa MCC II ambapo mraadi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa hapo mwakani ukiwa na lengo la kusaidia miundombinu ya umeme nchini.
Makubaliano hayo ni muendelezo wa ubia imara kati ya Marekani na Tanzania kati ya mwaka 2008 na 2013 ambapo MCC ilitekeleza mkataba wa miradi mikubwa ya uwekezaji katika sekta za maji, barabara, na nishati ya umeme nchini.
Miradi hiyo iligharimu jumla ya Dola za kimarekani milioni 698, chini ya mkataba huo mtandao wa nyaya za umeme wenye zaidi ya kilometa 3,000 ulijengwa.
Kwa kuzingatia mafanikio hayo katika utekelezaji wa wa programu zilizokuwa chini ya mkataba wa kwanza kuwahi kutolewa na MCC, taasisi hiyo iliichagua tena Tanzania kuingia katika mkataba wa pili utakaolenga sekta ya Nishati katika miundombinu pamoja na mageuzi ya kisera na mifumo ya udhibiti na kitaasisi.
Aidha, upembuzi yakinifu utaiwezesha Tanzania kuandaa miradi itakayoleta mageuzi katika sekta ya Nishati ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji wa shirika la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) katika maeneo ya kiufundi, usimamizi wa fedha na uendeshaji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya umeme katika maeneo ya vijijini.
Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) ni Taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea, shughuli zake zinajengwa katika misingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa pale unapoimarisha utawala bora, uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao unakuza uchumi na kuondoa umaskini.

HABARI ZILIZOTAWALA SIKU YA TAREHE 14/11/2014 HIZI HAPA JIKUMBUSHE

BONDIA THOMAS MASHALI ASAINI KUZIPIGA NA ABDALLAH PAZI JANUAR MOSI 2015 FRENDS CORNER

Bondia Thomasi Mashali kushoto akitia saini ya kupigana na Abbdallah Pazi kulia baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam
Bondia Abbdallah Pazi kulia akitia saini ya kupigana na Thomasi Mashali kushoto baada ya makubaliano na promota Kassim Texas katikati mpambano utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam
Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa
Promota Kassim Texas katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Thomas Mashali kushoto na Abdallah Pazi kuashilia makubaliano ya mpambano wao utakaofanyika january mosi katika ukumbi wa frends corner manzese 
Bondia Thomasi Mashali kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya makubaliano juzi  ya mpambano wao kufanyika January Mosi 2015 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaa Picha na SUPER D BLOG
===============================================================

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AFUNGUA KONGAMANO LA NHIF NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA

1Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dr. Seif Rashid akifungua Kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na wahariri pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali linalofanyika kwenye hoteli ya New Dodoma  mkoani Dodoma jana, Kongamano hilo la siku mbili linaendelea leo na linajadili mafanikio mbalimbali na changamoto zinazokabili mfuko huo katika mikoa mbalimbali na Halmashauri ambazo unatoa huduma zake. Kongamano hilo linamalizika leo 2Naibu Katibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dr. Deo Mtasiwa  akizungumza katika kongamano hilo wakati akimkaribisha waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid ili kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo. 3Kamimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Khamis Mdee  akitoa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali kwa mwaka mzima. 4Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto, Kaimu Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Athman Rehani wakiwa katika mkutano huo. 5Hance John Mwankenja Afisa Mwandamizi , Matekelezo NHIF pamoja na maafisa wengine wa mfuko huo wakiwa katika kongamano hilo. 006Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mh. Elibariki Kingu akitoa mada katika kongamano hilo. 6Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF Bw. Athman Rehani akitoa mada katika Kongamano hilo. 7Mkuu wa Wilaya ya Igunga na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Fatma Said Ally wakiwa katika kongamano hilo. 9Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika kongamano hilo. 10Grace Kingalame wa TBC wa pili na wadau wengine wakiwa katika kongamano hilo. 11Hosea Cheyo wa TBC Mbeya kushoto na Tom Chilala wa Star TV wakifuatilia mada. 12Wanahabari mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo. 13 14 15 Baadhi ya maofisa wa NHIF wakiandika mambo muhimu katika kongamano hilo.
=====================================================================

SKYLIGHT BAND NI MOTO WA KUOTEA MBALI, WAZIDI KUWAPA RAHA MASHABIKI WAO KWA BURUDANI NZURI

Pichani Kutoka kushoto ni Bella Kombo akiongoza mashambulizi ya jukwaa akipewa sapoti na Digna Mbepera(katikati) na kwa mbaliiiii ni Aneth kushaba.
Kama kawaida yetu inapofika mwishoni mwa juma yaani Ijumaa huwa inakuwa ni siku ya furaha na kubadilishana mawazo, kupunguza stress za kazini…..paleee Thai Village Masaki.Kwenye Jukwaa Bendi yako matata na inayotikisa Tanzania na Jiji la Dar Skylight Band wanakuwa wanakupa burudani ya nguvu na iliyoenda shule.Karibu leo kuanzia saa 3 kamili usiku upate zile Afropop, Zouk, Lingala,Sebene, Reggae, Naija Flava na zingine kibao!
Aneth Kushaba AK 47 akizipiga vocal za kutoshaaaa ili kuwapa burudani wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita.
Bella Kombo akitia madaha yake na swagga kibao ndani ya Thai Village.
Digna Mbepera (Mtoto Mzuri) akiimba kwa hisia kali kuwapa ladha wapenzi wa Skylight band ndani ya Thai Village
Anaitwa Hashimu Donode mkali wao akizipiga zile vocal kaliiii na tamuuu kuwapa raha mashabiki wake ndani ya Thai Village

UNESCO, SAMSUNG KUJENGA KIJIJI CHA DIGITALI OLOLOSOKWAN

DSC_0062Mwakilishi mkazi shirika la UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo wakibadilishana nyaraka za makubaliano hayo yaliyofanyika ofisi za UNESCO.
Na Mwandishi wetu
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limetiliana saini mkataba na kampuni ya elektroniki ya Samsung ya ujenzi wa kijiji cha digitali cha Ololosokwan, Loliondo.
Makubaliano hayo yalitiwa saini hivi karibuni kati ya Mwakilishi mkazi Unesco nchini Bi. Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania, Bw. Mike Seo katika hafla iliyofanyika ofisi za UNESCO.
Kijiji hicho kitakuwa na shule yenye Tehama ikiwa na maunganisho ya intaneti, kiliniki ya kisasa ikiwa na kituo cha teknolojia ya mawasiliano yenye kuwezesha utabibu (telemedicine) na jenereta linalotumia nguvu za jua kwa ajili ya kijiji hicho.
Utiaji saini huo ulioshuhudiwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO, bi. Leah Kihimbi kutoka wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo na Dkt. N. Iriya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dar es Salaam na wafanyakazi wa UNESCO.
Katika hafla hiyo Bi. Rodrigues amesema kwamba mradi huo utawezesha UNESCO kuwapatia vijana wa Kimasai elimu kutokana na ukweli kuwa kwa utamaduni na kazi zao za ufugaji wamekuwa wakipata shida ya kupata elimu.
DSC_0002Baadhi ya wafanyakazi wa UNESCO na Samsung wakifuatilia kwa umakini hafla hiyo fupi ya kutiliana saini makubaliano baina ya Samsung Tanzania na UNESCO.
“Kupitia kijiji hiki vijana wataendelea na masomo hata kama wanachunga mifugo yao”, alisema Bi. Rodrigues.
Naye Mkurugenzi wa Samsung Electronics nchini Tanzania miongoni mwa manufaa makubwa yatakayopatikana katika mradi huo wa kijiji cha digitali huko Loliondo ni kuweza kupata nishati rahisi na iliyo rafiki kwa mazingira.
Alisema kwamba Afrika imekuwa mstari wa mbele katika uanzishaji wa vijiji vya digitali. Aidha kwa kitendo hicho Afrika inaonesha dunia ni kwa namna teknolojia inaweza kutumika kuleta mabadikliko chanya yanayotakiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi waliopo vijijini.
Bi Leah Kihimbi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya habari,vijana, utamaduni na michezo, alisema kupitia vijiji vya digitali itawezekana kutekeleza program ya elimu kwa watu wanaoishi Loliondo huku tamaduni zao zikihifadhiwa.
Kijiji hicho cha Loliondo kitakuwa cha nne katika vijiji vya kidigitali barani Afrika. Inatarajiwa kwamba kijiji kingine kitajengwa mjini Zanzibar kwa ushirikiano wa UNESCO na Samsung Electronics mwaka 2015.
Untitled 1 
Pichani ni muonekano wa mchoro wa kijiji hicho utakavyokua.

Nyalandu amteua RC Singida Mwenyekiti wa Kikos kzi alichouunda jana.

images 
Waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amemteua Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Paseko Kone kuwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi kitachofuatilia uundwaji wa chama cha wafuga nyuki hapa nchini.
Nyalandu alimteua Mkuu wa Mkoa huo kwa kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wafugaji wa nyuki katika mkoa wake wa Singida bila kuchoka.
Waziri Nyalandu alitoa uamuzi huo wakati akifuga kongamano la ufugaji nyuki la Afrika lililomalizika Jijini Arusha jana.
Wajumbe Wengine walioteuliwa katika kikosi kazi hicho ni Juma Shaban Mgoo ambaye atakuwa katibu wa Kikosi kazi hicho na pia ni  Mtendaji Mkuu,wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na ambaye alikuwa mkamu mwenyekiti wa Kongamano atakuwa mjumbe katika Kikosi kazi hicho,wengine ni Ester Mkwizu Mjumbe.
Wajumbe wengine ni mwakilishi wa wafugaji nyuki ,mwakilishi wa wasomi na watafiti ili kikosi kazi kiwe na mchanganyiko wa pande zote.
Walioteuliwa wote watapaa barua jumatatu kwa ajili ya kuthibitisha uteuzi wao,ambapo waziri nyalandu alieleza kuwa kuwa uteuzi huo wa wajumbe wanaounda kikosi kazi cha kushughulikia uundwaji wa chama cha wafuga nyuki ni agizo lililotolewa na Waziri Mkuu wakati wa ufuguzi wa Kongamano la nyuki kuwa ipo haja ya kuundwa kwa chama cha wafugaji nyuki ili kiweze kuwaunganisha wafugaji wote ndani ya nchi na kuwa na mtandao mmoja wenye nguvu na sauti.
Katika hotuba yake alieleza jinsi Tanzania ilivyojithatitia kuhakikisha inainua ufugaji nyuki na sekta ya nyuki ili kuwapita nchi ya Ethiopia ambayo ndiyo kinara cha nyuki cha Ufugaji nyuki Afrika.
Akasema kongamano hili ni la kwanza kufanyika katika ardhi ya Tanzania  na limesaidia sana katikakuwafumbua macho watanzania hasa wafugaji nyuki hasa katika masuala muhimu yaliyosisitizwa katika mada zilizojadiliwa kwenye kongamano hilo yatasaidia kukuza sekta ya ufungaji nyuki hapa nchini.
Kongamano hilo lililojumuisha washiriki wapatao 550 kutoka katika mataifa ya Ghana,Ethiopia,Zimbabwe, Afrika kusini,Camerun,Sudani,Kenya,Uganda na Rwanda.
Washiriki wengine walitoka katika nchi ya Kanada,Marekani,Pakstan,Namibia,Misri, Zambia,Ubelgiji,Uturuki na mengine.limekuwa la kufana sana,mada 88 zilikuwepo,mada 45 zilijadiliwa,katiyake mada 26 zilihusu tafiti za nyuki,mada 17 zilijadiliwa kwa wafugaji nyuki.
Awali akimkaribisha waziri Nyalandu Mwenyekiti wa Kongamano hilo SelestinKisimba alieleza kuwa katika kongamano hilo wameondoka na mapendekezo sita mambyo wataenda kuyafanyia kazi mara moja ili kuinua sekta ya nyuki.
Baadhi ya Mapendekzo hayo ni kuwa ufugaji nyuki lazima uweb endevu kwa manufa ya wafugaji wote,,umuhimu wa ufugaji nyuki na maendeleo,tatizo la ukosefu wa mitaji,uendelezaji wa rasilimali zilizopo , kuongeza uzalishaji wa thamani ya asali,ambapo mapendekezo hayo yatasaidia kuboresha ufugaji nyuki.
Washiriki wamepata nafasi ya kutembelea maeneo ya ufugaji nyuki katika mikoa ya Singida,Dodoma na Ngorogoro Mkoani Arusha kuweza kujifunza na kuona hali halisi ya mazingira yalivyo hasa katika maeneo yanayofugwa nyuki.