KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha
la Krismasi iliyo katika kampuni ya Msama Promotions, imetangaza
kiingilio cha shilingi 5000 kwa wakubwa katika tamasha hilo katika mikoa
ya Nyanda za Juu Kusini, linalotarajia kuanza Desemba 25-28.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Abihud Mang’era watoto katika tamasha hilo watachangia shilingi 2000 ambako alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Mbeya, Iringa na Songea kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.
Mang’era alisema tamasha hilo Desemba 25 litafanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Sokoine, Desemba 26 litafanyika mkoani Iringa kwenye uwanja wa Samora na Desemba 28 Wilayani Songea kwenye uwanja wa Majimaji.
Aidha Mang’era alisema viingilio hivyo vitakidhi haja ya wakazi wa mikoa hiyo wenye kiu ya kupata neno la Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini watakaojitokeza kwenye tamasha hilo.

No comments:
Post a Comment