Mkuu
wa Wilaya ya Mpanda Mkoani KATAVI Paza Mwamlima mwesnye suti ya
bluuakipata maelezo toka kwa wataalam wa mifugo baada ya kuzindua
Mtambo wa Kuzalisha Kimiminika cha Nitrogeni Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda,wengine ni wataalamu wa mifugo Laurensi Eliasi ayelivaa Tishiti
ya mistari na Mzozomo Mbogo. Hapo
Mzozomo Mbogo akimpatia maelezo Mkuu wa Wilaya namna mtambo unavyofanya
kazi na Faida zake kwa Halmashauri wafugaji na Taifa kwa ujumla .
(Picha zote na Kibada Kibada-Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Mpanda.)
………………………………………………………………………………………………
Na Kibada Kibada-Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani
Katavi Paza Mwamlima amezindua Mtambo wa Kuzalisha Kimiminika cha
Nitrogeni utakaotumika katika kuhifadhi mbegu bora za mifugo kwa ajili
ya uhamilishaji mifugo na kuwezesha upatikanaji wa kosaafu za ng’ombe
zenye tija.
Akitoa Taarifa ya Mtambo huo,
kwa Mkuu wa Wilaya Afisa Mifugo kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi
Laurensi Elias ameeleza kuwa Mtambo huo uliletwa na Wizara ya Mifugo
na Uvuvi tangu mwezi juni mwaka huu na usimikwaji wake umekamilika mwezi
septemba mwaka huu shughuli iliyofanywa na Kampuni ya Cooporation Group
Ltd
Amesema gharama za Mtambo huu
hadi kufukishwa Wilayani Mpanda umetumia kiasi cha shilingi milioni 400
pamoja na gharama za usimikaji zilizogharimu kiasi cha shilingi milioni
37.2 hivyo kufanya jumla yote kuwa shilingi milioni 437.290,950/-
Mtambo huo ni aina ya Cryomech
120 una uwezo wa kuzalisha lita 5 kwa saa, kiasi hiki huzalishwa baada
ya muda wa kuwa tayari takribani saa nne baada ya mtambo kuwashwa.
Ili mtambo uweze kuanza kazi
kinahitajika kiasi cha shilingi milioni 39.7 kwa ajili ya kununulia
vifaa na gharama ya kuwapeleka watalaam kwenye mafunzo ili waweze
kusaidia kuendesha mtambo huo.
Amefafanua kuwa Ili mtambo
ufanye vizuri ni lazima mambo ya umeme sahihi na wa kutosha uwepo, mfumo
sahihi wa maji ya kutosha kwa ajili ya kupooza mtambo wakati wa
uzalishaji,uwepo wa mzuunguko mzuri wa hewa ya kutosha isiyo na joto
pamoja na usafiwa kutosha kuzuia vumbi inayoweza kuathiri mtambo.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Mpanda Estomihn Chang’ah ameeleza kuwa mtambo huo ni wa
kisasa na hapa nchini ni unapatikana katika Mkoa wa Arusha,Iringa na
Mbeya Pekee na huu ulioletwa katika Halmashauri ya wilaya ya Mpanda
utasaidia sana kuhudumia,Mikoa ya Kigoma,Rukwa Tabora,Mbeya na Iringa
nao watanufaika na mtambo huo kwa kuboresha mifugo kwa njia ya
uhamilishaji.
Aidha utaongeza kipato cha
Halmashauri kwa njia ya kuuza kimiminika katika taasisi mbalimbali kama
Hospitali na maeneo mengine ya jirani na mapato yatokanayo na gharama
za uzalishaji,Pia utainua kipato cha Taifa na wafugaji kwa kuuza ng’ombe
waliobora na wenye tija kuboresha lishe ya mwananchi.
Pia itapunguza maambukizi ya
magonjwa ya mifugo yanayotokana na kupandisha ng’ombe kwa kutumia madume
mfano ugonjwa wa kutupa mimba.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Mpanda Paza Mwamlima ameshauri Halmashauri kujenga urafiki na
wafugaji kwa kuwapa elimu ili wawe pamoja wafugaji wote na utoaji wa
huduma kwa kutumia mitambo huo utakuwa natija tofauti na sasa wafugaji
wakiwaona watalaam wanawakimbia wanakuwa kama maadui.
Elimu itolewa kwa wafugaji waone mtambo huo kuwa utawasaidia kubadili hali ya ufugaji wao.
No comments:
Post a Comment