AZAM, MTIBWA, SIMBA, YANGA KUCHEZA MAPINDUZI
Timu za Azam, Mtibwa Sugar, Simba
na Yanga zitashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayofanyika
kisiwani Zanzibar kuanzia Januari 1 hadi 13 mwakani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limetoa ruhusa kwa timu hizo kucheza mashindano hayo
baada ya kuhakikishiwa na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kuwa
kesi iliyofunguliwa dhidi ya viongozi wake imeondolewa mahakamani.
Kutokana na timu hizo kushiriki
Kombe la Mapinduzi, mechi zao za raundi ya tisa na kumi ya Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) zitachezwa katikati ya wiki baada ya kumaliza mechi zao za
michuano hiyo.
Hivyo mechi za VPL ambazo
hazitachezwa wikiendi hii ni kati ya Azam na Mtibwa Sugar, Mbeya City na
Yanga, na ile kati ya Mgambo Shooting na Simba. Mechi za wikiendi ijayo
zinazopisha michuano hiyo ni kati ya Kagera Sugar na Azam, Coastal
Union na Yanga, Mbeya City na Simba, na Mtibwa Sugar na Tanzania
Prisons.
18 WAPATA BEJI ZA UAMUZI FIFA
Waamuzi 18 wa Tanzania wamepata beji za uamuzi za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa mwaka 2015.
Idadi hiyo ambayo ni rekodi kwa
Tanzania inahusisha waamuzi saba wa kike. Waamuzi wa kati wa kike
waliopata beji hizo ni pamoja na Jonesia Rukyaa Kabakama aliyechezesha
mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga. Wengine ni Florentina
Zablon Chief na Sophia Ismail Mtongori.
Waamuzi wasaidizi wa kike
waliopata beji hizo ni Dalila Jafari Mtwana, Grace Wamala, Hellen Joseph
Mduma na Kudura Omary Maurice.
Kwa waamuzi wa kati wa kiume ni
Israel Mujuni Nkongo, Martin Eliphas Sanya, Mfaume Ali Nassoro na Waziri
Sheha Waziri. Waamuzi wasaidizi ni Alli Kinduli, Ferdinand Chacha,
Frank John Komba, John Longino Kanyenye, Josephat Deu Bulali, Samuel
Hudsin Mpenzu na Soud Iddi Lila.
No comments:
Post a Comment