DC Mpanda Paza Mwamlim akiwahutubia wafugaji
katika kijiji cha Sibwesa Wilayani Mpanda na kuwasisitiza umuhimu wa
hifadhi mazingira na kuwaasa wafugaji.
kupunguza mifugo yao wafuge ufugaji wenye tija,
Baadhi ya maeneo yaliyoathiliwa
na uharibifu wa mazingira kutokana na wingi wa Mifugo Katika Halamshauri
ya Wilaya ya Wilaya ya Mpanda.(Picha na Kibada Kibada Katavi
………………………………………………….
Na Kibada Kibada –Katavi
Makala
Sekta ya Mifugo Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi inakabiliwa na Changamoto mbalimbali
hali inayofanya sekta hiyo kutafuta mbinu na mikakati ya kukabiliana na
changamoto hizo ikiwemo uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na wingi
wa mifugo uliopo kuliko ukubwa wa eneo la kufugia mifugo hiyo.
Baadhi ya Changamoto hizo ni
kuwepo idadi kubwa ya mifugo katika halmashauri,Uzalishaji mdogo wa
mazao ya mifugo kama nyama na maziwa na kipato kinachotokana na uwepo wa
mifugo hiyo katika Halamshauri.
Changamoto nyingine ni
upatikanaji mdogo wa mbegu bora za mifugo hususani ng’ombe,eneo dogo la
malisho ukilinganisha na Idadi ya mifugo iliyopo kwenye Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda.
Pamoja na kuwepo kwa wingi wa
mifugo pia magonjwa mengi ya mifugo kama ndorobo,ndigana kati na homa
ya mapafu nayo ni moja ya changamoto inayoikabili sekta ya mifugo Katika
Halmashauri ya Mpanda.
Halmashauri ya Mpanda ambayo ni
moja ya Halmashauri katika Mkoa wa Katavi ina idadi ya Ng’ombe wapatao
87,928,mbuzi 44,348,Kondoo 8,712,Nguruwe 2,237, mbwa 7425,na kuku
141.832 hata hivyo uwepo wa mifugo hiyo bado haijatumiwa vizuri na
kubadili maisha ya wakazi wa Halmashauri hiyo na mkoa kwa ujumla
kiuchumi na kuinua pato lao kiuchumi.
Tafiti zinaonesha iwapoidadi ya
mifugo hiyo iliyopo ikitumiwa vizuri inaweza kuleta tija na kuwaondolea
umasikini wananchi katika maeneo husika.
Kwa mantiki hiyo wataalam wa
sekta ya mifugo wanayo kazi kubwa mbele yao kuhakikisha wanatumia elimu
yao kuwabadili wafugaji waweze kufuga ufugaji wenye tija tofauti na
ilivyo kwa sasa ambapo ufugaji umekuwa wa kutokuwa na tija na kila
kukicha imekuwa ni mivutano na migogoro kati ya wakulima na wafugaji
ingawa hali hiyo bado haijatokea katika Halmashauri ya Mpanda lakini
tunashuhudia maeneo mengi hapa nchini hususani Mkoani Morogoro,wilaya ya
Kilosa na Kilombero,Mkoani Pwani ,na Arusha na Tanga wakulima na
wafugaji migogoro ya kila mara.
Uwepo wa mifugo mingi katika
Halamshauri ya wilaya ya Mpanda pia kumeambatana nanUharibifu wa
mazingira kutokana na wafugajinhao kuhamahama na wengine kutumia njia
hiyo kwa kufyeka miti na mistu kwa shughuli za kilimo kwa kuwa wafugaji
walioko katika Halmsahauri ya Mpanda hao hao ndio wakulima.
Uchunguzi uliofanyika kwa baadhi
ya maeneo Mbalimbali Wilayani Mpanda inaonesha maeneo mengi
yanaoonekena kuathiri na Uharibifu wa mazingira na iwapo hatua za
makusudi hazitachukuliwa kwa haraka maeneo hayo yanaweza kugeka jangwa.
Baadhi ya maeneo yaliyoathirwa
na uharibifu wa mazingira kutokana na mifugo ni bonde la Mto Katuma
ambao ni tegemeo kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi hususani Mbuga ya Katavi
ya Katavi ambayo wanyama walioko huko hutegemea kupata maji kutoka bonde
la mto huo ambalo hutiririsha maji yake kupitia vijito vyake kupeleka
hifadhi ya Katavi.
Mbali ya kutegemewa kwa ajili ya
maji ya wanyama kama viboko na wengineo pia bonde la mto huo wa Katavi
ndilo linalotegemewa kwa kilimo cha mbuga unaozalishwa kwa wingi katika
maeneo ya Bonde hilo na kuwasaidia kuwaingizia pato wananchi Mkoani
humo.
No comments:
Post a Comment