Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria
wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia) akimkabidhi
hundi yenye thamani ya sh. mil. 18.9, kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya
Gotam General Traders, Winner Taluka (wa pili kushoto) kwa ajili ya
kusaidia ukarabati wa miundombinu ya maji iliyoharibika baada ya Soko la
Mchikichini Ilala kuteketea kwa moto. Wanaoshuhudia hafla hiyo
iliyofanyika Dar es Salaam jana, kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
soko hilo, Rehema Matali, Mjumbe wa Kamati ya Maji katika soko hilo,
Christopher Mbowe pamoja na Kaimu Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilala,
Ulinyelusya Mwamtobe.
Kilindo akikagua kisima cha maji
ambacho miundombinu yake iliharibika baada soko hilo kuteketea. Kisima
hicho cha maji awali kilijengwa kwa msaada wa TBL.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria
wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto), akiangalia
chemba ambamo kuna pampu ya maji iliyoharibika wakati wa janga la moto
lililoteketeza Soko la Mchikichini Ilala, Dar es Salaam, ambapo jana
kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa sh. mil. 18.9 za kukarabati
miundombinu ya maji katika soko hilo lenye wafanyabiashara wanaokadiriwa
7000.
Kaimu Mweka hazina wa Manispaa ya Ilala, Mwamtope akitoa shukurani kwa TBL kwa msaada huo wa kukarabati miundombinu.
Kilindo 9wa pili kulia) akijadiliana jambo na Rehema Matali kuhusu kalo linalotumiwa na Mama Lishe, Baba Lishe kuoshea vyombo
Moja ya mabomba yaliyoharibika na kutakiwa kufanyiwa matengenezo
Kilindo akitoka kukagua miundombinu ya maji katika soko hilo
No comments:
Post a Comment