=========================================
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imewapongeza wasambazaji
na wadau wa filamu nchini kwa mchango wao mkubwa katika kuelimisha,
kuhabarisha na kufundisha maadili ya mtanzania huku wakichangia katika
pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua
mkutano wa serikali na wasambazaji wa filamu nchini jana jijini Dar es
Salaam kujadili uporomokaji wa bidhaa za filamu nchini.
“Tunathamini sana kazi mnayoifanya, Serikali inawajali na ipo
tayari kushirikiana nanyi kwa kazi nzuri mnayoifanya hivyo ni vema
kufanya mkutano huu kuwa wa kisanyansi kwa kuangalia gharama mnazotumia
kuandaa bidhaa za filamu ili kuweza kukua kibiashara na kukuza uchumi wa
nchi” amesema Pro. Gabriel.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bibi Joyce Fisoo amesema kuwa Bodi haitaruhusu bidhaa zilizo chini ya
kiwango kupelekwa kwa watanzania kwa daraja la bei ya chini pamoja na
soko huria kwani hakuna uhuria usio na mipaka.
Bibi Fisoo amesema kuwa wananchi
siyo dust bin wanapaswa kupelekewa kazi bora na zenye hadhi kwani Bodi
inahitaji kujiridhisha kuhusu viwango vya filamu hizo na kuheshimu fedha
za watanzania kwa kuwauzia kazi bora zinazoendana na thamani ya fedha
zao.
Aidha Mwenyekiti wa wasambazaji wa bidhaa za filamu nchini Bw.
Emmanuel Miamba amewataka wadau na wasambazaji wa filamu nchini kuwa
wakweli, wazalendo, pasipo kuogopa kitu chochote na kuangalia maslai ya
wasambazaji wote na kama wataona uwekezaji katika kazi za filamu haulipi
basi wawekeze katika masuala mengine na sio kushusha bei kuua tasnia ya
filamu nchini.
Naye Bw. Chacha Matula kutoka Jembe entertainment amewaomba
wasambazaji kuwa na umoja na mshikamano utakaowawezesha kushirikiana kwa
pamoja na serikali kusitisha uporomokaji wa bei za filamu na
kuwadhibiti watu wanaotaka kuua kampuni za wasambazaji wadogo nchini.
No comments:
Post a Comment