MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA
NTOKELA WILAYANI RUNGWE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA CHESCO MAHENGE (41)
ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA
WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KANDO
YA BARABARA KWENYE MASHAMBA YA CHAI MNAMO TAREHE 07.12.2014 MAJIRA YA
SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAPINDUZI, KIJIJI CHA
NTOKELA, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA
MBEYA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA NA MICHUBUKO SEHEMU ZA MGONGONI.
INADAIWA KUWA MNAMO TAREHE
06.12.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE
AKIAGA KUWA ANAKWENDA MATEMBEZI KIJIJINI HAPO. CHANZO CHA MAUAJI
KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA MAREHEMU ALIKUWA
ANATUHUMIWA KWA TABIA YA WIZI KIJIJINI HAPO SIKU ZA NYUMA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE
DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA
SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA
TUHUMA MBALIMBALI KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA
NDAGA WILAYANI RUNGWE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ZELII MWAITAVILA (70)
ALIFARIKI DUNIA AKIWA ANAJIUGUZA NYUMBANI KWAKE ANAPOISHI PEKE YAKE
BAADA YA KUSHAMBULIWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.
MAREHEMU ALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA
MNAMO TAREHE 27.11.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI NYUMBANI KWA HAMIS
MATEO NA KURIPOTI KITUO CHA POLISI NA KUFUNGUA KESI KISHA KUPEWA PF.3.
HATA HIVYO HAKURUDI TENA POLISI HADI ZILIPOPATIKANA TAARIFA ZA KIFO
CHAKE.
WATUHUMIWA WAWILI AMBAO NI 1.
HAMISI MATEO (41) NA 2. SAMWEL SAMSON MWANAWAMBUGA (47) WOTE WAKAZI WA
KIJIJI CHA NDAGA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA
KATIKA TUKIO HILO. CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA
YA WATUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA NI MCHAWI.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUALAJE WILAYANI CHUNYA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MASUNGA LUSEBELO (23) AKIWA NA POMBE YA MOSHI
UJAZO WA LITA 03.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
07.12.2014 MAJIRA YA SAA 13:50 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA SUMBWE,
KIJIJI NA KATA YA LUALAJE, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA
WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI
MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA
NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment