Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma
Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kata ya Rasibura katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Tawi la Stendi huko Lindi Mjini tarehe
27.12.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha Lindi Mjini Mama
Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Tawi la CCM la Mbanja. Mama
Salma alitembelea tawi hilo tarehe 27.12.2014 kwa ajili ya kukagua kazi
ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.
Baadhi ya wajumbe wa Tawi la Chama Cha Mapinduzi Mabano katika Kata ya
Mbanja wakifurahia hotuba ya Mjumbe wa NEC Taifa wa Lindi Mjini Mama
Salma Kikwete wakati alipotembelea Tawi hilo tarehe 27.12.2014. Katibu
wa Shina la Wakereketwa Zahanati Kempu Ndugu Hidaya Chivi Ali
akikabidhi risala ya wanachama wa Shina hilo kwa Mjumbe wa NEC Taifa na
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 27.12.2014. Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha
Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na vijana na wananchi mara baada
ya kuzindua rasmi shina la wakereketwa Zahanati Kempu lililoko katika
Kata ya Rasibura tarehe 27.12.2014.
………………………………………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
Wakazi wa mkoa wa Lindi
wametakiwa kushikamana kwa pamoja, kufanya kazi kwa bidii na kuzitumia
rasilimali zilizopo ili kujiletea maendeleo.
Rai hiyo imetolewa jana Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia
wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika Mitwero Stendi Kata ya Rasibura wilayani humo.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema mkoa wa Lindi umejaliwa kuwa na
rasilimali nyingi ikiwa ni pamoja na zao la korosho, ardhi yenye
rutuba, bahari na gesi lakini bado kuna changamoto zinazowakabili
wananchi na hivyo kukwamisha maendeleo yao.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni
pamoja na elimu kwani baadhi ya wanafunzi wafikapo darasa la tano
wanaacha shule kwa ajili ya utoro, mimba za utotoni na vijana
kutokufanya kazi kwa bidii.
“Kuna baadhi ya watoto wakifika
darasa la tano wanaanza tabia ya utoro hakikisheni wanakwenda shule
kusoma kwani elimu itawasaidia katika maisha yao, msikubali waache
shule. Kutokana na umri wao mdogo wanaona raha kuacha shule na kwenda
kucheza lakini wakifika umri wa utu uzima ndiyo watakapoona umuhimu wa
elimu”.
Maisha bora kwa kila mtanzania
yanawezekana ikiwa kila mtu atapata elimu itakayomsaidia katika maisha
yake, wakati shule za Sekondari za Kata zinajengwa kuna baadhi ya watu
walitubeza na kuziita majina ya ajabu ikiwa ni pamoja na shule za
Yeboyebo lakini shule hizi zimewasaidia watoto wengi kutoka familia
maskini ambao wameweza kupata elimu”, alisema Mama Kikwete.
Kuhusu tazizo la mimba za utotoni
alisema ni hatari kwa maisha ya Mama na mtoto lakini kama kijana
atasoma mimba zitaepukika, jukumu la wananchi ni kuhakikisha watoto wao
wanasoma kwa bidii na kutokubali kupewa mimba ambazo zitawakatisha
masomo.
Kwa upande wa vijana MNEC huyo
aliwahimiza kuangalia mstakabali wa maisha yao na kutumia muda wao
kufanya kazi kwa bidii kwa kufanya hivyo watapata maendeleo kwani hizi
sasa kuna baadhi ya vijana wakati wa asubuhi wanaacha kwenda shamba
kulima na kucheza Pool kwa kufanya hivyo ni vigumu kupata maendeleo.
“Vijana wengine wanatumia madawa
ya kulevya na kuvuta sigara wanajua kwa kufanya hivyo ndiyo ujanja
kitendo ambacho siyo ukweli, bali unaharibu afya yako na kujirudisha
nyuma kimaendeleo. Kama wewe kijana unahitaji kuwa na maisha bora ni
lazima uachane na vitendo hivyo na kufanya kazi”, alisisitiza.
Licha ya kufanya mkutano huo wa
hadhara Mama Kikwete pia alifanya vikao na wajumbe wa Halmashauri kuu
ya CCM matawi ya Mbanja, Mabano na Mitwero Stendi na kuwataka wajumbe
hao kuwapa vijana nafasi za uongozi pale watakapojitokeza kugombea
nafasi hizo.
Pia aliwahimiza wajumbe hao
wakiwemo vijana, wanawake na wanaume kujitokeza kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo
mwakani ili kuwe na ushindani wa kutosha ndani ya chama.
Mama Kikwete yupo wilayani humo
kwa ajili ya shughuli za kichama na katika mkutano wa hadhara aligawa
kadi kwa wanachama wapya 23 walijiunga na Chama Cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment