TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 13, 2014

SIMBA YAIKANDAMIZA YANGA 2-0, MASHABIKI LUKUKI WAZIMIA UWANJANI

 Kocha wa Simba, Patrick Phir akisalimiana na kocha wa Yanga, Marcio Maximo kabla ya mchezo.
 Emmanue Okwi akiomba dua wakati akiingia uwanjani.
 Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Yanga.
 Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji waSimba.
Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Simba.
Kocha wa Yanga akitafakari.

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akiwa amenyanyua juu
Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe msimu wa pili uliofanyika leo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-0. 

 Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Mchezo, Dk. Fenella Mukangala akimkabidhi nahodha wa Simba, Emmanuel Okwi Kombe la Ubingwa wa mechi ya Nani Mtani Jembe.
 Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Umati wa mashabiki wa Yanga.
 Umati wa mashabiki wa Simba.
Mashabiki wa Simba wakiwa wamebeba mfano wa jeneza kuwakejeli watani zao.
 Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’
 Beki wa Yanga, Kelvin Yondan akimiliki mpira.
 Mwamuzi wa mchezi akimuonyesha kadi ya njano mshambuliaji wa Simba, Simo Serunkuma.
 Hassan Isihaka (kushoto) ana Ramadhani Singano ‘messi’ wakishangilia bao la kwanza la timu yao.
Beki wa Yanga, Oscar Joshua akimtoka Elius Maguri wa Simba.
Shabiki wa Yanga akipata msaada baada ya kuzimia jukwaani.
 Mashabiki wa Simba wakiwa na bango lenye idadi ya mabao waliyowahi kufungwa Yanga.
Leo ni 2-0…..
Burudani zikitolewa uwanjani.
 Mashabiki wakitolewa uwanjani baada ya kuzimia.
 Hali ilikuwa ngumu kwa mashabiki mpaka baadhi yao kuzimia.
Huduma ya kwanza kwa waliozimia ikitolewa.
 Beki wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa Simba, Hassan Isihaka.
 Danny Mrwanda akiwa ameshika kichwa baada ya kukosa bao la wazi.
Ivo Mapunda akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Simon Msuva akichuana na Issa Rashid.
Ivo Mapunda (katikati) akishangilia ushindi na wenzake.
Wachezaji wa Yanga wakiwa na huzuni baada ya kumalizika kwa mchezo.
Yanga wakiwa vichwa chini.
 Medali za washindi.

WAKENYA WAWAFUNIKA WATANZANIA MICHUANO YA TENISI DAR OPEN

DSC_0453Mmoja wa wadhamini kutoka kampuni ya mawikili ya IMMA ya Dar es Salaam, Alexander Sarac, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania kwa udhamini mkuu wa kampuni ya magari ya CFAO Motors kupitia brandi ya magari ya Mercedes Benz.
Na Mwandishi wetu
WACHEZA tenisi kutoka nchini Kenya wamewafunika watanzania katika michuano ya kimataifa ya kwanza ya tenisi kwa walemavu (Dar Open ).
Michuano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa kesho katika viwanja vya Gymkhana, majira ya saa 10 ambapo washindi watapewa tuzo zao.
Kwa mujibu wa matokeo ya hadi mchana wakati mwandishi wa habari hizi anaondoka viwanjani hapo, mechi saba zilienda kwa wakenya kwa nafasi ya wanaume na wanawake na mbili ndio walishinda Watanzania.
Michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO, Mercedes-Benz na kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA imelenga pia kuandaa wachezaji kwa ajili ya mechi za kufuzu michezo ya dunia zinazotarajiwa kupigwa nchini Kenya Februari mwakani.
DSC_0413Mshiriki wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania, Rehema Selemani akirusha mpira wakati akichuana na mshiriki kutoka Mombasa, Phoebe Masika (hayupo pichani).
Kwa mujibu wa msemaji wa wadhamini wa michuano hiyo Alexander Sarac, michuano hiyo yenye washiriki wanaume 17 na wanawake watano walioitwa kutoka Tanzania na Kenya, imelenga kuwezesha walemavu kuendeleza vipaji vyao vya kucheza tenisi.
Pamoja na kuwa na ushindi dhaifu wa watanzania kocha wa timu ya Tanzania amesema bado ana bunduki zake mbili na ana hakika kesho vikombe vitabaki Tanzania.
Fungua dimba ya michuano hiyo ilianzishwa na watanzania Novatus Temba na Moses Sebastian ambapo Temba alimchapa Sebastian kwa seti 2-0; mkenya Itaken Timoi alimvuruga Bernad Antony kwa seti 2-0 huku Mkenya mwingine Peter Mnuve akimtoa Mtanzania Albert John kwa seti 2-0.
DSC_0376Katika michezo mingine Rajab Abdallah kutoka Kenya alimtoa Adil Hashim kwa seti 2-0 huku Yohana mwila wa Tanzania akimpa taabu Kenya ambaye alimuondoa kwa seti 2-1.
Muingereza anayeishi nchini Ian Artetiel alimtoa Mtanzania Voster Peter kwa seti 2-1.
Mkenya Caleb Odisyo alimchapa Mtanzania Wiston Sango kwa seti 2-0 wakati katika mechi za wanawake, Mtanzania Rehema Seleman alimsulubu bila huruma Asia Mohamed wa Kenya seti 2-0.Katika mechi nyingine Asia Mohamed alimchapa Bihawa Mustafa kwa seti 2-1.
Naye Lucy Shirima wa Tanzania alitandikwa na Phoebe Masika wa Kenya kwa seti 2-0.
Timu ya Tanzania ambayo kwa sasa ndiyo inayotamba Afrika Mashariki kutokana na michuano ya mwisho iliyofanyika Nairobiu kutwaa ushindi ina kazi ya ziada kulinda heshima yake.
DSC_0404Mshiriki kutoka Mombasa, Phoebe Masika akishiriki mashindano hayo.
DSC_0418Mtinange ukiendelea.
DSC_0499Mshiriki wa michuano ya tenisi ya walemavu ya kimataifa kutoka Tanzania Yohana Mwila (kushoto) akipeana mkono na mshiriki mwenzake kutoka Mombasa, Rajabu Abdallah mara baada ya kumaliza mchezo wa seti 3 ambapo seti ya kwanza Rajabu Abdallah ameshinda 4-3 na seti ya pili ameshinda Yohana Mwila 4-3 na ya tatu ubingwa ukienda kwa Yohana Mwila 10-3 katika kutafuta mshindi wa robo fainali kwenye michuano hiyo iliyodhaminiwa na kampuni ya magari ya CFAO Motors, kupita brandi ya Mercedes-Benz kama wadhamani wakuu na kampuni ya mawakili ya Dar es salaam ya IMMMA.
DSC_0421Ofisa wa Kitengo cha masoko na huduma wa CFAO Motors Ltd, Angel Ndege akiwa amejumuika na washiriki hao uwanjani hapo.
DSC_0423Baadhi ya washiriki kutoka Tanzania na Mombasa wakishuhudia wenzao wakiumana uwanjani.
DSC_0436Vikombe vitakavyokabidhiwa hapo kesho kwenye fainali za michuano hiyo.
DSC_0488Ofisa wa Kitengo cha masoko na huduma wa CFAO Motors Ltd, Angel Ndege na Kocha wa timu ya wachezaji tenesi Tanzania, Riziki Salum wakiangalia vikombe vitakavyokabidhiwa kwenye fainali za michuano hiyo itakayorindima hapo kesho kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
DSC_0433Mmoja wa wadhamini kutoka kampuni ya mawikili ya IMMA ya Dar es Salaam, Alexander Sarac (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau wa mchezo wa tenesi waliofika uwanja hapo kushuhudia michuano hiyo.

Martha Mwaipaja apania kuburudisha

SAM_3999
“TAMASHA linafanyika siku maalum ambayo Yesu Kristo amezaliwa, nitatoa huduma kwa njia ya uimbaji naomba wakazi wa mikoa yote mitatu wafike kwa wingi wale ambao hawanifahamu pia watanifahamu siku hiyo na wataguswa na kupata ujumbe uliotukuka,” anasema mwimbaji Martha Mwaipaja.
Mwimbaji huyo anasema kuwa amejipanga vilivyo ikiwa pamoja na kufanya maandalizi ya hali ya juu huku akisistiza kuwa atafanya makubwa katika tamasha la Krismasi ambalo litakuwa la pili kufanyika.
Mwaipaja anasema kuwa anawaomba mashabiki wafike kwa wingi kwa sababu amepewa nafasi hiyo ya kulihubiri neno la Mungu kupitia uimbaji hivyo yupo kwa ajili yao ni vema wakajitokeza kwa wingi kupata upako.
“Naimba kwa ajili ya kumtumikia Mungu, natoa huduma kwa njia ya uimbaji hivyo watanzania wajitokeze siku hiyo muhimu ya kuzaliwa kwa Yesu naamini watafurahi kwa jinsi ninavyofanya maandalizi ya tamasha hili kubwa ambalo limepangwa kufanyika siku yenye Baraka za Mungu,” 
Mwimbaji huyo anayevuma na nyimbo zake nyingi ambazo anatarajia kuziimba katika tamasha hilo la aina yake aliziita atakazoimba kuwa ni pamoja na Tusikate ‘Tamaa’ ambako alisema kuwa anaupenda wimbo huo kwa sababu wengi unawatia moyo.
Anasema kuwa  mbali ya wimbo huo ambao  upo kwenye albamu yake ya kwanza pia anatarajia kuimba wimbo wa ‘Ombi langu’ambao unapatikana katika albamu yake ya pili huku akifafanua kuwa maana ya wimbo huo kuwa mungu ametengeneza njia katikati ya aliowakumbuka nay eye yumo.

Rose Muhando na Kamata Pindo la Yesu kutawala

index
JINA la Rose Muhando ni mojawapo ya majina yanayofanya vizuri katika muziki wa Injili barani Afrika  hasa kutokana na uwezo wake jukwaani pindi anapofikisha uinjilishaji kwa waamini na mashabiki mbalimbali.
Muhando ni mzaliwa wa kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Tanzania, Afrika Mashariki na ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa lugha ya Kiswahili ambaye umahiri wake awapo jukwaani umefanikisha kutambulika barani Afrika. 
Rose atakayepanda jukwaani kuanzia Desemba 25, Agosti 3 mwaka huu alizindua albamu yake Kamata Pindo la Yesu yenye nyimbo za ‘Facebook’, ‘Bwana Niongoze’, ‘Wewe Waweza’, ‘Usiniache’, ‘Nibariki na Mimi’, ‘Usivunjike Moyo’ na ‘Kwema’. 
Awali Rose kabla hajawa Mkristo alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu. Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa anaumwa na yuko kitandani akiwa na umri wa miaka 9, aliugua kwa muda wa miaka mitatu na baadae alipona na kubadili dini na kuwa Mkristo.
Rose alizama kwenye muziki katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary’s katika kanisa la Kianglikana la Chimuli.
Januari 31 mwaka 2005, Rose Muhando alizawadiwa tuzo ya Mtunzi bora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na albamu Bora ya Mwaka. Tuzo hizo zilitolewa katika Tamasha Tanzania Gospel Music Awards, 2004
Desemba mwaka 2005 alihudhuria katika tamasha la Nyimbo za Injili katika kusaidia kuchangia kwa watoto na wajane Dar es Salaam ambapo alitekeleza ipasavyo uchangiaji huo.
Februari 2011, Rose Muhando alisaini mkataba na Mult Album Recording Deal na Kampuni ya Sony Music ya Afrika Kusini. Kusaini huko kulitangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Tanzania na hiyo ni mara ya kwanza kufanyika Afrika Mashariki.
Baadhi ya albamu za Rose Muhando ni:
1. Mteule uwe macho, 2004
2. Kitimutimu, 2005
3. Jipange sawasawa, 2008
4.Utamu wa Yesu 2012
4.Kamata Pindo la Yesu 2014
Tuzo alizopata
2005 -Tanzania Music Awards: Mwimbaji Bora wa Kike Nyimbo za Dini (“Mteule uwe macho”) 
2009 – Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili
2008- Alitunukiwa tuzo nchini Kenya ya Mwimbaji Bora wa Injili Afrika
Amewahi kuzawadiwa kitita cha Sh200,000 na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

Watakaopamba Tamasha la Krismasi

images
Na Mwandishi Wetu
WAKATI zikiwa zimebaki siku chache kuelekea Tamasha la Krismasi linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, wadau na waumini wa dini mbalimbali hapa nchini  wanatarajia kupokea neno la Mungu kupitia waimbaji wenye mvuto wa aina yake katika muziki huo ambao unafanikisha ukaribu baina ya Binaadamu na Mungu.
Ukaribu huo baina ya binaadam na Mungu pia unafanikishwa kupitia Wachungaji na Maaskofu mbalimbali watakaojitokeza katika tamasha hilo ambalo litafanyika kwenye mikoa ya Mbeya, Iringa na Ruvuma katika Wilaya ya Songea.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions ambayo inaandaa tamasha hilo, Alex Msama maandalizi ya tamasha hilo yamefanyika kwa asilimia kubwa kama viwanja na maeneo mengine muhimu yamekamilika.
“Maandalizi ya Tamasha la Krismasi mwaka huu yamefanyika kwa kiasi kikubwa, hivyo wadau wa muziki huo wajiandae kupokea injili kutoka kwa waimbaji na maaskofu mbalimbali watakaohudhuria,” alisema Msama.  
Tamasha la Krismasi lina lengo la kudumisha amani kwa Tanzania kwani mwaka huu Kauli mbiu  ya tamasha hilo ni “Tanzania ni ya Kwetu, Tuilinde na Tuipenda,” alisema Msama.
Kupitia Tamasha la Krismasi na Pasaka, vituo mbalimbali vya kulelea watoto wenye uhitaji maalum wanapata mahitaji muhimu kupitia viingilio vinavyopatikana.
Kampuni ya Msama Promotions haikuishia hapo imeenda mbali zaidi kwa kuelekeza nguvu zake zaidi kwa kujipanga kwa lengo la kujenga kituo cha Kimataifa katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Rafiki wa Wasiojiweza.
 Anasema Tamasha la Krismasi ni zao la Tamasha la Pasaka ambalo limeshika hatamu ya muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, ambako waimbaji mbalimbali kutoka katika nchi hizo wanashiriki kutoa huduma.
 Aidha Msama anawataja waimbaji watakaopanda jukwaani kwenye tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Bonny Mwaitege, Emmanuel Mgogo, Fraja Ntaboba, Solomon Mukubwa, Edson Mwasabwite, Upendo Kilahiro, Joshua Mlelwa, Tumaini Njole na Martha Mwaipaja.

Mgodi wa Resolute wakabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma, Masele asema tukio hilo limefungua ukurasa mpya

unnamedNaibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Stephen Masele (aliyesimama katikati) akishuhudia halfa fupi ya kusaini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Resolute Peter Beilby. Wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi (wa pili kuchoto aliyesimama),Mkurugenzi Kampuni ya Resolute Rose Aziz na baadhi ya waliohudhuria.
unnamed1Meneja Mazingira   baada Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair (Kulia), akimkabidhi funguo mbalimbali za majengo ya eneo la mgodi wa Resolute Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Madini) Stephen Masele (Kushoto) mara makabidhiano ya eneo la mgodi.
unnamed2Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe funguo mbalimbali za majengo ya mgodi wa Resolute kwa ajili ya Chuo cha Madini Dodoma.
unnamed6Meneja Mazingira wa Mgodi wa Resolute Jackie Sinclair akikabidhi moja ya vifaa ambavyo vitatumiwa na Chuo cha Madini Dodoma kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo wakati wa halfa ya kukabidhiana eneo la mgodi wa Resolute. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele, Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi
unnamed7Sehemu mgodi ambao shughuli za uchimbaji zilikuwa zikifanywa na mgodi wa Resolute ambao pia umekabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma. Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo Madini Dodoma Mjiolojia Mwandamizi Subian Chirangilwe ameeleza kuwa,mgodi huo utatoa fursa kwa wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu shughuli za uchumbaji.
…………………………………………………………………………..
Na Asteria Muhozya, Nzega Mgodi wa Resolute uliopo Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana tarehe 12 Desemba, 2014, ulikabidhi eneo la Mgodi kwa Chuo cha Madini Dodoma katika hafla fupi iliyofanyika na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia madini Stephen Masele aliyekuwa mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Bituni Msangi, Viongozi Waandamizi wa Wilaya ya Nzega, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Kamati ya Kitaifa ya uchimbaji, Uongozi wa Juu wa kampuni ya Resolute na wananchi. Akihutubia katika hafla hiyo, Naibu Waziri Masele alieleza kuwa, tukio la kukabidhiwa eneo hilo la Mgodi kwa Chuo ni tukio ambalo limefungua ukurasa mwingine kutokana na kwamba Chuo cha Madini Dodoma kitaiwezesha Tanzania kuzalisha wataalamu zaidi waliobobea katika tasnia hiyo ambao mchango wao kwa taifa unahitajika katika kuendeleza sekta ya madini. “Tunataka wanafunzi wasome kwa vitendo, hii itawezesha kupata wataalamu waliobobea. Ni nafasi kwa wanafunzi na Chuo cha Madini kuitumia fursa hii vizuri. Najua kuna mawazo mchanganyiko ya kupoteza mapato kwa Halmashauri na mengine ya kupata Chuo lakini, kufunga mgodi ni sehemu ya Sheria ya madini”, aliongeza Masele. Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bintuni Msangi, akizungumza katika halfa hiyo, alieleza kuwa, Mgodi wa Resolute una historia ya kuwa mgodi wa kwanza nchini kuzalisha madini ya dhahabu na kuogeza kuwa, ndani ya kipindi cha miaka 12 cha uhai wa mgodi huo umeweza kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 290 za Kitanzania ikiwa ni kodi mbalimbali zilizotolewa na mgodi huo kama mrahaba. Aliongeza kuwa, Halmashauri iliweza kupata kiasi cha shilingi bilioni 6 ikiwa ni kodi na kiasi cha Tsh bilioni 6 kilitumiwa na mgodi huo kuwezesha za kijamii ikiwemo ujenzi wa zahanati, shule, upatikanaji wa huduma safi ya maji katika eneo linalozunguka mgodi huo. Pamoja na eneo la mgodi huo kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini Dodoma, vilevile mgodi umekabidhi majengo, mitambo, maabara ambapo, kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo cha Madinini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile alieleza kuwa, eneo hilo litatumiwa na wanafunzi wa mwaka wa pili kwa ajili ya masomo ya vitendo. Mgodi wa Resolute umefunga rasmi shughuli zake za uchimbaji madini ya dhahabu katika eneo hilo, ambapo ulianza kazi zake mwaka 1998. Kabla ya makabidhiano hayo, mgodi huo umefanya ukarabati, ujenzi wa madarasa, na uhifadhi wa mazingira.