Siku
kadhaa tu baada ya rais Kikwete kumfuta kazi Anne Tibaijuka kama waziri
wa ardhi,nyumba na makao ,kiongozi huyo amewaambia wakaazi wa bunge
lake kwamba hawakumchagua kama waziri bali kama mwakilishi wao wa bunge,
kulingana na gazeti la The citizen nchini Tanzania.
Tibaijuka
alipigwa kalamu kutokana na maadili yake kufuatia kashfa ya akaunti ya
tageta escrow ambapo alipokea sh.billioni 1.6.'' Mungu anayetoa ndiye
aliyechukua jina la mungu libarikiwe alisema tibaijuka akimaanisha kuwa
yule aliyempa kiti hicho cha uwaziri ndiye aliyekichukua.
Katika
kile alichoelezea kama harakati za kukitetea kiti chake katika uchaguzi
wa 2015,Tibaijuka aliwaonya wapinzani wake wa kisiasa kwamba yeye ndiyo
chagua bora la wapiga kura.
Kulingana na The Citizen kiongozi huyo
aliwashukuru wapiga kura wa eneo bunge lake kwa kumchagua kuwa
mbunge,wadhfa aliodai kumfungulia milango ya kupewa uwaziri.
''Lazima
muelewe kwamba ninyi mulinipigia kura mimi ili niwahudumie bungeni na
sio kama waziri,kwa hivyo yaliotokea si ndwele tugange yajayo kwa kuwa
tayari kashfa ya escrow imezikwa'',aliwaambia wakaazi wa Muleba.
Hatahivyo
bi Tibaijuka amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na viongozi wa
upinzani waliochaguliwa katika uchaguzi wa madiwani wa hivi karibuni
No comments:
Post a Comment