TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 3, 2015

WAGONJWA WANYANYASWA KINGONO UK

Wagonjwa wadaiwa kunyanyaswa kingono katika hospitali za Uingereza.
Mlipuko wa kisiri wa unyanyasaji wa kingono katika hospitali za Uingereza umegunduliwa huku takwimu mpya zikionyesha zaidi ya mashambulizi 1600 yaliripotiwa kwa polisi katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.
Kumbukumbu zilizopatikana na gazeti la The Guardian chini ya sheria ya uhuru wa habari zinaonyesha ongezeko la asilimia 50 ya ripoti za unyanyasaji wa kingono kwa kutumia nguvu katika hospitali tangu mwaka 2011.
Unyanyasaji huo unashirikisha visa 157 vya ubakaji.Takwimu za unyanyasaji huo katika hospitali zilitolewa na vituo 38 vya polisi kati ya vituo 45 nchini Uingereza.Wagonjwa hospitaliniRipoti hiyo inadai kuwa mashambulizi 1,615 yanayojulikana yanafanyika katika kliniki za kibinafsi,na vituo vyengine vya afya.
Lakini viongozi wa mashtaka wanasema kuwa hadi asilimia 90 ya visa vya unyanyasaji haviripotiwi swala linaloonyesha kwamba takwimu za ukweli huenda ziko juu zaidi.

BAADHI YA WAKE WA MFALME MSWATI

Meet some of KING MSWATI's wives, Very Hot, the Guy must be lucky

MAGARI YAGONGANA NA KUPINDUKA MAKUTANO YA SHULE YA MSINGI OYSTERBAY DAR MCHANA WA LEO

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwwb0BCc162gnAyKBv5zDGhybHUOioq8p9489DhV6hUUY5nr37Ia7q8-qE9D7nZnOhtUCY6iRBdOwBxxQ8FOX4C9AQUoWCrB4ek48k4L-fqXlV2Ey-Nr11pny_SW2CG0hX0HWOX65ISFSA/s1600/10888652_10155040293165154_4139546440372624351_n.jpg 
Wasamalia wema wakifanya utaratibu wa kumuokoa Dereva wa Gari aina ya Isuzu Trooper iliyopiga mweleka katika makutano ya Shule ya Msingi Oysterbay,mara baada ya kugongana na gari nyingine aina ya Toyota Vitz iliyokuwa ikitokea upande wa Coco Beach jijini Dar mchana wa leo na kupekea dereva wa Gari hii (alikuwa ni Mama mtu mzima ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) kuumia sehemu ya kiuno na mkono.
Gari hii ilikuwa inatokea upande wa St. Peter's kuelekea Morogoro Store na Vitz ilikuwa ikitokea upande wa bahari na kuvuka ghafla barabara hiyo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiWTKWhOPeq6WxonQhYpaMvw795DZ8ziBYGuggv_zCYiNU4pcdq3xVzaGBExv8321wEG4gTUkN-MkCI9OnCmtVNsGQ6mFTxok6ReK1g32-RHfwuaZqd2Ty6AKwS0Ji3FvnuaFPQFa2k_3pv/s1600/1505602_10155040292785154_2703405919875079041_n.jpg 
Mashuhuda wakiwa wameizunguka gari hiyo mara baada ya kufanikiwa kumtoa Mama aliekuwa akiendesha Gari hilo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5DBXh_2ffgVNPIejrxS_652cOkArggc5XpI1u49mJ-MiAxeJndDYMoiKhIMRyHcTaX4lwI33i-_4vRLqnUb2wXAOUSr3-wPKzAxKERfH10UzCdbKNtP-2lUjjAMeYUMXHMQdYQMXZPzjF/s1600/10906411_10155040293730154_642835539450069019_n.jpghttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgnTKn5UUMqhoMA6f6aXVkI1d46d5z1sHdlCw1nR8f2TRpjIqUKToWZx7GuR2y3HWhMwIkxWs14xl152p4O5d83Vgmcp86Fn-jRkXYrQB-yXFqFwAAQ7eAcZx3mH4RIJZe9D5iQ45Mcz2G7/s1600/10906451_10155040292990154_5109094717712458656_n.jpg
Huyu ndio Mama aliekuwa akiendesha Gari iliyopinduka

Msama ajing’atua kwa Rose Muhando

index
NA MWANDISHI WETU
 
HATIMAYE Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ameibuka na kutamka yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine.
Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokana
na nafasi yake katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15.
Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose.
“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika na kushindwa kutokea.
“Lakini, naomba watumishi wa Mungu wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama wafanyavyo wengine.
“Nimekuwa nikimlipa kiasi cha fedha anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja wake,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza:
“Agosti mwaka huu, kampuni yangu ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu, haikuwa na maana kwamba ni Meneja wake.
“Nilimualika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa fedha, lakini hakutokea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wengine ambao wamekuwa wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.
“Pia wiki iliyopita nilikuwa na Tamasha la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo, lakini hakutokea na tulishamlipa,” alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza kuwa amemsamehe na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.
Alieleza kuwa hana tatizo na mwimbaji huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa akipata taabu kutoka kwa baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu hatokei na inaonekana yeye ndiye amemzuia.
“Sijawahi kupokea mialiko kwa niaba ya Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema wadau wakafahamu hilo,” alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika, angeshafanya hivyo muda mrefu dhidi ya Rose.
Aidha, Msama amekana kuhusiana na madai ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa hajawahi kumuona akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.
“Baadhi ya vyombo vya habari vinaandika ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake binafsi na hakuna mtu mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima na mwenye kujielewa,” alisema Msama.
Rose ni mwimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini aliyejipatia sifa ndani na nje ya ukanda wa Afrika Mashariki ambaye mwishoni mwa mwaka 2013, alisaini mkataba
wa kufanya kazi na kampuni ya muziki ya Sony ya Afrika Kusini.
Miongoni mwa albamu zilizompa umaarufu Rose kiasi cha kuwa alama ya mafanikio ya muziki wa injili nchini, ni ‘Uwe Macho,’ Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, ‘Mungu Anacheka’ na Wololo na Kamata Pindo la Yesu aliyoachia hivyo karibuni.

BENKI YA ZANZIBA WAKABIDHI MABASI YA ABIRIA.

unnamedMkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour Mohamed akikata utepe kama ishara ya kukabidhi mabasi matatu kwa Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Bi Zaina Ibrahim Mwalukuta (kushoto)  yaliyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya kuchukulia abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume yenye thamnai ya shilingi za Kitanzania Mia Tatu na Ishirini Millioni,(kulia) Mkurugenzi Masoko wa PBZ Seif Suleiman,[Na Mpiga Picha Maalum) unnamed1 Miongoni mwa Mabasi yaliyotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) likiwa tayari limeanza  kazi ya kubeba abiria wanaokwenda kupanda ndege katika Kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume Kama ilnavyoonekana Pichani,[Na Mpiga Picha Maalum.]

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

index
Napenda nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi wa taharuki iliyotokea jana tarehe 02 Januari, 2015 katika jiji la Dar es Salaam ikiwahusisha baadhi ya vijana wanaojikusanya kwenye vikundi na kujiita Panya road na pengine kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.
Chanzo cha taharuki hiyo, kulitokana na kuuawa kwa kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Mohamed Ayub na wananchi tarehe 01/01/2015 katika maeneo ya Tandale kwa Mtogole kwa tuhuma za wizi wakati wa mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya. Tarehe 02/01/2015 majira ya saa tisa mchana yalifanyika mazishi ya kijana huyo katika makaburi ya Kihatu Kagera Mikoroshini na taarifa zilizokuwa zimelifikia Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam ni kwamba baada ya mazishi hayo vijana wenzake na marehemu walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi cha mwenzao kuuawa. Aidha, kabla vurugu hizo hazijafanyika na kwa vile Polisi walishaona dalili ya vurugu hizo, tayari walifanikiwa kuzidhibiti.
Baada ya vurugu hizo kudhibitiwa na Polisi, vijana hao walitawanyika kwa kukimbia katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuzua taharuki kubwa kwa wananchi kwamba huenda kila walipokimbilia wanampango wa kuwafanyia fujo raia wema, jambo ambalo wasingeweza kulifanya kwa vile Polisi walikuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jiji.
Kufuatia hali hiyo na Jeshi la Polisi nchini likiwa linaendelea na msako mkali wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaojihusisha na uhalifu huo, tunawaomba wananchi watulie, wasiwe na hofu na waendelee na majukumu yao kama kawaida. Mpaka sasa tunawashikilia watuhumiwa 36 kwa mahojiano na uchunguzi utakapokamilika tutawafikisha mahakamani mara moja.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa vijana hao wananojihusisha na vikundi hivyo kuacha tabia hiyo mara moja. Tumejipanga vizuri katika mikoa yote kuhakikisha kwamba nchi inaongozwa kwa kufuata utawala wa sheria, hatutamwonea muhali mtu yeyote ama kikundi cha watu wanaotaka kuvuruga amani ya nchi na kutia hofu wananchi.
Wananchi waendelee kutupa ushirikiano kwa kutoa taarifa kupitia namba ya simu 0754 78 55 57, namba za makamanda au katika kituo chochote cha Polisi.
Imetolewa na:- Advera John Bulimba – SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Usiku wa Old is Gold taarab kila Jumapili ndani ya Safari Carnival

index
Na Andrew Chale

USIKU wa Old is Gold taarab  unatarajiwa kurindima ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikochezni B, kwa wadau kupata burudani ya muziki wa mwambao wa kizamani.
Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin  alieleza kuwa  ni kila Jumapili  ndani ya ukumbi huo utakuwa na burudani ya kipekee kwa nyimbo za mwambao pamoja na ‘surprise’ mbalimbali kwa watakaofika hapo.
“Kila jumapili  kwa kiingilio cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa mwambao  watashuhudia shoo ya Usiku wa Old is Gold ndani ya Safari Carnival” Alisema Asia Idarous
Aliongeza kuwa, mbali na burudani ya taarab za zamani  pia kutakuwa na ‘Surprise’ mbalimbali” kwa wadau watakaojitokeza kwenye usiku huo.
Aidha,  Asia Idarous alisema usiku huo, pia umedhaminiwa na  Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds
fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo.

DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOFUNIKA MWAKA MPYA NCHINI RWANDA

img_530781a3cStaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa amebebwa na wacheza shoo wake siku ya mwaka mpya  kwenye uwanja wa Amahoro Kigali, Rwanda na kukonga nyoyo za mashabiki wake waliokuwa wamefurika kwenye uwanja huo ili kumshuhudia mwanamuziki huyo maarufu Afrika na Dunia kwa sasa hebu angalia matukio ya picha wakati wa onyesho holo kubwa na la kukaribisha mwaka 2015
10906340_862102993811516_489874224053741055_n
10888634_862055837149565_7184403002292823290_n

Diamond Platnumz visits the Kigali Memorial Centre at Gisozi

The Tanzanian singer Diamond Platnumz has who is in Rwanda for two forthcoming concerts, visited the Kigali Genocide Memorail centre to have a glimpse of what happened in  1994 when the genocide against the Tutsi was committed.
Diamond and Zari  seeing one of the historical archaives displayed in the Kigali Genocide Memorial centre 
He visited different rooms where historical archives are displayed for visitors and he deposed flowers to the tombs where thousands bodies of innocent Tutsis are resting in peace.
The singer  Diamond has expressed his swallow feelings about what he saw and his lover Zari Hassan has cried so much due to what she saw at the Kigali Genocide Memorial centre.
During a press conference that took place after the visit, Diamond urged Rwandan artists to work hard and reach beyond Rwandan borders as to become more popular and earn more money.
During  the Press conference  
During the Press conference
He urged local artists to be more professional and reach high 
He urged local artists to be more professional and reach high
As they arrived at Kigali Genocide memorial centre  
As they arrived at Kigali Genocide memorial centre
Listening to the explanations of the tour guide  
Listening to the explanations of the tour guide
Heading to another room 
Heading to another room
As they saw images displaying the horror  committed during the 1994 genocide the couple become horrified  
As they saw images displaying  how the 1994 genocide was committed,  the couple become horrified
The wife fell into tears  
The wife fell into tears
He wrote into the books for visitors  
He wrote into the books for visitors
After visiting the centre, the couple went back in the Hotel where they are accommodated
After visiting the centre, the couple went back in the Hotel where they are accommodated

RAIS DR. SHEIN AFANYA UZINDUZI MAEGESHO NA NJIA YA KUPITIA NDEGE(APRON AND TAXIWAY)

 unnamedRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakikata utepe kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar(kushoto0 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji,[Picha na Ikulu.] unnamed1Wananchi na Viongozi mbali mbali walioalikwa katika sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] unnamed2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wakati alipowasili katika uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo  katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
unnamed3Msoma Risala Farida Rajab Yussuf akisoma risala hiyo mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo  katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] unnamed4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Kaimu Meneja wa Benki ya Dunia Tanzania Monthe Biyoudi wakifungua pazia kwa pamoja  kuzindua maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] unnamed5Wasanii wa Ngoma ya Kibati wakitoa burudani yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) uzinduzi uliofanyika leo  katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alikuwa mgeni rasmi wa shuhuli hiyo ,[Picha na Ikulu] 
 unnamed6 
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akitoa nasaha fupi na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake wakati wa uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) leo  katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] unnamed7Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa  Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa maegesho na njia ya kupitia Ndege (APRON AND TAXIWAY) uzinduzi uliofanyika leo  katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar huko Kiembesamaki nje ya Mji wa Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu]
unnamed8Ndege zmbali mbali zikiwa katika Paki ikionesha  sura halisi ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa cha Abeid Amani Karume -Zanzibar ilivyo ambapo  Ndege za mashirika mbali mbali ya ndege zinaouwezo wa kutua hapa nchini na kuweza kukuza pato la Taifa letu .[Picha na Ikulu.]

SHULE YA MSINGI KIBINDU HATARINI KUFUNGIWA ,MBUNGE,DIWANI WAHAHA KUMSAKA MKURUGENZI

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni.
……………………………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
SHULE ya msingi Kibindu,Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani,ipo hatarini kufungiwa kutokana na vyumba vya madarasa kuanguka na miundombinu yake kuwa chakavu hivyo kuhofiwa kuhatarisha maisha ya wanafunzi na walimu.
Aidha shule hiyo imekuwa ikiezuliwa baadhi ya majengo yake mara kwa mara kutokana na kutofanyiwa ukarabati tangu shule hiyo ijengwe zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Kutokana na hali hiyo wanafunzi wa shule hiyo wanakabiliwa na ukosefu wa vyumba vya madarasa vilivyo bora na imara hali inayosababisha wanafunzi 200 kulundikana katika chumba kimoja.
Akizungumzia hali hiyo mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ambae yupo katika ziara ya siku 10 jimboni humo akitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo shule hiyo ambayo baadhi ya majengo yake yameanguka ,alisema hayuko tayar kushuhudia wanafunzi wakiendelea kusoma katika mazingira ya hatari.

Ridhiwani alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya kukagua madarasa hayo na kushuhudia vyumba vinne vinavyotumika kuwa hatarini kubomoka kutokana na kutawaliwa na nyufa.
“Nimesikitishwa sana na ningekuwa  na uwezo ningeifunga hii shule isitumike kwani shule inafunguliwa tarehe 14 mwezi huu ,wanafunzi watakuja kusomea wapi ,wakati pia majengo yaliyobakia yanaweza kuanguka wakati wowowte pia,ni lazima juhudi za lazima zifanyike kuokoa maisha ya wanafunzi hawa” alisema Mbunge huyo.
Ridhiwani alisema kuwa atawsiliana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Ibrahim Matovu ili waone ni namna gani wataweza kuelekeza nguvu zao katika shule hiyo ili iwe katika mazingira bora .
Diwani wa kata ya Kibindu Mawazo Mkufya alisema taarifa za uchakavu wa miundombinu ya shule hiyo tayari amezifikisha ngazi ya halmashauri, ambapo nae kwa upande wake aliomba shule hiyo ifungiwe ili ukarabati ufanyike
Mtendaji wa kijiji Cha Kibindu Juma Mgaza, alisema shule hiyo ina matatizo ya kuezuliwa mara kwa mara wakati wa mvua kutokana na miundombinu yake kuwa chakavu.
Mgaza aliitaka  halmashauri ya wilaya hiyo kufanyia kazi changamoto hiyo kubwa ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi.
Shule ya msingi Kibindu kwa sasa ina wanafunzi 907 wa darasa la kwanza hadi la saba ambao wanatarajia kuanza mhula wa masomo kwa mwaka 2015 wiki ijayo huku ikiwa na vyumba vinne kati ya 14 vinavyohitajika.
Mbali ya hayo vyumba vya madarasa vimeanguka na vingine vimeweka nyufa kubwa ambazo zinahofiwa kuanguka wakati wowowte na kusababisha athari kwa wanafunzi na walimu.

RIDHIWANI KWETE AANZA ZIARA YA KIKAZI KATIKA VIJIJI 40 CHALINZE

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo.Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali ya Vijijini kutoka CCM.
Watioto wakiruka mtaro kumuwahi Ridhiwani Kikwete alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Watoto wakigawiwa ndizi na Ridhiwani.
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja ambapo aliwaahidi kutatua tatizo la mawasiliano ya simu kwa kuwapelekea mnara
Sehemu ya umati wa wananchi uliohudhuria mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Msanja
Ridhiwani akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwa Mduma, Kata ya Kibindu, ambapo aliwahidi  kuboresha barabara na mawasiliano ya simu
Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika Kijiji cha Kwa Mduma wakati wa ziara yake katika jimbo lake la Chalinze, Kata ya Kibindu