Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini na
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa CCM wa Tawi
la Kilimahewa lililoko katika Kata ya Mwenge Ndugu Mohammed Madodo mara
baada ya kuwasili katika Tawi hilo kwa ajili ya mkutano na viongozi wa
Tawi tarehe 28,12.2014
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi
Mjini Mama Salma Kikwete akiwahutubia wajumbe wa Halmashauri ya Tawi la
Barabara ya Kawawa lililoko katika Kata ya Matopeni tarehe 28.12.2014.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama cha Mapinduzi anayewakilisha
Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akihutubia wajumbe wa Halmashauri ya Tawi
la Kilimahewa huko Lindi Mjini wakati wa ziara yake ya kuyatembelea
matawi ya CCM wilayani humo tarehe 28.12.2014.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma
Kikwete akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai aliyemtembelea Mama Salma kwenye Ikulu
ndogo huko Lindi tarehe 28.12.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
……………………………………………………………………
Na Anna Nkinda – Maelezo, Lindi
29/12/2014 Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi
mjini Mama Salma Kikwete amewataka vijana kuwa na msimamo na kutokubali
kutumika katika vurugu zinazohatarisha amani na usalama wa nchi.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alitoa rai hiyo hivi karibuni wakati
akifungua shina la vijana wakeleketwa la kikundi cha Zahanati Kempu
lililopo Kata ya Rasibura wilaya ya Lindi mjini.
Alisema vijana wengi hawajui
Historia ya nchi hivyo basi baadhi ya watu wasio na nia njema wanaitumia
nafasi hiyo kuwarubuni na kuwashawishi kufanya vurugu zinarudisha nyuma
maendeleo ya eneo husika.
“Msikubali mkoa wetu wa Lindi
kuwa kichaka cha majaribio na kutumika katika vurugu, kuweni na
msimamo wa kuitetea amani yetu kwani mkifanya vurugu matatizo
yanapotokea ninyi ndiyo mnaoangamia na hao waliowashawishi
wanawakimbia”.
Kama atakuja mtu hapa na
kuwashawishi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni sawa hakuna
atakayezuia tunahitaji kuwa na maendeleo katika mkoa wetu, lakini
kuwashawishi ili mfanye vurugu na kuharibu vichache tulivyonavyo
msikubali”, alisema Mama Kikwete.
Aidha MNEC huyo aliwasisitiza
vijana kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili waweze kujiletea maendeleo
yao na ya mkoa huo kwa kuwa vijana ndiyo wanaotegemewa na ni nguvu
kazi ya Taifa.
Akisoma taarifa ya kikundi hicho
Hidaya Chivii ambaye ni Mtunza fedha alisema kikundi hicho kilianzishwa
tarehe 5/7/2014 kikiwa na wanachama 23 kati ya hao wanaume ni 18 na
wanawake ni watano.
Chivii alisema madhumuni ya
kuanzishwa kwa kikundi hicho ambacho kinajihusisha na kazi ya kuendesha
pikipiki (bodoboda) kwa upande wa wanaume na ususi kwa upande wa
wanawake ni kujikwamua na hali ngumu ya maisha na kuweza kujiendeleza.
“Waendesha pikipiki tunakabiliwa
na changamoto ya kunyang’anywa pikipiki hasa ifikapo wakati wa uchaguzi
kwani wamiliki walio wengi ni wanachama wa chama cha Wananchi (CUF) na
sisi ni wanachama wa CCM au wanatupa pikipiki zao kwa masharti magumu
yakiwemo ya kukipigia kura chama chao”, alisema Chivii.
Alizitaja changamoto nyingine
zinazowakabili kuwa ni pamoja na kutokuwa na vitendea kazi vyao wenyewe
na kutokupata mafunzo ya ujasiriamali.
Wakati huo huo Mama Kikwete
alifanya vikao na viongozi wa Halmashauri kuu ya tawi ya CCM katika
matawi ya Kilimahewa na barabara ya Kawawa na kuwahimiza wajumbe
kuendelea kushikamana na kuwa kitu kimoja ili waweze kufanya kazi zao
kwa ufanisi zaidi.
Akiwa katika tawi la Kilimahewa
lililopo Kata ya Mwenge aliwapokea vijana wanne kutoka chama cha
Wananchi (CUF) ambao walijiunga na CCM.
Mama Kikwete ambaye ni mjumbe wa
NEC Taifa kupitia wilaya ya Lindi mjini yupo wilayani humo kwa ajili ya
kuimarisha kazi za chama hicho ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na
viongozi na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment