Waziri
wa uchukuzi Mh.Dk. Harrison Mwakyembe ameridhia hatua ya mamlaka ya
udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini ( SUMATRA ) ya kuzuia safari za
meli ya Mv.Victoria katika ziwa victoria, baada ya meli hiyo kugundulika
na hitilafu mbalimbali zinazoweza kuhatarisha maisha ya abiria.
Dk. Mwakyembe ameridhika na
hatua hiyo baada ya uongozi wa bandari ya mwanza kumtembeza sehemu
mbalimbali za meli hiyo kongwe iliyotengenezwa toka mwaka 1960, na
kujionea jinsi mitambo yake ilivyochakaa kutokana na kufanya safari zake
kati ya miji ya mwanza na bukoba kupitia bandari ya kemondo ambapo
amesema serikali haiwezi tena kurudia makosa, yaliyosababisha meli ya
Mv.Bukoba kuzama na kupinduka mei 21 mwaka 1996 na kusababisha vifo vya
watu zaidi ya 800.
Awali kaimu meneja wa kampuni
ya huduma za meli nchini ( MSC ), fabian mayenga amesema kwamba meli
hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 1200 na tani 200 mizigo, katika
ukaguzi uliofanywa na SUMATRA imebainika kuwa haiwezi kuendelea kufanya
safari zake hadi hapo itakapofanyiwa matengenezo makubwa yanayokisiwa
kugharimu zaidi ya shilingi bilioni mojahuku akisema vifaa kwa ajili ya
matengenezo hayo vitawasili nchini katika muda wa wiki 12 hadi 15 ili
meli hiyo ianze kuendelea kuhudumia wananchi.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa
mwanza kukagua mradi mkubwa wa upanuzi na ukarabati wa uwanja huo
unaofanywa na kampuni ya Beijing Construction Engineering group kwa
gharama ya shilingi bilioni 105, waziri huyo wa uchukuzi mh. Dk.
Harrison Mwakyembe amesema serikali inasikitishwa kulipa deni la
shilingi bilioni 140 ambalo limesababishwa na ufisadi wa baadhi ya
watumishi wa shirika la ndege nchini ( ATC ), huku akisema serikali
inaendelea kukaribisha mashirika mengine ya ndege ili kuweka kwenye
sekta ya usafiri wa anga.
No comments:
Post a Comment