Mahmoud Ahmad Arusha
Serikali Mkoani Arusha Imewataka
wakazi wa Mkoa huo Kuhakikisha kuwa wanaendelea kudumisha Amani,Umoja
na Mshikamano sanjari na kujitolea katika kufanikisha shughuli za
kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na katibu Tawala wa mkoa huu Addo Mapunda wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake ambapo alisisitiza
wakazi wa mkoa huu kufuata sheria kanuni na taratibu za nchi ikwemo usafi wa mazingira.
Aliwatahadharisha wananchi hao
kutofuata mkumbo na kujihusisha na ushabiki wa baadhi ya vyama vya siasa
ambavyo vimekuwa vikiendesha siasa za chuki,udini na uhasama jambo
ambalo limekuwa likiwagawa wananchi katika makundi na kupelekea uwepo wa
vitendo vya uvunjifu wa amani.
“napenda kuwakukumbusha wananchi
wa mkoa wa Arusha kuwa suala la maendeleo sio la Serikali pekee bali ni
jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa nashiriki kikamilifu katika
shughuli za kujiletea maendeleo”alisema Mapunda.
Akizungumzia shule za Sekondari
za Kata amesema kuwa Serikali imejipanga kikamilifu na tayari umaliziaji
wa majengo ya maabara na vyumba vya madarasa uko katika hatua za mwisho
kabisa kukamilika na kuwataka wananchi kuepukana na dhana potofu kuwa
shule za Kata hazina viwango vizuri vya ufaulu wa wanafunzi.
Mapunda amesema kuwa Mkoa wake
umejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi hata mmoja
aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani ambaye atakosa
kujiunga na shule kwa uhaba wa vyumba vya madarasa kwani mkoa umejipanga
kikamilifu kukabiliana na changamoto hiyo.
Kuhusu suala la uchaguzi wa
serikali za mitaa alisema kuwa anashukuru uchaguzi huo umekwenda kwa
mafanikio na kuwa wananchi walipewa fursa zxa kuwachaguwa viongozi
wanaowataka.
“Kikubwa ni wananchi kupewa fursa za kuwachagua viongozi
wanowataka bila ya kuwepo
shinikizo hali ambayo imekuwa ikichangia uvunjifu wa Amani ndio maana
umeona mkoa huu hauna matukio ya uvunjifu wa amani kama ilivyokuwa
kabla”
No comments:
Post a Comment