“TAMASHA linafanyika siku maalum
ambayo Yesu Kristo amezaliwa, nitatoa huduma kwa njia ya uimbaji naomba
wakazi wa mikoa yote mitatu wafike kwa wingi wale ambao hawanifahamu
pia watanifahamu siku hiyo na wataguswa na kupata ujumbe uliotukuka,”
anasema mwimbaji Martha Mwaipaja.
Mwimbaji huyo anasema kuwa
amejipanga vilivyo ikiwa pamoja na kufanya maandalizi ya hali ya juu
huku akisistiza kuwa atafanya makubwa katika tamasha la Krismasi ambalo
litakuwa la pili kufanyika.
Mwaipaja anasema kuwa anawaomba
mashabiki wafike kwa wingi kwa sababu amepewa nafasi hiyo ya kulihubiri
neno la Mungu kupitia uimbaji hivyo yupo kwa ajili yao ni vema
wakajitokeza kwa wingi kupata upako.
“Naimba kwa ajili ya kumtumikia
Mungu, natoa huduma kwa njia ya uimbaji hivyo watanzania wajitokeze siku
hiyo muhimu ya kuzaliwa kwa Yesu naamini watafurahi kwa jinsi
ninavyofanya maandalizi ya tamasha hili kubwa ambalo limepangwa
kufanyika siku yenye Baraka za Mungu,”
Mwimbaji huyo anayevuma na
nyimbo zake nyingi ambazo anatarajia kuziimba katika tamasha hilo la
aina yake aliziita atakazoimba kuwa ni pamoja na Tusikate ‘Tamaa’ ambako
alisema kuwa anaupenda wimbo huo kwa sababu wengi unawatia moyo.
Anasema kuwa mbali ya wimbo huo
ambao upo kwenye albamu yake ya kwanza pia anatarajia kuimba wimbo wa
‘Ombi langu’ambao unapatikana katika albamu yake ya pili huku akifafanua
kuwa maana ya wimbo huo kuwa mungu ametengeneza njia katikati ya
aliowakumbuka nay eye yumo.
No comments:
Post a Comment