HUYU NDIYE RAIS WA TANZANIA 2015.
: Urais
Sio Cheo, Urais ni Utumwa, Urais ni Msalaba Mzito, Rais anatakiwa kuwa
Mtumishi wa Watu kwa sababu anabeba Masalaba wa Watu Wote, Rais ni Baba
wa Watu Wote, anayetakiwa kuwajali Watoto Wake Wote, asiyekubali Kula
Wakati Kuna Watu Miongoni mwa Watoto Wake Wakilala na Kushinda Kwa NJAA,
IKULU NI MZIGO MZITO, watanzania Tayari Wenyewe Wameona na Kuyashuhudia
Maneno ya BABA wa TAIFA, na kila Uzito na Ujazo Wake, Kipimo cha Uzito
wa IKULU, ni Tofauti na Kipimo cha uzito wa nafasi Yoyote Kwa Uzani,
Kimawazo, Kiutendaji, na Uwajibikaji wa KILA mmoja Umeonekana,
Watanzania Siyo Karungu Yeye Kwamba Wao Vichwa kisha Watanzania ni
Magamba wanaingia na Kutoka, Nikichungulia tu niko nje na nikichungulia
tu niko ndani, KIRAIS RAISI, IKULU siyo mahala pa Kukimbilia ila SERA
ndo zinampeleka mtu IKULU, Wananchi wakishamkkubali, kwa SERA zake,
katika yale anayowambia wananchi kisha akayatakeleza na wananchi Watampa
URAIS, URAIS aununuliwi kama Karanga, Kwamba izi ni njugu Tutauziana
kwa Mafungu, URAIS wowote unaonunuliwa siku zote ikumbukwe ipo Siku
Utakuja KUUZWA, Tunapomchagua mtu kuwa Rais ni kwamba tunamwambia awe
mtawala wetu, awe juu yetu kwa Mamlaka ya kila jambo, mwenye maamuzi ya
Mwisho, mwenye kutenda juu ya HAKI na SHERIA, kwa Faida ya Wananchi
anatakiwa kutenda na si VINGINEVYO. IKULU SIYO PANGO LA WAFANYABIASHA,
IKULU SIYO SEHEMU YA KWENDA KUPUMZIKA, IKULU SIYO SEHEMU YA MISIKITI,
IKULU SIYO SEHEMU YA MAKANISA, IKULU SIYO SEHEMU YA MIGAO NA MIGAHAWA,
IKULU SIYO SEHEMU YA WAHUNI, NA IKULU SIYO SEHEMU YA MATAMBIKO, IKULU NI
MAHAPA PATAKATIFU. PA PATAKATIFU. RAIS ANATAKIWA KUWA MTAKATIFU ZAIDI
YA SALA NA IBADA, Mpenda AMANI, mtetezi wa haki, Mpigania Maendeleo ya
Watu Wake, Jemedari, Kamanda, Mwenye Nguvu Kimwili, Kiroho na Kimawazo,
asiyeyumbishwa na jambo, Mwenye kutoa Maamuzi Sahihi, Rais atakiwi kuwa
na Makundi, Rais atakiwi kuwa Mbaguzi, Rais atakiwi kuwa mwenye Uroho na
Madaraka, Rais atakiwi kuwa mchochezi, Rais atakiwi kuwa Mwenye Tamaa
na Uroho wa kujilimbikizia Mali, Rais atakiwi kuwa Mwenye Hasira na
Mwenye Maamuzi ya Haraka, Rais atakiwi kusema Uwongo, na Rais atakiwi
KUPANGIWA, Rais atakiwi kuwa na Ukabila,Rais atakiwi kuwa na Udini, Rais
atakiwi kuwa Muhuni, Rais atakiwi kuwa Mlevi, Rais atakiwi kutoa RUSHWA,
Rais atakiwi kupokea RUSHWA, Rais atakiwi Kulala Usiku na Mchana,
atakiwi kujulikana Muda wa Kulala na Mtu yeyote Isipokuwa kwa MKE/MUME
wake, Rais atakiwi kuwa mtu wa kusafiri safiri, atakiwi kuruhu au
kushiriki Uovu, Rais atakiwi kuzoeleka, Rais atakiwi kuipenda Nafsi yake
kuliko ya watu wake, NA URAIS hauna UMRI: 2015
No comments:
Post a Comment